Boflo, huyu ni bata gani anayetangulia mbele ya watoto wake?
Nijuavyo mimi bata huwatanguliza vifaranga wake, kisha yeye hubaki nyuma.
Huyu bata aliyewaacha wanawe wadumbukie mtaroni ni mfano halisi unaotukabili sisi leo.
CCM imetundumbukiza mtaroni wakulima na wafanyakazi, imebaki na mafisadi inaowalinda na kuwakumbatia kwa udi na uvumba.
JUMAPILI KAREEM
Mmh kazi ipo
Nimejisikia vibaya, ni huzuni kumpoteza hata mmoja kati ya wadogo hawa!
Hivyo ndivyo magamba wanavyo baki wa chache na kumuachia mama yao aendelee kuongoza taifa!
Hata nyani pia hupandisha wanaye juu ya mti na kuwatupa watoto chini ili kuwakomaza. Hilo ni jaribio tu, alitaka kuona kati ya watoto wake ni yupi mwenye akili ya kuvuka vikwazo bila kuangamia, sasa hao waliotumbukia ni wazembe kwa nini watumbukie wakati kwa kila shimo kuna sehemu ya kuvukia? Ndio maana akageuka kuwangalia hapo ana watukana kama namsikia "mabwege nyie mbona mwenzenu kavuka vizuri?, kila siku nawachunga nikiwaweka mbele yangu halafu mnajisifu mnajua sana leo nimewaweka nyuma yangu niwaone werevu wenu mmetumbukia shimoni".View attachment 68105
.............
Huyu bata mie namwana kwamba ni genius.
Kwa nini ulee mapakashume ambayo hayana hata chembe ya akili??
Kama hayo matoto yangekuwa na akili, yangekataa kuvuka na kumlazimisha mama kurudi kuwatafutia njia bora.
I wish tungepata mtu kama huyo bata ili atusaidie kusafisha virus vilivyoenea kila mahari....hata ikibidi kubaki na Mtanzania mmoja, ni poa...atazaa na kuanza upya!!
Babu DC!!