Dogo akaja mikono mitupu!

Mkuu mkiingia mtamboni upya tustuane, ntakuomba unipe kolamu yangu niwe narusha makala zangu pale. Nilikuwa mwanachama hai wa Jitambue na nllikuwa natuma michango yangu sana kule. Dah! Nimekumbuka mbali sana wakati nikiwa paparazi wa kujitolea wa magazeti ya Taifa Letu, Nipashe na Alasiri.
Kumbeeee.............. Nilikuwa nanusa harufu ya utambuzi kwenye michango yako humu. Aisee, waswahili wa Pemba hujuana kwa Vilemba.....................Nilikuwa najiuliza kama wewe si mmoja wa wadau?
Kwa kweli inabidi turudishe ule utambuzi maana nahisi sasa litakuwa na mwitikio mkubwa kwani wakati ule wadau wengi walikuwa wanalipotezea, si unajua Wa-TZ tunapenda UDAKU kuliko makala zenye kuelimisha!
Tupo pamoja mkuu, tutaendelea kuwasiliana kwa kila hatua ya kurejesha gazeti hilo.
 
mi nina kopi zake kama 20 hivi ninazo na huwa ninapitiapitia hizo nakala for reference

aise lile gazeti, sitalisahau, lkn niliona kwa kadiri siku zilivyokuwa zinaenda lilianza kupoteza ladha. Mku kama mnalirudisha zingatia mlivyoanza, lilikuwa supa. Naikumbuka ile hadithi ya Msukule, nikafuatilia mpaka mwisho, dooo! kumbe jamaa alikuwa naota, aise mlifunika
 
nina wasiwasi kama hela ya bia hukua nayo hayo mambo yaliishaje kimya kimya mmh
 
unanikumbusha enzi za gazeti la JITAMBUE la marehemu mzee Munga Tehenan. Kulikuwa na makala inasema 'Nilivyofedheheka'
 
Kumbe hata wewe uliwahi kufedheheka.......................................LOL
 
Mtambuzi huu uzi ni mzuri ila syo kisa chako.Naomba ukiri mbele ya wana JF kabla cjakurushia madongo.Kiri ulipoutoa mana nakumbuka nshawah kusoma stori hii.Ukipindisha maneno tu protokali inafata.Nakusubiri ukiri.Mwenzako mie nkikot mahal huwa nakiri jamvini.Na wewe fanya hvo mkuu
 
Kumbe hata wewe uliwahi kufedheheka.......................................LOL

katika maisha hakuna ambaye hajawahi kufedheheka. Hicho nilichosema hakinihusu mimi bali kulikuwa na ukurasa kwenye hilo gazeti wenye stori kama yako. Hata taito za stori zenyewe zilikuwa katika muundo uliotumia
 
Kumbeeee.............. Nilikuwa nanusa harufu ya utambuzi kwenye michango yako humu. Aisee, waswahili wa Pemba hujuana kwa Vilemba.....................Nilikuwa najiuliza kama wewe si mmoja wa wadau?
Kwa kweli inabidi turudishe ule utambuzi maana nahisi sasa litakuwa na mwitikio mkubwa kwani wakati ule wadau wengi walikuwa wanalipotezea, si unajua Wa-TZ tunapenda UDAKU kuliko makala zenye kuelimisha!
Tupo pamoja mkuu, tutaendelea kuwasiliana kwa kila hatua ya kurejesha gazeti hilo.

Naomba tupeane taarifa ya hilo gazeti maana hata mimi nlikuwa msomaji wake maarufu sana nlikuwa na copy nyingi sana za Jitambue na Mshauri wako lakini bahati mbaya niliziacha home hivi nipo ng'ambo miaka kibao,ikiwa mtalirudisha hewani tujuzane,munga alikuwa ni zaidi ya mshauri!
 
Kumbeeee.............. Nilikuwa nanusa harufu ya utambuzi kwenye michango yako humu. Aisee, waswahili wa Pemba hujuana kwa Vilemba.....................Nilikuwa najiuliza kama wewe si mmoja wa wadau?
Kwa kweli inabidi turudishe ule utambuzi maana nahisi sasa litakuwa na mwitikio mkubwa kwani wakati ule wadau wengi walikuwa wanalipotezea, si unajua Wa-TZ tunapenda UDAKU kuliko makala zenye kuelimisha!
Tupo pamoja mkuu, tutaendelea kuwasiliana kwa kila hatua ya kurejesha gazeti hilo.
Count me in kiongozi!
 
