Dogo janja

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,193
“Ninawashukuru sana watu wa Arumeru Mashariki ambao hawakujali umri wangu, uwezo wangu kifedha, historia ya familia yangu katika siasa, na mapungufu niliyokuwa nayo lakini wakakubali kunichagua!
Najua walikuja wengi na fedha nyingi,
Najua walikuja wengi na majina makubwa,
Najua walikuja wengi na kila aina ya mbwembwe,
Najua walikuja wengi na bendi nyingi na wakahonga sana,
... Najua walikuja wengi wakanitukana na kunisema sana! Lakini hatimaye sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, na lile alilolipanga mwenyezi Mungu limekwenda kutimilika!

Walipoambiwa mimi ni mdogo kiumri, walisema siendi bungeni kupeleka mvi au miaka, na wakasema wanahitaji dogo janja na si kubwa jinga,
Walipoambiwa mimi sijaoa, wakasema mimi siendi bungeni kusuluhisha ndoa,
Walipoambiwa mimi ni masikini, walisema wanahitaji masikini mwenzao,
Walipoambiwa sina kitambi, walisema bungeni siendi kucheza mieleka…”


-Mh. Joshua Nassari
 
[video=youtube_share;A7Ng3Y0fa80]http://youtu.be/A7Ng3Y0fa80[/video]
arachugaaa
 
[video=youtube_share;A7Ng3Y0fa80]http://youtu.be/A7Ng3Y0fa80[/video]
arachugaaa
Huyu mtoto naye ni mkali sana na anakua akiwa na damu ya cdm mwilini. Akija kukomaa itakuwa hatari tupu.
 
Back
Top Bottom