Dola bei juu, kulikoni thamani ya shilingi?!

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,168
1,071
Wiki hii inaonekana sarafu yetu inazidi kuporomoka..
Bei ya dola inazidi kupaa ..kulikoni thamani ya fedha yetu..

Uthibiti wa matumizi holela ya fedha za kigeni wapaswa kutekelezwa kwa vitendo...
Kodi za nyuma,ada za shule,uagizaji bidhaa,malipo ya huduma mbalimbali...

Wenzetu Afrika Kusini wameweza na wamefanikiwa kwa kiwango kikuu kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni ndani ya nchi yao..Imewasaidia sana kuujenga uchumi wao,kuudhibiti uchumi wao..
 
Ni tatizo la sarafu zote ambazo zinaitegemea Dollar. Kenya pia pamoja na shilling yao kuwa stronger dhidi ya TZS lakini inapoteza thamani dhidi ya Dollar pia. Sababu kubwa wanadai ni matokeo ya policies za Don Trump. Tuamke!
 
Umeongea point sana mkuu maana bila kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni kwetu hapa lazima tutaangukia pua. South Africa ukitaka kubadili fedha za kigeni lazima uwe foreigner otherwise kwa mzawa au raia lazima mamlaka zihusike na sababu iwepo.
 
Wiki hii inaonekana sarafu yetu inazidi kuporomoka..
Bei ya dola inazidi kupaa ..kulikoni thamani ya fedha yetu..

Uthibiti wa matumizi holela ya fedha za kigeni wapaswa kutekelezwa kwa vitendo...
Kodi za nyuma,ada za shule,uagizaji bidhaa,malipo ya huduma mbalimbali...

Wenzetu Afrika Kusini wameweza na wamefanikiwa kwa kiwango kikuu kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni ndani ya nchi yao..Imewasaidia sana kuujenga uchumi wao,kuudhibiti uchumi wao..
ilikuwa ngapi na imefikia ngapi? na ni mwaka gani na mwaka gani? ni mwezi gani na mwezi gani?
 
Wiki hii inaonekana sarafu yetu inazidi kuporomoka..
Bei ya dola inazidi kupaa ..kulikoni thamani ya fedha yetu..

Uthibiti wa matumizi holela ya fedha za kigeni wapaswa kutekelezwa kwa vitendo...
Kodi za nyuma,ada za shule,uagizaji bidhaa,malipo ya huduma mbalimbali...

Wenzetu Afrika Kusini wameweza na wamefanikiwa kwa kiwango kikuu kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni ndani ya nchi yao..Imewasaidia sana kuujenga uchumi wao,kuudhibiti uchumi wao..
dola bei gani? leta takwimu
 
hii hapa
 
Attachments

  • DSC_0013.jpg
    DSC_0013.jpg
    177.8 KB · Views: 81
  • DSC_0014.jpg
    DSC_0014.jpg
    102.5 KB · Views: 87
Kawaida sana, hakuna kigeni hapo
Lakini mkuu mwaka 2015, tulishudia constant dropping ya shiling Tanzania mpaka kufikia 2180 kutoka 1600, na ikabaki hapo kwa karibu mwaka wote 2016 haikupanda wala kushuka, mwaka huu imeanza kushuka tena leo unatuambia tuone kawaida wakati tunategemea kuagiza vitu vingi ikiwemo mafuta toka nje?
 
Mkuu Google rate ya 2015 haikufika 1600, kazi zangu natumia sana dollar, kulipia sehemu mbali mbali.
 
Tangu magufuli aingie madarakani kazuia usafirishaji wa mazao kutoka Tanzani kama vile vitunguu. Sasa tunaface in balance trade. Yani tunaingiza bidhaa zaidi ya kutoa. Tutacontrol inflation lakini sio value of money.
 
Back
Top Bottom