Dodoma leo: Waraka wakusanywa

Dodoma leo: Waraka wakusanywa

mwaka huu hadi katiba ipitishwe tutashuhudia mengi
 
Katika kile kinachoonekana kama kugonga mwamba kwa chama tawala (CCM) kusambaza Waraka wa Siri unaobeba Rasimu Mbadala ya Katiba mpya, chama hicho kimeamuru kukusanywa mara moja kwa Waraka huo ili asakwe aliyeuvujisha kabla. Chanzo cha kuaminika toka Makao Makuu ya CCM hapoa Dodoma kinasema kuwa CCM imetaharuki baada ya kugundua kuwa Waraka huo umeshawafikia hadi Wajumbe wapinzani.

'Mambo ni magumu kwetu. Leo umeona tulivyoangushwa kwenye 'kura ya wazi'. Sasa chama kinakusanya Waraka wake. Sina hakika kama huo ndio utakuwa mwisho wa udhibiti wa chama kwa Wajumbe wanaofungamana na chama kwakuwa Waraka huo ndio msimamo wa chama.' kilisema chanzo hicho

'Mambo ya msimamo ni magumu sana. Nadhani,chama kingeweka utaratibu wa kuelimisha Wajumbe taratibu hadi wajue kwanini CCM inasimamia mambo fulanifulani. Hii ya kulazimishana,itaiaibisha chama hapo mbeleni. Hakuna elimu yoyote itolewayo kwa wana-CCM waliopo hapa Dodoma zaidi ya kumezeshwa tu msimamo wa chama.' alisema Mjumbe mmoja wa Bunge la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkoa wa Mara (CCM)

Siasa za chama changu hunishangaza sana. Waraka ulishasambaa na kusomwa. Itasaidia nini kuukusanya muda huu? Utakusanywaje?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)
Mkuu Tupatupa, ni kweli tumeangushwa kura za wazi? Mbona mimi siamini kama kuna anayeweza kutuangusha sisi chama dola jamani.
 
kweli ccm hamnazo;na huu ambao kwenye akili watauchukuake?
 
CCM wanatakiwa wajue kuwa kila siku idadi ya wajinga inapungua. Tunaandaa katiba ya nchi siyo ya CCM! Wakumbuke usemi usemao, "mjinga akielevuka, mwelevu yu mashakani"
 
chadema tumeanza na mungu tutamaliza na mungu

Ccm daima

Hili swala la katiba linahitaji nguvu ya watu wengi sana juu ya unazi wa vyama....

Kama wanaoitwa wapinzani wana hoja za msingi bila shaka watahitaji kuungwa mkono na baadhi wa wanaCCM.

Kwenye hili ni vema tukatukuza michango ya kila anayesimama upande wa masilahi ya wananchi walio wengi....In this case tuwapongeze pia baadhi ya wana CCM waliokuwa wakiupinga waraka huu hata kama hawakufanya hivyo hadharani.
 
sijamuona Msalani aje hapa atetee kwa maslahi ya lumumba,ccm walisha kosa mamlaka mda mrefu sana ya kutawala
kinacho waweka madarakani ni vyombo vya usalama wa nchi tu,
jana HAPHREY POLEPOLE kamishina wa tume ya mabadiliko ya katiba alisema jambo moja kuwa waraka wa ccm umesha feli kabisa maana yale mambo ya msingi hasa ya kudhibiti madaraka ya rais wao ccm wamesema kuwa yatungiwe sheria,
sasa kama ccm wao wenyewe hawataki madaraka ya rais yadhibitiwe wameridhika na utawala huu na hizo zilizotengulia,maana anaamka rais LEO anasema MVURA wewe ni katibu wangu hotuba,na hakuna mtu yeyote anayeweza hata kuhoji
ccm uwezi mpa mtu kama Nape ukatibu wa itikadi na uenezi zao la daraja la 4 la mwisho ukategemea mikakati yako isivuje
 
mwekundu umemsikia rungwe?amesema kuwa tatizo ni watu kufikiri kwa kutumia matumbo,hilo ndilo tatizo
 
sijausoma huu walaka aliye na link a-reply hapa nisome pumba zao hawa watawala
 
Mbinu zao zote zile za kuliangamiza taifa Mwokozi anawaumbua kwa kuziweka hadharani. Aibu kubwa.
 
ccm inafanya siasa za kishamba na zilizopitwa na wakati vibaya mno ! Hivi ni akina nani ni washauri wa hiki chama ? HAKIKA CCM ITAKUFA NA HAITARUDI TENA .
 
Back
Top Bottom