Dodoma: Aua Mke kisa chakula na wivu wa mapenzi

Dodoma: Aua Mke kisa chakula na wivu wa mapenzi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa mauaji ya Lea Eliud Mazengo (50), mkazi wa Kijiji cha Lamaiti, Wilaya ya Bahi, ambaye alikutwa amefariki dunia akiwa shambani baada ya kuripotiwa kupotea.

Kwa mujibu wa taarifa za familia, marehemu aliondoka nyumbani Julai 20, 2026 kuelekea shambani kwa ajili ya kuvuna alizeti, lakini hakurejea. Ndugu na watoto wake walianza msako na baadaye waligundua mwili wake ukiwa umefichwa chini ya magunia ya alizeti yaliyokuwa shambani.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Gallus Hyera, amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu aliuawa kwa kukabwa shingoni na aliyekuwa mume wake, huku chanzo kinachodaiwa kuhusishwa na tukio hilo kikiwa ni wivu wa kimapenzi.

Mmoja wa wanafamilia amesema kabla ya tukio hilo, marehemu na mume wake walikuwa na migogoro ya kifamilia, ikiwamo masuala ya chakula. Amesema hali hiyo ilifikia hatua ambapo marehemu alifukuzwa katika chumba walichokuwa wakilala na kuanza kulala sebuleni.

Kamanda Hyera amesema uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mazingira yote ya tukio hilo, huku viongozi wa kijiji wakieleza kuwa marehemu alikuwa kiongozi wa serikali ya kijiji na mtu aliyekuwa akiheshimika katika jamii.
Miak 50 tayari faken age bado mtu anaweka wivu?
 
Binafsi sina wivu wa kufikia kuuwa mkuu labda sababu ya pesa sio mbunye. Nimekua sasa wanawake nina experience nao kiasi chake Hawaeleweki Wanataka nini? Ni wewe kujiwekea priority mengine yatafwata. Kuna X wangu ameolewa na Kibopa ndoa ya Kanisani Kabisa lakini huwa ananiletea mbunye zikimjaa just imagine. Mwanamke ni Shetani ili muende sawa na wewe Unakuwa Ibilisi
Niko tofauti kidogo na wewe, siwezi kuua labda kwa sababu ya kujilinda tu, sio pesa wala mahusiano.

Ila ndio hivyo mkuu, usiwe too obsessed na mbunye.
 
Back
Top Bottom