Dola yamtisha mwandishi wa Mwananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dola yamtisha mwandishi wa Mwananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bei Mbaya, Aug 27, 2011.

 1. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Mwandishi wa habari anayealindikia gazeti la Mwananchi kutokea Arusha, Mussa Juma, ameanza kuandamwa na Serikali na sasa uraia wake umeanza kuhojiwa huku yeye akihusisha hatua hizo na msimamo wake katika kazi zake.

  Habari zilizothibitishwa na vyombo vya dola zimeeleza kwamba Mussa amekua akifuatiliwa kwa muda mrefu sasa kabla ya kuitwa na kuhojiwa rasmi na vyombo vya dola akituhumiwa kuwa uraia wake una utata.

  Mbali ya kuandika habari za uchunguzi na zile za kisiasa, Mussa amekua mstari wa mbele katika kuwaunganisha waandishi wa habari mkoani Arusha na mikoa jirani ya Manyara na Kilimanjaro, lakini pia amekua kiungo na waandishi wageni wanaotembelea Arusha.

  "Baada ya kuripoti kwa kina utata katika tukio la uchaguzi wa Meya na vurugu zilizosababishwa na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mapema mwaka huu, nilianza kuandamwa na baadhi ya watendaji wa Idara ya Usalama wa Taifa ambao walinionya niache kuandika habari za matukio hayo la sivyo ‘nitakiona'," alisema Mussa Juma.

  Kilele cha vitisho na ujumbe alizotumiwa kilifika juzi baada ya maafisa wa Idara ya uhamiaji Arusha kufika ofisi za gazeti la Mwananchi kumtafuta Musa na walipomkosa walimpigia simu yake ya kiganjani wakimtaka kufika ofisini kwao siku inayofuata, Agosti 23, 2011, saa 3 asubuhi bila kumweleza sababu za wito huo.Alisema pamoja na tukio la umeya, afisa huyo pia alimtuhumu kuishambulia na kuiumbua Serikali katika tukio la mgogoro wa jamii ya Wamaasai wa eneo la Lololiondo Wilayani Ngorongoro na kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Oterllo Business Co-Operation (OBC) na pia mgogoro wa Mashamba ya NAFCO Wilayani Hanang.

  Kilele cha vitisho na ujumbe alizotumiwa kilifika juzi baada ya maafisa wa Idara ya uhamiaji Arusha kufika ofisi za gazeti la Mwananchi kumtafuta Musa na walipomkosa walimpigia simu yake ya kiganjani wakimtaka kufika ofisini kwao siku inayofuata, Agosti 23, 2011, saa 3 asubuhi bila kumweleza sababu za wito huo.

  Akiwa ameongozana na wakili wake, Shilinde Ngalula, na mmoja wa wafanyakazi wa Mwananchi mkoani Arusha, Peter Saramba, Mussa alifika ofisi za uhamiaji na kutakiwa kutoa maelezo lakini Ofisa huyo wa uhamiaji alikataa kufanya mahojiano mbele ya Mwanasheria na Mfanyakazi wa Mwananchi, jambo lililozua mgogoro uliodumu kwa muda wa saa mbili.

  Alisema kama vyombo vya dola vinaona kuwa uandishi wake na mwenendo ya gazeti la Mwananchi si sahihi kuna taratibu za kufuata ili madai yao yafanyiwe kazi, "Nimekuwa mwandishi kwa zaidi ya miaka 15 sasa sijawahi kushitakiwa kwa kuandika habari zozote za uchochezi au kupotosha sasa nashangaa vitisho dhidi yangu," alisema Mussa Juma.


  chanzo: FikraPevu
   
 2. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Mfamaji haishi kutapatapa, ndo serikali yetu hii iliyo legelege kama mlenda,
  Mwisho wao unakuja tuu, kifo chao kipo karibu mno.
  Wanasheria wajipange tuu kumtetea kwenye hayo wanayotaka kumsingizia
  kama ni kweli.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hata KARL MARX alifukuzwa ujeruman kwa sababu alikuwa ni mhariri ambae ni radical,,,so mim nachoamin ni kuwa amewagusa sana hao watawala,,,,,,haya ni ya ULIMWENGU
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kila mtu ana haki ya kuhojiwa mbele ya mwanasheria wake na sheria ipo wazi kuhusu hivo na ni haki yake ya msingi hakuna mtu anaeweza kumnyanganya haki hiyo sasa inakuwaje ofisa uhamiaji akatae kumhoji mbele ya mwanasheria wake kama sio mambo ya kisongombingo??? yaelekea ofisa uhamiaji yupo juu ya sheria, nampa pole mwandishi aendelee kufanya kazi bila zengwe wala asife moyo tupo nyuma yake.
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nimeongea na wakili wa Mussa Shilinde Ngalula kuwa ni kweli jamaa walilumbana takribani masaa mawili hoja kubwa ikiwa ni Mussa kutoa maelezo mbele ya waandishi wa habari. Aliyekuwa akimhoji Mussa ni DCP wa Uhamiaji Mwanguku ambapo aliishia kwa kujaza fomu fulani ambayo ingetoa particulars za Mussa.

