Dodoma: Wanahapana wagoma, Kamati yaachwa marikiti

Ndo mtajuwa maana ya maridhiano...

1. Maridhiano gani mnayataka wakati vinavyosababisha mfanye maridhiano mnaendelea navyo..??
2. Cha kutueleza wananchi ni kwamba rudisheni hela mliyotumia... MWIGULU ALISHASEMA... Tatizo lenu CCM yeyote anayeleta mawazo mbadala huwa mnamwita msaliti... NYERER ALISHASEMA, CCM SI MAMA YAKE... sasa hao uliowaita wanaHAPANA, WAMEIRUDIA KAURI HIYO KIVINGINE...
3. Na kiwa nini muwahoji waliosema hapana pekee..?? Wale waliosema NDIYO kwa nini hawaitwi kuridhiana ili wajiunge na wanaHAPANA..??
4. Yaani hao saba/nane ndo mnawaogopa sana hadi kuwaundia kama ya maridhiano kuliko wananchi..??? JE IKITOKEA MWANANCHI MMOJA AKASEMA HAPANA, NAYE MTAMUUNDIA KAMATI YA MARIDHIANO..?? TATIZO MNA KELELE SANA KABLA YA KUVUKA MTO.
5. Mlidhani kura za wazi ndo mtashinda, sasa HAPANA ZA WAZI HAZICHAKACHULIKI..

MMESEMA WAPIGE KRA... KWA WAZI AU KWA SIRI KUTEGEMEANA NA MAAMUZI YA ANAYEPIGA KURA...

1. KWANINI KURA YA HAPANA IUNDIWE TUME..??
2. Kwa nini kura NDIYO haiundiwi tume..??
3. Waliowahi kupiga kura za hapana huko nyuma waliwahi kuundiwa tume..??

kwa kiasi kikubwa umeandika vizuri, ulipoalitaja kwa unafiki jina la naibu katibu mkuu ccm bara umeharibu kila kitu.
 
Sauti ya mungu sauti ya watu

mungu shuka bwana kwenye lile jengo angamiza tu baadhi ukianza na mh sitta

tuwe na amani kwenye hii katiba
 
Sitta anazidi kusema uongo bungeni kuwa kuna ukawa wawili wameomba kupiga kura na tayari wameshapiga.hajasema Kama wamepiga indigo au hapana.anachozidi kung'ang'ania ni kwamba lazima katiba ipite.nadhani huyu mzee anazidi kuchanganyikiwa awahishwe mirembe kabla ya kuharibikiwa zaidi.nimemsikia hehe sit a na mapalala aliendelea kuwatukana maaskofu kuwa ni wameandika waraka wa kijinga.
 
kwa kiasi kikubwa umeandika vizuri, ulipoalitaja kwa unafiki jina la naibu katibu mkuu ccm bara umeharibu kila kitu.
Hapana, si kwamba CCM kuna wabaya tu na ambao wanasema mabaya tu kila wakati... Kuna wakati wanatoaga kauli tunazoziunga mkono.. Wakisema mazuri tuwasifie, wakisema mabaya tuwakosoe...
 
Linapokuja suala la Wa-zanzibar, mimi huwa namuunga mkono mhe.Kessi
 
1922133_644441985654444_3906370969595424213_n.jpg
 
Eeeeefuu!!!sijui nianze kufungua shampagne mie,hongereni wana HAPANA!!!
 
Kamati ya Maridhiano nayo ikagomewa.Wazanzibari wamesema wao wameshasema HAPANA na hawatasema NDIYO kwa vyovyote vile. Mwenyekiti Sitta amearifiwa kuwa Kamati ya Maridhiano iliishia kusubiri bila wahusika kujitokeza.Vimesikika viapo vya kutorudi nyuma.Hapa Dodoma mambo ni moto.Kila mmoja anasema na kushauri lake. Njiapanda. Tutokaje?

Intelijensia inaonesha kuwa kura za HAPANA za wazi na siri zimeshakwamisha akidi ya kupitisha Rasimu iliyopendekezwa na Kamati ya Chenge. Ndiyo maana Kamati ya Maridhiano iliundwa haraka sana kusaka maidhiano ya kiakidi.Lakini,Wazanibar wameapa kulinda kura zao za HAPANA walizozipiga sirini na bayana. Njiapanda. Tuamue kuelekea wapi?

Tafadhalini Wazanzibari,tuokoleeni Rasimu hii ili,kama chama tawala,tupate cha kusema kwa watanzania. Tutasemaje mambo yakibaki hivi yalivyo?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (kwasasa Dodoma kurudi Dar)

Ooooooh time will tell, Jah will never give the power to oppose!
Bob Marley 1981
 
mnasherehekea nini. mnadhani hao wajinga wanaopiga kura kwa maelekezo ya mabwana zao watakwamisha katiba? mtu hajachangia hata thumni, mwanzo hadi mwisho halafu kura anakurupuka 'hapana'. kwa msingi huo ikibidi kanuni zirekebishwe, nusu tu, katiba inapita.

Ee kweli bora kanuni zirekebishwe. Hata iwe kura moja tu ya mheshmiwa 6 katiba ipite. Wasituchezee hawa.
 
CCM hovyo kweli mnasaka maridhiano maji shingoni. Hamjasikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini. Serves you right kudharau umma.
 
Hivi kwa sasa huyu mzuzu anajiskiaje maana kwa sasa hatakiwi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi!

S.i.t.a cheo chako kizuri kama mawazo yako
 
Matokeo yakiendelea hivi hivi, basi laana za Watanzania zitakuwa zimetua mahali pake! Naomba Mungu hadi dakika hiyo ya Oktoba 4 matokeo yabaki haya haya!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom