VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Hatimaye leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli atalihutubia Bunge na kulizindua rasmi Bunge hili la 11. Kumekuwa na minong'ono isiyo na mfano kuhusu kitakachotokea leo ndani ya Bunge leo kabla,wakati na baada ya Rais Magufuli kuhutubia.
Wapo wanaosema huku wakihema kuwa UKAWA watatoka Bungeni. Wapo wanaosema kutwa nzima kuwa UKAWA watazomea au kupiga kelele zisizo na vigeregere. Wapo wanaosema na kutamani kuwaona UKAWA wakibaki na kumsikiliza Rais Magufuli akihutubia Bunge na kueleza mwelekeo wa nchi yetu kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.
CCM wanasemwa kama walijipanga kushangilia na hata kulia kwa furaha isiyo na karaha wakati Rais akihutubia. Wanatajwa kama wenye furaha isiyo na kifani wala kupimwa kwenye mzani kabla, wakati na baada ya hotuba ya Rais Magufuli leo hapa Dodoma. Nami, kama kada wa CCM, nitaondoka hapa Dodoma baada ya Rais kuhutubia. Nami nimo.
Kusemwasemwa kote huku kunachagizwa, si kuigizwa, na mkwamo wa kikatiba huko Zanzibar. UKAWA hawatamani wala kutaka kumuona Rais Shein wa Zanzibar akiingia Bungeni kama Rais halali wa Zanzibar. CCM wanasema kuwa Rais Shein ni halali kwakuwa uchaguzi wa Zanzibar umefutwa na yeye Dr. Shein anabaki kuwa Rais hadi mpya achaguliwe.
Ni VUTA-NKUVUTE hapa Dodoma. Hali lakini iko shwari na hakuna yoyote tahadhari wala hatari. Kwani, CCM na UKAWA mmejipangaje? Leo, afe mkwezi au zipasuke nazi, mambo yatafanyika hapa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Last edited by a moderator: