Dokezo kuhusu Dini ya Uislam

Unajua unajadili jambo natu anayejua jambo hilo. Nakuuliza ibada gani ?
Kwenye sherehe ya maulid hamfanyi ibada?
Namaanisha kama maulud ni Haram kwa nn waislamu bado wanaendelea kuisheherekea na hufanya ibada ya hiyo sikukuu. Hapo hujaelewa nini?
 
Imani hiyo imeletwa na wao au Yesu ?

Kama Imani imeletwa na Yesu, ili ilete maana lazima taratibu zote awe amezifundisha Yesu.

Mnapoweka taratibu zenu ni kwamba Yesu alikuwa hajui bali nyinyi ndio mnajua zaidi yake, Bali Yesu alifanya uhaini ndio maana nyinyi mkaweka taratibu zenu.

Sisi kuelekea Makka, ni maagizo aliyopewa Mtume Toka kwa Allah. Nyinyi huo utaratibu aliufundisha Yesu ?
 
Napposema huwezi kuutenga uislam na uarabu, namaanisha kama ambavyo huwezi kuitenga Tanu/ccm na nyerere. Hapo umenielewa au bado

Uislamu kuendelea kuwepo hata baada ya mtume kufa hiyo mbona sio hoja? Ulifikiri ili kuutenga uislam n uarabu ilibidi uislam ufe baada ya mtume kufa?

Nimekutolea mfano wa nyerere na ccm. Nyerere kafa, karume kafa lakini ccm bado ipo, au nayo wanachama wameihifadhi vifuani? Kitu kuendelea kuwepo haimaanishi hiko ni sahihi au sio sahihi, uwepo wake hutegemea mapokeo ya wanaopenda.
Waanzilishi wa Freemason walishakufa, Ila chama bado kipo. Unataka uniambie na yenyewe ni nzuri sababu wanachama wameendelea kuwepo?
 
Wewe huwa ni mpumbavu
Thinitisha kwa andiko la biblia.

Kauli zinazonukuliwa kwa kudai kuwa ni ushahidi kuwa Yesu mwenyewe alitaka mafunzo yake yakafundishwe kwa ulimwengu wote yamo katika Injili ya Mathayo 28.19-20, Injili ya Luka 24.46-49 na Marko 16.15.

Mathayo inasema:
Basi, enendeni, mkwafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 28.19-20

Luka anatwambia:

(Yesu) akwaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, naweletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kueni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

Luka 24.46-49

Na Injili ya Marko inasema:

(Yesu) akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Marko 16.15

Je, imekuwaje?

Yesu ni kigeugeu?

Mbona huku anawakataza wanafunzi wake wasende kuwahubiria ila kabila kumi na mbili za Israili, na huku anawaambia nendeni kuwahubiria Injili ulimwengu mzima.

La, Yesu si mbabaishi, wala si kigeugeu.

Hebu natuziangalie vilivyo hizo amri mbili, moja ya kuwa mafunzo yake wasifunzwe ila wana wa Israili tu, na ya pili ni hii ya kuwa watu wote wafunzwe dini.

Vipande vyote vitatu tulivyonukulu mwishoni havitaji mambo ya Yesu alipokuwa na maisha yake ya uhai wa kidunia, lakini vyaeleza mambo yaliyotukia baada ya "kufufuka kutoka wafu" kama inavyosimuliwa na Injili zote tatu.

Yajuulikana kuwa Injili ya mwanzo kuandikwa ni Injili ya Marko.

Hizo nyingine ziliandikwa baadae, na labda ujuzi wao ulitegemea hiyo hiyo Injili ya Marko.

Yajuulikana vile vile kuwa maneno yote yaliyohusu kufufuka Yesu kutokana na wafu, pamoja na hayo maamrisho ya kwenda kuihubiri Injili "kwa kila kiumbe", kinyume na maamrisho yake yote ya kuwa asihubiriwe ila Muisraeli tu - maneno hayo yote hayakuwamo katik Marko ya asli, bali yaliongezwa baadae.

Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.

William Neil akiandika katika tafsiri ya Biblia iitwayo Harper's Bible Commentary anasema:

"Kama lipo jambo lolote katika uchunguzi wa Injili ambalo juu yake wataalamu wamekubaliana, ni kuwa kufika hapa (yaani Marko 16.8) Injili ya Marko inakoma.

Sehemu iliyobaki ya sura (yaani 16.9-20) ndio hiyo iitwayo "Kimalizio kirefu" cha Injili.

Kimalizio hicho hakionekani katika nakala za miswada ya zamani, na ambacho ni nyongeza iliyopachikwa katika karne ya pili kutokana na maongezo ya Mathayo, Luka na Matendo...

ushahidi wa kale kabisa ulioandikwa juu ya Kufufuka (Yesu) haumo katika Injili bali katika barua ya kwanza ya Paulo kuwapelekea Wakorintho 15.3-8."

Maneno hayo ya Paulo aliyowaandikia Wakorintho na ndio mara ya kwanza kutajwa kufufuka kwa Yesu ni haya:

Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maaandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; badaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

1 Wakorintho 15.3-8

Ikiwa kipande chote tangu mstari 9 mpaka mstari 20 katika sura 16 ya Injili ya Marko, kimepachikwa, basi kisa chote cha kufufuka Yesu kimebuniwa.

Mwenye kubuni kisa hichi ni Mtakatifu Paulo.

Hivyo ndivyo tunavyoweza kuagua kutokana na kuisoma Biblia, kwani maandishi ya kwanza hayamo katika Injili bali yamo katika barua ya Paulo kwa Wakorintho.
 
Sio kwamba alisema, hakujua kusoma wala kuandika, na Qur'an imesema hivyo.

Sasa tuambie wewe alisikia Toka kwa nani, sababu hata walio ishi nae kwa uwezo wake wakusimulia ya kale walimuamini sababu sio jambo la kawaida.
 
Allah pia ndio aliagiza mzunguke mara 7?.
Naomba aya.

NB: Kumbuka waarabu walikuwa wanazunguka kaaba kabla ya Uislam. Na kuabudu masanamu yao 360
akikujbu hapa vzr bila porojo leo naslimu aisee. NIPO TYR KUCHUKUA DHAMBI ZOTE ZA SHETANI NA MIMI NDIYE NIWE SHETANI NAYE SHETANI ASAMEHEWE KULIKO KUWA MUISLAM dini ya harakati za ksiasa inayoenezwa kwa vita..dini mungu anayepganiwa na wanadamu.
 
Kwenye sherehe ya maulid hamfanyi ibada?
Namaanisha kama maulud ni Haram kwa nn waislamu bado wanaendelea kuisheherekea na hufanya ibada ya hiyo sikukuu. Hapo hujaelewa nini?
Kijana huelewi nilichokuuliza ? Niambie ibada gani wanafanya, unajiuliza Mimi tena.
 
Mtume alifundisha kupiga adhana huku spika zikiwa zimewekwa juu ya msikiti? Kwa Nini mnatumia maspika ikiwa mtume hakutumia?

Kwenye ibada msikitini na wakati wa mawaidha mnatumia mic, mtume alifundisha na kufanya ibada kwa mic?

Sasa hivi mna smartphone, mtume alitukia smartphone?

Kwa hiyo mnaenda kinyume nae?
 
Unatoa mifano mfi kweli kweli, chama ni jambo moja na Uislamu mmeunasibisha na uarabu.

Hivyo vyote ulivyo viongelea hapa unaweza kuvitenga na hao waasisi wake kabisa.
 
Ila hakuwa mweusi. Tunamtaka mweusi.
Tafsiri yako ya mweusi ni mtu wa aina gani? Dani alves mm namuona mweupe lakini kule Europe alikua anaonekana ni mweusi akatupiwa hadi ndizi

El hadji diouf mm namuona sio mweusi Ila huingia kundi la watu weusi. Unahisi kwa nini?
 
Kijana huelewi nilichokuuliza ? Niambie ibada gani wanafanya, unajiuliza Mimi tena.
Swali langu mbona rahisi Sana, mnaposheherekea sikukuu ya maulid huwa hamfanyi ibada? Hili swali Lina ugumu gani?
 
Spika sio katika jambo la kiibada, unaweza kusali bila spika na swala ikakubaliwa, na sio sharti kwamba bila spika hakuna sala.

Jifunze kutofautisha mambo. Vipi kiongozi wako anaweza kuendesha ibada pasi na hayo mavazi au wewe ushawahi kuvaa kanzu ukaingia hivyo Kanisani ?
 
Tafsiri yako ya mweusi ni mtu wa aina gani? Dani alves mm namuona mweupe lakini kule Europe alikua anaonekana ni mweusi akatupiwa hadi ndizi

El hadji diouf mm namuona sio mweusi Ila huingia kundi la watu weusi. Unahisi kwa nini?
Mweusi mwenye rangi nyeusi, sababu wapo Waafrika weupe mno.
 
Swali langu mbona rahisi Sana, mnaposheherekea sikukuu ya maulid huwa hamfanyi ibada? Hili swali Lina ugumu gani?
Nimekujibu, ibada gani ? Sababu maulidi ni jambo la uzushi, jambo ambalo Mtume hajalifundisha. Sasa unaposema Kuna ibada zinafanyika ni ibada gani hizo ?
 
Unatoa mifano mfi kweli kweli, chama ni jambo moja na Uislamu mmeunasibisha na uarabu.

Hivyo vyote ulivyo viongelea hapa unaweza kuvitenga na hao waasisi wake kabisa.
Ndio nilikuuliza kwa nn uislamu usinasibishwe na uarabu ikiwa Quran imeandikwa na waarabu?

Unasema unaweza kuitnga ccm na nyerere?? Hebu nieleze kivipi unaweza itenga ccm na nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…