Dodoma ipandwe miti sasa

m2020

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
979
1,353
Sio kila kitu mpaka aseme Rais wetu Magufuli jamani. Hebu pandeni miti sasa hapo jijini Dodoma kwa kila kaya iwe na miti isiyopungua 2 na iwe ni jukumu la wahusika kwenye kaya.
 
Hakuna muhamasishaji wa kuanzisha na kutunza Miti.Mkuu wa mkoa na Mkurugenzi wa Dodoma,wote hawapendi miti.Mawazo na Akili zao ni kuuza Ardhi,ili wapate sifa ya Makusanyo.Kitu hiki walitakiwa kutoa Amri kwa Watendaji na Wenyeviti wa mitaa walazimishe kila Kaya ipande miti Kumi na kuitunza kwa Lazima,na iwe hivyo kila mwaka.Kama walivyotaka kufanya kwenye Miche ya korosho,ambapo iligaiwa kila ofisi Serikali ya mtaa,wafanye hivyohivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu msimu wa mvua ungekua mzuri
Serikali inunue miche na raia pia wanunue
Upandaji uwe shirikishi mfano taasisi za umma na binafsi,wenye viwanja,hoteli nk
Yani kila mtu ahusishwe
 
Kweli. Serikali kuanzia ngazi ya chini kabisa (ya mtaa) wangeshirikishwa.
 
Usipowaambia wapande miti ya matunda utashangaa wamepanda, mikaratusi, mikambokambo na miarobaini
 
Umesema kweli. Hakuna anayetoa mwongozo kuhusu upandaji wa miti kwenye jiji hili la Dodoma. Miti iliyopo mingi ni juhudi za viongozi wa iliyokuwa CDA wakati huo ikishirikiana na Manispaa ya Dodoma wakati huo. Miti iliyo kituo cha zamani cha daladala kilichofungwa madreva wa Taxi walisimamiwa waoteshe miti eneo lile nakuhakikisha inakua. Vijiwe vya bodahoda vilivyosambaa jijini wangehamasishwa kupanda miti.

Mvua zinanyesha viongozi ngazi za mkoa, wilaya toeni maelekezo watu wapande miti na kuitunza kwenye maeneo yao. Upandaji na kutunza miti iwe agenda ya kigumu kwenye mikutano ya vijiji na mitaa.

Ubarikiwe sana Stayfar.

Back
Top Bottom