Dondoo za kuwa msafi na mtanashati

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,676
Reaction score
861,008
Ni mara chache mno kukutana na mwanamke anayependa mwanaume mchafu, anayenuka jasho mwenye aleji na maji
vijana wanapenda utanashati ili wawe kivutio kwa wengine hasa wanawake, lakini kuna watanashati lakini sio wasafi, kwa nje wamependeza lakini ndani loh...majanga full fungus ukimwambia avue soksi mtagombana
UWAPO MTANASHATI ZINGATIA PIA HAYA YA USAFI

1:MAPELE USONI, ni tatizo kwa wanaume wengi na wanafikiri ni maradhi kumbe ni uchafu
kidevu kinabeba nongo jasho na mafuta yote yanayotiririka usoni hivyo unyoapo zingatia haya
_usitumie wembe zaidi ya mara mbili
_safisha kidevu chako kwa maji ya moto kabla na baada ya kushave
_kiwembe cha kidevuni usikitumie kunyoa kwingineko
_tumia gillete au bic au brand nyingine yoyote nzuri
_safisha kidevu kila ulalapo
_kama una dalili ya mapele kidevuni, kisugue kidevu kwa mswaki laini kisha paka ndimu
_PAKA MAFUTA YA NAZI


2:FUNGUS SEHEMU ZA SIRI,hii husababishwa na uchafu, unaoga mwili wote lakini huko chini unakusahau, fanya hivi kutibu tatizo
_usivae chupi mbichi au yenye unyevu
_shave at least twice a week
_usivae chupi zaidi ya mara moja
_oga kila ulalapo
_kina uogapo sugua kende na maeneo yanayozizunguka kwa kitaulo kisha suuza vema
_kausha vizuri PAKA MAFUTA YA NAZI
_lala uchi au vaa bukta nyepesi kuvipa vifaa nafasi ya kupumua
_usilale bila kujiswafi ufanyapo ngono

3:FUNGUS MIGUUNI NA MIGUU KUNUKA, hali ya TANZANIA ni ya kitropiki hivyo kuna joto mno, viatu tuvaavyo vingi ni semi leather hivyo kuifanya miguu ipumue mno
fanya hivi
_ jitahiti kuwa na pair zaidi ya moja za viatu
_usirudie soksi
_usivae soksi mbichi au nyevu
_kila uogapo jitahidi kusugua kati kati yavidole kwa kitaulo kidogo
_hakikisha unakausha miguu vizuri kabla ya kuvaa soksi
-PAKA MAFUTA YA NAZI
kwa jinsi hiyo utakuwa umetatua matatizo makubwa matatu na kuokoa pesa nyingi, utaulamba kwa nje lakini pia ndani utakuwa uko njema, hata sweetie akitaka kuzama hutaona noma kupanua miguu, au ukienda kwa mama mkwe hutaona noma kuvua viatu
 
Asante,,,, bora ww umesema maana hali ni mbaya!!!!!!
Ongezea na jinsi ya kupiga mswaki wengine midomo tatizo hakafu full kujifanya anapenda denda!
 
Na sie tunaovaa majeans ofisini unatuweka kundi gani?

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
well kijana umetisha..
 
Ntasave hizo data soon... Good deeds indeed!
 
..umefanya vizuri kukumbushia..wanajua yote ila kuna baadhi wanapuuzia... na utanashati mzuri ni ule unaoambatana na usafi
 
pedicure muhimu mkuu...
 
Utakuwa umeokoa mahusiano mengi ya watu kwa uzi huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…