sir Ganto G
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 573
- 114
Wakiwa saloon kinyozi akamwambia rafiki yake " kuna dogo mmoja ni mjinga mjinga sana,sijawahi ona dogo mjinga kama yeye, na muda si mrefu atakuja na ntakuthibitishia ujinga wake.
Dogo akaangia saloon, Kinyozi akachukua noti ya elfu mbili akaweka mkono wa kulia na coins za mia mia mbili mkono wa kushoto, Dogo akachagua coins na akaondoka zake.
"si umeona nilichokuwa nakisema Dogo ni mjinga ni mjinga wa mwisho, utadhani katoka kijijini leo" Kinyozi akapiga kelele.
Siku ya pili Rafiki wa kinyozi akamwona Dogo kwa mbali akiwa analamba Chostik baada tu ya kutoka kwa kinyozi kama kawaida yake, rafiki wa kinyozi " wee Dogo mbona kila ukipewa uchague hela unachukua coins badala ya noti?".
Dogo akajibu "siku nitakapo chukua ile noti tu ndo utakuwa mwisho wa kamchezo"