  Duuuuuuh kazi kweli kweli.
   
 6. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Mpaka hapo usalama wa taifa watakapojitenga na chama tawala ndipo tutashuhudia mabadiliko yakiutawala(sitaki kusahihishwa kwa hili)
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Mwanza wamemuua Massatu, haitutishi, tutaendelea kuandika na kuumbua kila udhalimu wa serikali hii legelege
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sitak kukupinga gudgooD
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ati??????hu iz massatu????
   
 10. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ni haki ya raia tu.
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Nakuunga Mkono hoja kwa 100%

   
 12. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  jamani arusha nzima anaandika mwandishi mmoja msipende kufikiri kimasaburi , yeye anauhakika ni raia apeleke vielelezo si watamuacha . Watendaji wakitimiza wajibu mnawazonga wasipotimiza Kelele.

  Cha msingi rungu hilo liwadondokee na wahamiaji haramu waliozagaa maeneo mbali mbali nchini isiwe mwandishi huyo pekee zoezi lisimame
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  .. Dola ya Gaddafi ..ilifanya haya haya!!!
   
 14. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  kiburi chao kimeegemea hapo
   
 15. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Wametoka Saed Kubenea sasa wamehamia kwa Mussa
   
 16. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Sakata la uchunguzi wa uraia wa mwandishi wa gazeti la Mwanananchi mkoani Arusha, Mussa Juma, limeendelea kuchukua sura mpya baada ya maofisa uhamiaji kuvamia nyumbani kwake na kumhoji mama yake mzazi kwa zaidi ya saa mbili.

  Akizungumza nyumbani kwa Mussa, eneo la Sakina Kiranyi, wilayani Arumeru jana, mama mzazi wa mwandishi huyo, Amina Ramadhani (65), alisema maofisa hao licha ya mambo mengine, walitaka kujua alipozaliwa, lini walioana na mumewe na asili yao, "Pamoja na kuhoji nilipozaliwa mimi na mume wangu, pia walitaka kujua tarehe na mahali alipozaliwa Mussa, shule ya msingi, sekondari na chuo alikosoma na nafasi yake kitaaluma Kampuni ya Mwananchi," alisema Amina.
  Alisema alilazimika kuwahoji maofisa hao watatu walioongozwa na mwenzao aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwamboka, iweje wanafuatilia uraia wa Mussa pekee ambaye ni mtoto wa 9 kati ya 12, aliowazaa lakini wakamjibu kuwa wao wameagizwa kumchunguza mwandishi huyo pekee.

  Kwa mujibu wa Amina, mumewe alikuwa mtumishi wa Serikali idara ya ujenzi tangu ujana wake hadi mwaka 1993 alipostaafu wilayani Maswa. Akizungumza kwa simu jana, Mwamboka alisema hawezi kuongelea suala hilo kwa sababu siyo msemaji, huku akielekeza atafutwe ofisa aliyemtaja kwa jina la Kingdom, anayepatikana chumba namba moja ofisi za uhamiaji mkoa.

  Hatua ya Mussa kuchunguzwa uraia wake, inadaiwa kuwa shinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa idara za Serikali wasiopendezwa jinsi anavyoripoti habari zinazohoji uhalali na taratibu mbalimbali zinazochukuliwa na dola, hasa mgogoro wa kisiasa kuhusu umeya Manispaa ya Arusha.

  source: Mwananchi
   
 17. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ww ni Mtanzania kweli, hebu connect dot to dot juu ya kilichoandikwa.Wangapi walishika nyadhifa nyeti katika nchi hii badae wakaambiwa sio watanzania.Muulize Jenerali Ulimwengu. Uhamiaji, Usalama wa Taifa ni vibaraka wa viongozi.Malalamiko mangapi wamepelekewa kuhusu wageni wasio na vibari vya kufanya kazi nchini lakin wako kimya.
   
 18. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2011
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 811
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Tatizo kubwa lipo katika huu mfumo wa hizi Taasisi zetu kuanzia hao TISS na utitiri mwingine kutokumbambua wanamtumikia nani?
  Naamini wengi wao wanaamini kwamba wapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya magodfather wao
  TUNA KAZI KUBWA WATANZANIA WENZANGU YA KUJIKOMBOA
   
 19. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2011
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 811
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Tatizo kubwa lipo katika huu mfumo wa hizi Taasisi zetu kuanzia hao TISS na utitiri mwingine kutokumbambua wanamtumikia nani?<br>Naamini wengi wao wanaamini kwamba wapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya magodfather wao<br>TUNA KAZI KUBWA WATANZANIA WENZANGU YA KUJIKOMBOA
   
 20. K

  Kampemba Member

  #20
  Aug 29, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Embros Kingdom Mwanguku(DCI) the Great:Kwa huyu mutu Mussa uka na job,hamalizagi kesi msumbufu,unatakiwa ujipange sana lasivyoo hakiyako itapotea maana huyo alie kamata hiyo kesi yako alisha ugua kichaa sasa ugunjwa huu unatabia ya kujirudia rudia kuringana na miezi kwa huu kwake ni mwezi mchanga sasa hapo subiri timbwili hilo uliloliona mbado.
   
Loading...