Dokta Mwaka kamshinda Dr. Kigwangala?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,353
38,559
Jana nilisikia kwenye Redio Klouz Fm matangazo yale yale yaliyokuwa yanamtangaza Tabibu Mwaka na Tiba zake hasa kuhusu tiba ya Ugumba ambayo tuliambiwa kwamba ni ya kughushi.Kwa Redio kama Klouz ambao hadi Rais amejibainisha kuwa ni shabiki wao kuendelea kutangaza matangazo hayo ni dhahiri kwamba wanaamini Dokta Mwaka yuko sahihi dhidi ya Dr. Kigwangala.

Kwa nini Dr. Kigwangala hajaja kwa Jamii kutuambia ni nini kinaendelea dhidi ya Dokta Mwaka. Kigwangala alitumia fedha na rasirimali za umma kupambana na Mwaka lakini mwisho wa siku sisi wenye fedha zetu hatujulishwi uhalali au uharamu wa tiba za Dokta Mwaka. Nini kinaendelea??
 
Kingwangala alionesha uwezo mdogo wa kukabiliana na mambo kwani mtu mmoja na mdogo kama Dr. Mwaka hakuwa wa kufuatwa na convoy yote ili ilikua ni wa kutaarifiwa tu kwa barua na kuitwa ofisini. Ona sasa leo yaonekana wazi waziri ameshindwa na Mwaka.
 
inawezekana maan hao hao wakubwa watibiwa kwake. hana tofauti na mzee ambilikile wa loliondo!! na kikombe chake feki!! je kaishia wapi?
 
inawezekana maan hao hao wakubwa watibiwa kwake. hana tofauti na mzee ambilikile wa loliondo!! na kikombe chake feki!! je kaishia wapi?
Kwa maneno haya tunataka kuaminishwa kwamba pamoja na mbwe mbwe zoote tunazooneshwa kuwa Magufuli ana nguvu za "ajabu", kumbe kuna watu wanaizidi nguvu serikali yake!!
 
Back
Top Bottom