Dodoma na Unafiki wa Viongozi Wake

The Worshiper

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
302
89
Ni saa moja kasoro asubuhi hapa Dodoma nipo kwenye Daladala na rafiki yangu,mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ,tunatokea Area C mahali tunapoishi kuelekea chuo kuwahi vipindi.Mimi nina muda sasa, nipo mwaka wa tatu chuoni lakini mingi zaidi hapa Dodoma,ni kama mwenyeji wake,mambo mbalimbali,vioja,vituko,siasa na mambo mengine mengi yanayofanyika nayafahamu zaidi yake.

Njiani kunaonekana bize tofauti na siku nyingine na kuna msongamano fulani wa magari unaotokana na wakinamama wanaooneka kuwabize kusafisha barabara,mafundi wa taa za barabarani nao wako juu wanakarabati,ni jambo linaloonekana kama geni kwa mwenzangu ambaye tangu aingie mji huu semester yake yote hii ya kwanza hakuwahi kuona barabara ikisafishwa.Naye hasiti anauliza “Sikuwahi kuona barabara inasafishwa hapo kabla” Namjibu kifupi “Kuna wageni”.Anaonekana kunielewa lakini akiwa na maswali mengi kichwani.Baada ya muda kila mmoja yuko darasani kwake, sauti kali ya ving’ora inapenya masikioni vinaharibu tention hapa chuo,tunasubiri hali itulie,wageni washaingia.Uhakika wa jibu langu ashaupata.


Leo vipindi vinaisha jioni kabisa,tunatoka tunaelekea ghetto(nyumbani)barabara yote taa zinawaka anashangaa anaonekana kufurahia hali hii, ni mara yake ya kwanza pia kuona hapa,mji msafi,angavu unameremeta,lakini zamu hii haniulizi anajisemea mwenyewe kwa kiingereza It's amaizing!! nami namwambia “It will only take one week”,anakunja uso anajibu kwa maneno makali kidogo,That’s F***** bongo politics.Naweza kuzihisi hisia zake kwenye hilo,nanyamaza tunasonga.


Wiki moja sasa imepita barabara na mji wote ni mchafu Akinamama hawaonekani tena barabarani, kibarua kwisha mpaka mgeni aje tena.Giza nalo limeshika hatamu,hakuna anayejali,si mkuu wa mkoa,mkurugenzi,diwani wala mwenyekiti wa mtaa,Ndiyo,wageni siwamekwishaondoka!.Ni kama mji hauna serikari tena.Naam tumerudia zama zetu.Funika kombe mwanaharamu apite.Mgeni ashapita,ashatumwagia sifa mji wetu ni msafi usiku ni kama mchana,tunafurahi tunasema karibu tena Mgeni.Naam Mgeni ashaondoka tunazima taa zetu tunaanza kupapasa tena gizani huku njiani tukienda mwendo wa chura hapa pale hapa pale kuukwepa uchafu.Nayakumbuka tena maneno ya rafiki yangu That’s F***** bongo politics,nasonya naangalia milingoti ya taa nakujiapia mwenyewe sitovumilia tena.
 
wagogo washamaba sana hapa mjini 2015 lazima tuweke mbunge wa chadema, wa ccm watakuwa kama maloloe bugos mp na BSc yake ya online
 
Back
Top Bottom