VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Katika kile kinachoonekana kama kugonga mwamba kwa chama tawala (CCM) kusambaza Waraka wa Siri unaobeba Rasimu Mbadala ya Katiba mpya, chama hicho kimeamuru kukusanywa mara moja kwa Waraka huo ili asakwe aliyeuvujisha kabla. Chanzo cha kuaminika toka Makao Makuu ya CCM hapoa Dodoma kinasema kuwa CCM imetaharuki baada ya kugundua kuwa Waraka huo umeshawafikia hadi Wajumbe wapinzani.
'Mambo ni magumu kwetu. Leo umeona tulivyoangushwa kwenye 'kura ya wazi'. Sasa chama kinakusanya Waraka wake. Sina hakika kama huo ndio utakuwa mwisho wa udhibiti wa chama kwa Wajumbe wanaofungamana na chama kwakuwa Waraka huo ndio msimamo wa chama.' kilisema chanzo hicho
'Mambo ya msimamo ni magumu sana. Nadhani,chama kingeweka utaratibu wa kuelimisha Wajumbe taratibu hadi wajue kwanini CCM inasimamia mambo fulanifulani. Hii ya kulazimishana,itaiaibisha chama hapo mbeleni. Hakuna elimu yoyote itolewayo kwa wana-CCM waliopo hapa Dodoma zaidi ya kumezeshwa tu msimamo wa chama.' alisema Mjumbe mmoja wa Bunge la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkoa wa Mara (CCM)
Siasa za chama changu hunishangaza sana. Waraka ulishasambaa na kusomwa. Itasaidia nini kuukusanya muda huu? Utakusanywaje?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)