PreGE2025 Maganya awaonya wanaowatishia watia nia

PreGE2025 Maganya awaonya wanaowatishia watia nia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
MwenyekitI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Fadhili Maganya amewaonya watu wanaotishia kuwa watakata majina ya wagombea wa nafasi ya Ubunge na Udiwani, kwakuwa hawana mamlaka.

Kauli hiyo aliitoa juzi Mkoani hapo wakati akizungumza na wanachama wa CCM, kabla ya chama kutoa waraka wa kusitisha mikutano inayohusisha wajumbe wa vikao vya uchujaji na uteuzi wa wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani.

“Tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu sasa tangu Juni 20 hatuna Madiwani na ifikapo Juni 27 hatuna Mbunge nafasi zote zinabaki kwa wanachama wa CCM wanaotaka nafasi ya ubunge, udiwani na uwakilishi.

Zipo kauli zimeanza kujitokeza za watu kutishiana kwamba wewe unayegombea udiwani, ubunge tutakata jina lako, wewe huna mamlaka ya kumwambia hivyo mgombea mwenzako kwamba utakata jina lake.

Alisema katika vikao waliambizana kuleta wagombea wanaochagulika na kukubalika na wanachama hivyo vikao hivyo vitaleta watu hao.

“Sasa wewe unataka kuleta mipango ya kukata jina la mtu unakataje, sisi tunataka turahisishe uchaguzi, wewe unataka kuturudisha kwamba tuanze kuhangaika kubembeleza kuwasafisha wagombea wetu kwa dodoki na sabuni hatuna muda huo.

Tunataka watu wanaokubalika na kuchagulika, tunaamini kwamba mtawatendea haki wana Njombe kwa kuwaletea wagombea wanaokubalika.”

Alisema kwa bahati nzuri sasa ni watatu ambao watachujwa na vikao na kurudisha jina moja huku akieleza safari hii wanasimamisha miamba kwelikweli hivyo atakayeshindwa ashindwe.

Kuhusu ubunge alisema yapo maneno na majigambo kwamba fulani atakatwa jina lake halitarudi na kuhoji chama kimempendekeza halafu nani ana uwezo wa kukata.

Alihoji, “Wewe una nafasi gani ya kukata jina la mgombea lililopendekezwa ?.

Alisema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema ana nafasi 10 hivyo akimtaka mtu atamteua katika nafasi hizo, na kwamba bado wapo watu wanadai kuwa wametumwa na Rais.

“Mojawapo ya mambo ninayofanya nikiwa ziara hii nakwenda na majina, natangulia nayo Dodoma ya wale wanaosema wametumwa na Rais nayafikisha kwamba Mwenyekiti nilikwenda Njombe nikamkuta fulani na fulani wanasema umewatuma.

1750836293894.png
 
Back
Top Bottom