Dodoma: Serikali kufunga kamera za usalama maeneo mbalimbali ili kupunguza uhalifu

Miji mikuu ya nchi haipaswi kuwa na fujo kelele huwa tulivu na zaidi huwa kimya ikiganania na makao makuu ya taifa fulani na mahala pa utendaji na country administrative palaces,
':::mwl jkn hakutaka makao makuu ya aina hii, mwl alikusudiaa kuifanya Dom kama "KREMLIN"
 
Mtaka mtu wa dili ashaanza ku-force kama alivyokuwa aki-force simiyu kwenye barabara
Wakati LISSU anashambuliwa eneo lilikuwa na camera au hapana. Kama zilikuwepo zilisaidia nini?waache kuchezea Kodi zetu!!
 
Nchi za Afrika siku tukikubali kubadilika akili zetu ndipo chochote tunachofanya kitakuwa na msaada.Kamera pasipo wahusika na viongozi kubadilika na kuacha maigizo zitakuwa na msaada, vinginevyo zitakuwa fursa za watu kupiga hela kuanzia uwekaji wa miundo mbinu mpaka usimamizi.
 
Serikali imedhamiria kufunga kamera za usalama katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kupunguza uhalifu ambao umeanza kushamiri katika maeneo ya jiji hilo baada ya Serikali kuhamia Dodoma huku wimbi la watu likichagiza hali hiyo ya uhalifu.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka wakati wa Hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe kinachojengwa katika eneo la Chang’ombe, jijini Dodoma.

Adhma hiyo ya kujenga kituo imekuja baada ya matendo ya uhalifu ikiwemo uporaji, ubakaji, udhalilishaji, matumizi ya dawa za kulevya kushamiri katika maeneo ya Chang’ombe hali inayopelekea wananchi wa maeneo hayo kuishi kwa wasiwasi wakihofia matendo hayo ya uhalifu.

“Maeneo mengi ya jiji la Dodoma tutafunga kamera za usalama barabarani, hatuwezi kuwa na jiji ambalo polisi wetu wanakimbizana na wahalifu muda wote, tutatumia teknolojia hiyo kudhibiti uhalifu wa aina mbalimbali, Dodoma ni Makao Makuu ya nchi lazima pawe salama nawashauri wahalifu watafute shughuli nyingine ya kufanya hapa si salama tena kwa kazi zao” Mtaka

Akizungumzia Ujenzi wa Kituo hicho cha Polisi, Mkuu wa Mkoa huyo aliwataka wananchi kushirikiana na serikali kuhakikisha kituo hicho ujenzi wake unakamilika mapema ili kianze kutoa huduma za kiusalama katika maeneo hayo.

“Chang’ombe inakua inahitaji kituo kikubwa kitakachofanya kazi saa ishirini na nne ili wafanyabiashara na wananchi wafanye shughuli zao kwa muda wote na sio biashara zifungwe kwa kuhofia uhalifu, sasa kazi ya serikali sio kukwambia ufunge biashara yako muda gani kazi ya serikali ni kukulinda ili kuwepo na uhuru wa kutoa huduma, kwahiyo wananchi tushirikiane ili kituo kimalizike haraka” Mtaka

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Naibu Katibu Mkuu Ramadhani Kailima alisema wizara imetoa kiasi cha shilingi milioni 10/= kama mchango wake katika ujenzi wa kituo hicho na kikikamilika kitaweza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo upelelezi wa matukio, upelekaji wa majarada ya kesi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ambayo yatapelekwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Katika hafla hiyo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alichangia papo hapo mifuko hamsini ya sementi kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka.
Hadi leo bado tuuu hatujaziona
 
Wamefunga camera kwenye majengo ya serikali lakini bado baadhi ya viongozi wanazembea,wanakula rushwa,wananyanyasa watanzania,wanafanya ngono maofisini nk. Sasa wanazifunga barabarani zitasaidia nini?
Zaidi zitawanasa wanavyoomba rushwa na hao ndio watakaoanza kuzifanyia hujuma
 
Back
Top Bottom