Ndio nilikuwa nimetia timu jijini Dar kwa mara ya pili mnamo mwaka 1989 baada ya mara kwanza kuja na kuchafua hali ya hewa nikiwa kwa kaka yangu na kupigwa patresheni kijijini. Safari hii nilifikia kwa mjomba angu ili kuona kama mjomba ataweza kunisaidia kuendelea na masomo ya kidato cha sita. Basi, nikawa nakaa kwa mjomba maeneo ya Temeke kata ya 14 nikiwa sina shughuli maalum ya kufanya. Hapo jirani na kwa mjomba kulikuwa na mzee mmoja Mshihiri mwenye duka.

Mzee huyo alikuwa na mtoto wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka 12 wakati huo, ambaye alikuwa anasoma darasa la tano. Huyu mtoto alinizoea sana na mwisho akaniomba niwe namfundisha. Lakini fundishwa yake ilikuwa ya ajabu, kwani alichokuwa anataka ni kufanyiwa homework wanazopewa shuleni basi. Kila nikimfanyia homework akawa ananipa kitu kidogo kama shilingi 200 au 300. Nikawa mzee nimepata kibarua. Nikiona imepita wiki hajaleta homework namuuliza kulikoni, kama walimu wana malaria au vipi. Iliendelea hivyo mwisho nikawa namwambia anipe hela hata kama simfanyii homework.

Nilimwambia kwamba nasubiri kwenda Chuo Kikuu na kumwahidi kwamba, nikimaliza Chuo Kikuu nitakuwa Mbunge wa Temeke na kwa sababu yeye atakuwa mkubwa wakati huo, nilimwambia nitampa ukuu wa wilaya. Kwa sababu ya utoto na somo la Siasa halikuwa likipanda alikubali. Akaanza kuiba fedha nyingi dukani kwao na kuniletea. Dhambi eh, wakati mwingine! Nikiwa hapo Temeke nikaanza uhusiano na binti mmoja. Naye binti nikamwambia nasubiri kwenda Chuo Kikuu na kwamba, mambo yangu ni mazuri, vijihela vya chipsi kuku havinisumbui. Huyu binti aliniamini kwa sababu yule bwana mdogo wakati huo homework zilikuwa zimeongezeka na mshiko nao ukawa umeongezeka.Siku moja yule binti alinifuata akaniambia ana hamu sana ya chipsi na bia. Mzee mzima nilikuwa na kama shilingi mia tu mfukoni. Ilibidi nimwambie yule binti asubiri.

Nilikwenda hapo dukani kwao dogo na bahati nilimkuta. Nilimpiga signo na kumwita kando. Nilimwambia nina shida ya kufa na kupona, anitafutie shilingi 1,000. Dogo aliahidi kwamba, baada ya dakika ishirini angeniwezesha. Aliniambia baba yake akienda kuswali Insha tu, atashughulikia chapchap shida ya mwalimu wake wa tuisheni ya homework, yaani mimi.
Nilimwambia naenda kumsubiri baa ambayo anaijua, kwani tulikuwa tukienda hapo mara kadhaa kunywa soda. Nilimuuliza kama ana uhakika atapata, akasema niondoe hofu kabisa, ni lazima apate, basi nilimpitia demu wangu tukaenda pale baa. Nilipofika pale baa niliagiza bia kwa ‘mtoto’ na chipsi. Kwa sababu wahudumu walikuwa kidogo wananijua hawakunidai kabla. Tukawa tunapiga darasa na ‘mtoto’ huku akijinoma chipsi, kuku na bia. ‘Mtoto’ akamaliza msosi na bia, ikaagizwa bia ya pili, dogo hatokei.

Wasiwasi ukanishika, niliona ni vyema nifuatilie.
Ile nasimama, nikamwona dogo akiwa na baba yake na kaka yake fulani mnoko sana na Polisi aliyevaa sare. Nilihisi kama vile sipumui na sina mwili. Kabla sijapata muda wa kujiuliza, nilimsikia dogo akisema, ‘ni huyu hapa, huwa nampa kila siku.’ Nilijua kila kitu kimekwenda ndivyo sivyo. Dogo alikuwa menaswa kwenye jaribio lake la kunasua ile elfu. Pale nilikuwa mtuhumiwa namba moja wa kumghilibu mtoto kujipatia mali, halafu hapo mezani chipsi, kuku na bia mbili zinahitaji kulipiwa. ‘Afande mchukue bwana, tapeli mkubwa.’ Yule kaka yake dogo alisema. ‘Bwana uko chini ya ulinzi kwa tuhuma za kumtuma mtoto kufanya uhalifu wa wizi dukani. Naomba tufuatane kwenda kituoni.’ Alisema yule Polisi.

