Dodoma: Spika Ndugai ashangaa baadhi ya makofi yanayopigwa na Wabunge

Dodoma. Spika wa Bunge Job Ndugai amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakipiga makofi bungeni lakini haijulikani wamepiga ya nini.

Ndugai alisema hayo jana wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Khamis akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu (CCM) Husna Sekiboko kwamba polisi wamekuwa wakishindwa kufika kwa wakati maeneo mbalimbali kwa sababu ya kukosa mafuta na matengenezo ya magari.

Awali, akijibu swali Khamis alisema kwa mujibu wa sheria ya bajeti wenye fungu ni mkuu wa polisi nchini (IGP) na Ma-RPC hivyo fungu likitoka kwa IGP linakwenda kwa RPC na kisha kugawiwa kwa wakuu wa polisi wa wilaya husika.

Alisema wanalichukua suala hilo na kwenda kukaa na wadau ili kuona namna wanavyoweza kulifanyia mabadiliko.

Hata hivyo, majibu hayo yaliwafanya baadhi ya wabunge kumpigia makofi naibu waziri huyo, hali iliyomuibua Ndugai ambaye alisema kuna wakati wabunge wanapiga makofi haifahamiki wanapiga ya nini.

Ndugai alihoji kuwa: “Halafu waziri akakae na wadau, wakina nani? Halafu tunashangilia (wabunge) tunakubali hiyo kanzu.”

.
Screenshot_20210209-120825.jpg
 
Amkumbuke swaibu yake aliyeliona hilo mwanzo ,hata yeye Ndugai alikuwa anamcheka ,..hawakumuwelewa yule aliehoji kutowaelewa wabunge wa CCM,,,mna njaaa eeee mmeshiba eeeei...... Hongera sana Mbunge mstaafu aliekijulikana kwa jina la Bwege,aliyaona zamani haya anayoyaona leo Ndugwai.
 
Ooho kimeumana, bunge la kijani, tutaelewa tu kijani kibichi, kijani mpauko, kijani ya jani la mgomba, jani la muembe! 😂

Inaonekana hawakupeana maelekezo vizuri!

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Back
Top Bottom