Does the rest of the world know this | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Does the rest of the world know this

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njowepo, Nov 26, 2009.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Pori la Selous linaongoza kwa tembo duniani

  na Mohammed Mhina, Polisi

  PORI la Akiba la Selous, linaongoza kwa idadi kubwa ya tembo wakati pori la Katavi mkoani Rukwa, linaongoza kwa kuhifadhi idadi kubwa ya mamba ikilinganishwa na mapori na hifadhi nyingine duniani.
  Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori nchini, Erasmus Tarimo, wakati akizungumza na askari wa operesheni kipepeo inayoendelea kwenye mapori ya akiba ya Selous, alipowatembelea kujionea maendeleo ya operesheni hiyo.
  Tarimo alisema Tanzania inahitaji kuendeleza rekodi nzuri ya uhifadhi wa wanyamapori, wakiwemo tembo, mamba na twiga ili kuendelea kuwavutia wageni na kuongeza pato la taifa.
  Alisema serikali inahimiza operesheni kipepeo inayoendeshwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Idara ya Wanyamapori katika kukabiliana na ujangili kwenye mapori ya akiba na hifadhi za taifa hapa nchini iwe ya kudumu.
  Alisema Tanzania inahitaji kuendeleza rekodi ya uhifadhi wa wanayamapori wakiwamo tembo, mamba na twiga ili kuendelea kuvutia wageni na kuongeza pato la taifa.
  Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mkuu wa Operesheni Maalumu nchini ambaye ndiye msimamizi wa Operesheni Kipepeo, Naibu Kamishna (DCP) Venance Tossi, alisema doria za pamoja na operesheni za mara kwa mara katika mapori ya akiba na hifadhi za taifa, zitatokomeza ujangili nchini.
  DCP Tossi alisema Jeshi la Polisi liko tayari kushirikiana na chombo chochote kuhakikisha usalama wa nchi unaimarika kwa kuhakikisha hakuna mtu ama kikundi cha watu kitakachotishia usalama wa raia na mali zao.
  Naye Dk. Pascal Kumburu wa kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi nchini anayeshiriki katika operesheni hiyo, aliwakumbusha maofisa na askari wanaoshiriki operesheni hiyo, kujiepusha na vitendo vya ngono.
  Operesheni hiyo ambayo inaendelea katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya pori la akiba la Selous, inaingia awamu ya pili inayoishirikisha mikoa ya kati, kaskazini na Kanda ya Ziwa, kwa lengo la kukomesha vitendo vya ujangili kwenye mapori ya akiba na hifadhi za taifa nchini.
  Pori la Akiba la Selous lililopo katika mikoa minne na wilaya 10 zilizopo katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Lindi na Rukwa, lina ukubwa wa kilometa za mraba 50 na ina hifadhi aina mbalimbali ya wanyama.
  Wilaya zenye utajiri huo ni za Ulanga, Kilombero, Mvomero na Kilosa mkoani Morogoro; Rufiji na Kisarawe za mkoani Pwani, Kilwa na Liwale za Mkoa wa Lindi na wilaya za Tunduru na Namtumbo zilizopo katika mikoa wa Ruvuma.

   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  jamani mijitu mingine nyie tabu loo. hila inajitambua kama inamitatizo ya asili chill son
   
Loading...