Wahudumu wa baa nao walikuwa wamefika wakitaka kulipwa chapaa zao. Nilimtazama yule demu wangu ambaye siku zote huwa anakunywa na kula chipsi kuku bila kujua kwamba, ni Juhudi za mfadhili dogo.
‘Tunamdai afande, tunaomba atulipe kwanza.’ Mhudumu mmoja alisema. Nilijiuliza ni wakati gani radi huwa zinapiga bila mawingu ya mvua. Ni kwa nini isiwe wakati kama ule? ‘Lipa bwana twende zetu.’ Afande alifoka. Nilijifanya kupekua mifukoni na kusema, ‘nimezisahau nyumbani.’ Baba yake dogo alisema, ‘hujasahau chochote, ulikuwa ukisubiri kuletewa, ule na hawara yako. Mimi niwatafutie, nyie mbugie, tena bia! Hapana hiyo haikubaliki.’

Najua mnatamani kujua kilichotokea baadaye.(Umbeya tu!) Kwa taarifa yenu sikupelekwa Keko wala Ukonga, mambo yaliisha kimya kimya. Na kijijini sikurudishwa, nilipelekwa shule na baadae chuo na leo niko hapa JF.

mizaha, masengenyo na uongo ni dhambi, na waongo wote sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto kiebriti, tubu na kuacha uovu ili upate baraka za Mungu math25.41, ufunuo 21.8, mithali 28.13
 
mtambuzi hebu tunga vitabu vya hadithi fupi fupi kama hizi, utatajirika nakwambia...
 
Ule uzi wa Mazishi Songea ulikuwa ni kiboko mzee, yaani mzee mzima nikakalishwa kwenye kigoda kutambikiwa kwa sababu ya unzinzi! ile sitakuja kuisahau..............LOL
Lakini hii ya leo umeionaje.................... nilifedhehekaje!?

Unajua Mtambuzi yaani siwezi kupita thread uliyoianzisha kwa sababu najua itakuwa ya kipekee na huna haja ya kukurupuka kwa maana ya kuwa wa kwanza kuanzisha.

Unajipanga pole pole na kuifanjia full editing kisha ikitoka ipo mahali pale.

Ya leo imenichekesha sana mtu mzima sijui kichwa yako huwa inafikiria nini. Big respect mkuu.
 
mizaha, masengenyo na uongo ni dhambi, na waongo wote sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto kiebriti, tubu na kuacha uovu ili upate baraka za Mungu math25.41, ufunuo 21.8, mithali 28.13

Unajuaje kama si mzaha, jamani ndiyo maana ikawepo jokes. Ni mangapi mabaya tunafanya ya kumchukiza Mungu wetu hatuhesabu ila hili?
 
Ndio nilikuwa nimetia timu jijini Dar kwa mara ya pili mnamo mwaka 1989 baada ya mara kwanza kuja na kuchafua hali ya hewa nikiwa kwa kaka yangu na kupigwa patresheni kijijini. Safari hii nilifikia kwa mjomba angu ili kuona kama mjomba ataweza kunisaidia kuendelea na masomo ya kidato cha sita. Basi, nikawa nakaa kwa mjomba maeneo ya Temeke kata ya 14 nikiwa sina shughuli maalum ya kufanya. Hapo jirani na kwa mjomba kulikuwa na mzee mmoja Mshihiri mwenye duka.

Mzee huyo alikuwa na mtoto wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka 12 wakati huo, ambaye alikuwa anasoma darasa la tano. Huyu mtoto alinizoea sana na mwisho akaniomba niwe namfundisha. Lakini fundishwa yake ilikuwa ya ajabu, kwani alichokuwa anataka ni kufanyiwa homework wanazopewa shuleni basi. Kila nikimfanyia homework akawa ananipa kitu kidogo kama shilingi 200 au 300. Nikawa mzee nimepata kibarua. Nikiona imepita wiki hajaleta homework namuuliza kulikoni, kama walimu wana malaria au vipi. Iliendelea hivyo mwisho nikawa namwambia anipe hela hata kama simfanyii homework.

Nilimwambia kwamba nasubiri kwenda Chuo Kikuu na kumwahidi kwamba, nikimaliza Chuo Kikuu nitakuwa Mbunge wa Temeke na kwa sababu yeye atakuwa mkubwa wakati huo, nilimwambia nitampa ukuu wa wilaya. Kwa sababu ya utoto na somo la Siasa halikuwa likipanda alikubali. Akaanza kuiba fedha nyingi dukani kwao na kuniletea. Dhambi eh, wakati mwingine! Nikiwa hapo Temeke nikaanza uhusiano na binti mmoja. Naye binti nikamwambia nasubiri kwenda Chuo Kikuu na kwamba, mambo yangu ni mazuri, vijihela vya chipsi kuku havinisumbui. Huyu binti aliniamini kwa sababu yule bwana mdogo wakati huo homework zilikuwa zimeongezeka na mshiko nao ukawa umeongezeka.Siku moja yule binti alinifuata akaniambia ana hamu sana ya chipsi na bia. Mzee mzima nilikuwa na kama shilingi mia tu mfukoni. Ilibidi nimwambie yule binti asubiri.

