Mwafrika anafaidika vipi kwenye ushindi wa Democratic au Republican.
Afrika itakuwa wapi?
Wamerekani wenye asili ya Afrika, walifanya mkutano mkubwa sana siku chache zilizopita, walisema wamempigia kura, wamemshangilia na kufurahia kuwa na Rais wa kwanza mwenye asili ya Uafrika yaani "Mtu mweusi", lakini hawajaambulia lolote. Inasemekana Waafrika wamekuwa na wakati mgumu sana, kudhalilishwa katika kipindi hiki cha miaka 4 ya Utawala wa Obama.
Hili sio suala la ubishi, hili suala linatakiwa kuangalia ni sera za mambo ya nchi za nje za Marekani, kuna zingine hazibadili hata kama Clinton, Mweusi au Mweupe awe Rais.
Tuwe makini sana na Bara letu, Usalama wa Bara letu, Mali zetu, Maslahi ya watu wetu na kizaji kijacho.
Tunatakiwa tutoe viongozi wanaopenda Afrika yetu na watu wake, na wako tayari kutumia mabilioni ya pesa zao wenyewe kutetea Afrika yetu, kama Bwana Trump.
Tabia ya Mbwa koko yakusubiri misaada na kupewa masharti lazima iishe.
Afrika itanyanyuka tuu. Jasho na damu ya Mwafrika itakuwa na thamani siku moja.
Waafrika wataheshimiwa na watapewa hadhi kama binaadamu wengine tuu. Ushindi wa Mwafrika unakuja.