Dodoma: Wanafunzi 92 waliorejea shule baada ya kujifungua, wakwama kuendelea na masomo

Dodoma: Wanafunzi 92 waliorejea shule baada ya kujifungua, wakwama kuendelea na masomo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
Ugumu wa maisha na kukosekana kwa Wasaidizi wa kulea Watoto kumetajwa kuwa kuwa sababu ya kusitisha masomo kwa Wanafunzi 92 kati ya 265 waliorejea masomoni baada ya kupata ujauzito shuleni chini ya Utaratibu wa Kuboresha Elimu Sekondari (SEQUIP).

Msimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dodoma, Anna John anasema “Takwimu hizo ni kwa Mwaka 2022 na 2023 katika vituo 9 vya Dodoma, baadhi ya sababu nyingine wanazotaja kuwakwamisha ni Wanafunzi hao kushawishiwa kurejea kwa wenza wao.”

Chanzo: Azam TV
 
Waliosema "Mchovya asali haonji mara moja" walifikiri na kuona mbali sana.

Wanahutaji elimu ya ziada ili kuhakikisha wanafanya maamuzi yenye msimamo. Kama shule au familia wachague moja.
 
Kuwasaidia hao nikuwapa Elimu ya Kujitambua ngono hipo tu na haiwezi kuisha wanaweza hata kujichua na nk ni Ajabu Sana mtu kuacha kufocus na Future yake na akawaza kufanya Ngono ambayo hipo muda wote na faida zake ni chache kuliko Hasara
 
Siku hizi watoto uko shuleni wanakutana na Wazazi kwenye vipindi class yaani unakutana na single mothers wanaofundishwa colony economy,Tungo tata nk
 
Natamani kufahamu idadi kamili ya wanafunzi walioshindwa kuendelea na hayo masomo katika shule ya Sekondari Mpwayungu.
 
Alifungwa nani mtaani kwenu. Kesi zipo Lakini tangu napata fahamu sijawahi kusikia mtu ninaemjua au wa katani kwetu kafungwa.
Wengine wanafungwa sana tu nenda magerezani utawakuta.
 
Back
Top Bottom