Nilikwenda hapo dukani kwao dogo na bahati nilimkuta. Nilimpiga signo na kumwita kando. Nilimwambia nina shida ya kufa na kupona, anitafutie shilingi 1,000. Dogo aliahidi kwamba, baada ya dakika ishirini angeniwezesha. Aliniambia baba yake akienda kuswali Insha tu, atashughulikia chapchap shida ya mwalimu wake wa tuisheni ya homework, yaani mimi.
Nilimwambia naenda kumsubiri baa ambayo anaijua, kwani tulikuwa tukienda hapo mara kadhaa kunywa soda. Nilimuuliza kama ana uhakika atapata, akasema niondoe hofu kabisa, ni lazima apate, basi nilimpitia demu wangu tukaenda pale baa. Nilipofika pale baa niliagiza bia kwa ‘mtoto’ na chipsi. Kwa sababu wahudumu walikuwa kidogo wananijua hawakunidai kabla. Tukawa tunapiga darasa na ‘mtoto’ huku akijinoma chipsi, kuku na bia. ‘Mtoto’ akamaliza msosi na bia, ikaagizwa bia ya pili, dogo hatokei.

Wasiwasi ukanishika, niliona ni vyema nifuatilie.
Ile nasimama, nikamwona dogo akiwa na baba yake na kaka yake fulani mnoko sana na Polisi aliyevaa sare. Nilihisi kama vile sipumui na sina mwili. Kabla sijapata muda wa kujiuliza, nilimsikia dogo akisema, ‘ni huyu hapa, huwa nampa kila siku.’ Nilijua kila kitu kimekwenda ndivyo sivyo. Dogo alikuwa menaswa kwenye jaribio lake la kunasua ile elfu. Pale nilikuwa mtuhumiwa namba moja wa kumghilibu mtoto kujipatia mali, halafu hapo mezani chipsi, kuku na bia mbili zinahitaji kulipiwa. ‘Afande mchukue bwana, tapeli mkubwa.’ Yule kaka yake dogo alisema. ‘Bwana uko chini ya ulinzi kwa tuhuma za kumtuma mtoto kufanya uhalifu wa wizi dukani. Naomba tufuatane kwenda kituoni.’ Alisema yule Polisi.

Wahudumu wa baa nao walikuwa wamefika wakitaka kulipwa chapaa zao. Nilimtazama yule demu wangu ambaye siku zote huwa anakunywa na kula chipsi kuku bila kujua kwamba, ni Juhudi za mfadhili dogo.
‘Tunamdai afande, tunaomba atulipe kwanza.’ Mhudumu mmoja alisema. Nilijiuliza ni wakati gani radi huwa zinapiga bila mawingu ya mvua. Ni kwa nini isiwe wakati kama ule? ‘Lipa bwana twende zetu.’ Afande alifoka. Nilijifanya kupekua mifukoni na kusema, ‘nimezisahau nyumbani.’ Baba yake dogo alisema, ‘hujasahau chochote, ulikuwa ukisubiri kuletewa, ule na hawara yako. Mimi niwatafutie, nyie mbugie, tena bia! Hapana hiyo haikubaliki.’

Najua mnatamani kujua kilichotokea baadaye.(Umbeya tu!) Kwa taarifa yenu sikupelekwa Keko wala Ukonga, mambo yaliisha kimya kimya. Na kijijini sikurudishwa, nilipelekwa shule na baadae chuo na leo niko hapa JF.

heheh! teteteh! jamaani naumia kwa kucheka, lilopita kwa mwezio linafurahisha, liikukpata linauma kweli, lkn yote ni changamoto na maji ya maisha, unanikumbusha kisa kilichonipata nikiwa na miaka kama mitano, lkn aliyehusika ni kaka yangu kuimba kondoo na kumchinja na mm kuambiwa nikae nija panda nikiona watu nimwambie alikuwa kichakani, cc ni wafugani, wenye kondoo walipotokea nikakimbia mpaka nyumbani nikajifungia ndani, kaka akashikwa wakaja nae hom, kumbe waliniona nikikimbia, mwenyewe akanipakata nakuniambia sipigwi wala kugombezwa niseme yote, nikasema yote, kaka akapigwa ikaishia hapo lkn ilikuwa miaka ya 80 kweusi.
 
wewe utakuwa wa juzi tu maana zamani hizo Dar tulikuwa hatulipi pesa kwanza tukienda bar, hata kama ni mgeni.Hayo ya kulipa kwanza yameanza miaka ya karibuni. Ila hadithi ni nzuri sana
 
Back
Top Bottom