Dodoma: Askari Polisi auliwa na raia

Dodoma: Askari Polisi auliwa na raia

Tabby

Mimi naomba tutenganisha siasa na mambo mazito kama haya. Mimi naamini kabisa kinachotendeka sasa hivi ni jamabo zito sanaaaaa. Haijatokea hata siku moja wananchi wakamwua askari kikatili hivyo.

Hiyo siyo jadi na mila za Watanzania. Kuna kitu kikubwa sana kipo kinakuja na kitafika. Serikali inatakiwa iwe makini sana na mwendelezo wa vitu vinavyotokea sasa hivi.

Kwa mawazo yangu kinachotokea sasa hivi ni mwendelezo wa mtandao wa kuuawa kwa askari na kupokonya silaha kule Geita(? sikumbuki vizuri ni mwaka jana lilitokea), Tanga, Ikwiriri, na juzi juzi Morogoro. Polisi vilevile wamepigwa mabomu kule Songea mara kadhaa.

Huu ni mwanzo wa ngoma, inakuwa lele baadaye inakomaa. Boko Haram walianza kwa kuwaua Wakristo makanisani sasa wanawaua Waislamu wenzao.


Beware Tanzanians. Beware. Something is coming your way.
 
Last edited by a moderator:
Hoja hii ijadiliwe bungeni; ni hatari sana kwa usalama wa walinzi wa raia na mali zao.
 
Na wapigwe tu.. CCM inawachonganisha Polisi na Raia kwa kujua au kwa kutokujua. Matokeo yake ndiyo haya.
 
Rest in peace kamanda Joseph Isaack Swai my classmate na jirani yangu kitaani Arusha. wana PCB longido high school tutakukumbuka daima kwa ucheshi wako..

Polisi jamii Dodoma imepoteza mtu makini sana. i will dearly miss you bro.

Pumzika kwa amani
 
Mmmh japo habari hii haina detail za kutosha ila kwa matukio ya karibuni nadhani tunakoelekea si kwema...huu mpishano wa wananchi kujichukulia sheria mkononi na polisi ku enforce sheria isivyotakiwa unatuelekeza kubaya!

Kuna kitu kikubwa kinakuja. Sidhani kuwa Watanzania tumefikia hapo. Unganisha na vitendo vya uporaji wa silaha nyingi uliofanyika siku za karibuni na kulipuliwa Askari Polisi kule Songea. Ni mategemeo yangu kuwa watu wa Usalama wa Taifa na vyombo vingine wanayafanyia kazi haya matukio yote.
 
Waueni tu hila kama nao wengikuwa wauaji km mnavyodai sidhani km mmengukuwa mnaandika utumbo huo kwa amani labda niulize kuna askar aliuwa raia akabaki salama na kazi yake si wote wapo jela? ss mnaposhabikia binadamu mwenzio kuuliwa we unajiona uko salama kbs?

Hapo ni sawa na nyani kucheka wakt chaka linawaka moto wkt jion atakosa pa kulala. Ebu tukemee maovu bila kujali ni nani wala nani kila raia ana haki ya kuishi na mungu hapendi tuwe wanyama kiac hicho.
 
Waziri wa mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Bungeni sasa hivi kuwa polisi ameuawa leo mjini Dodoma wakati akijaribu kumuokoa mtoto ambaye alikuwa "anauawa" na mzazi wake! Anasema mtoto ameokolewa.

Hata hivyo, hakusema mtoto alitaka kuuawa kivipi na wala hajasema polisi kauawa vipi mbali na kuonya wananchi na chuki dhidi ya polisi!


Imekuwaje hapo Dom?
Intelijensia haikuwepo au?Hata hivo nasema acha wapigwe tu!

Jana nimemsikia Mkulu wanji hii akisema WATU WANASHANGAA NINI LIPUMBA AKIPIGWA NA POLISI???
Na mimi nauliza hivi, WATU WANASHANGAA NINI POLISI AKIUAWA NA WANANCHI?????

This is TIT for TAT. Lazima kitaeleweka tu.
 
Hoja hii ijadiliwe bungeni; ni hatari sana kwa usalama wa walinzi wa raia na mali zao.

Nimuda muafaka kwa ccm kujitafakali, tunakoenda polisi watakimbia mitaani. Haowezekani polisi watese na kuuwa raia hovyo hovyo wao polisi wasiuwawe.
 
Chang'ombe ni wabandidu ndo njia ya mnadani wezi wa mjini wanatoka chang'ombe!Kuna kundi kama Panya Road ogopa!
 
Alienda vp peke yake, wakati taratib za kuarrest razima waaanzie askar wawi?
 
Eebwana chang'ombe dodoma ni uswahilin balaaa kama manzese ndo mana ben paul hakupataja kumpelema sophia huko
 
Hali hii isipodhibitiwa sasa huko mbeleni tutaja lia na kusaga meno.

Watawala wamekaa pembeni wakidhani labda wako salama. Historia itatuhukumu.
 
Hao wanabebaga search warrant feki. Waliwahi kuja kunisearch nilipoenda kituoni nikakuta ni feki.
 
ameonya wananchi na chuki dhidi ya polisi? me nadhan angeonya polisi na chuki dhidi ya watanzania!
Angeonya ccm kuwa na chuki kwa wananchi kupitia polisi.
Polisi ni wahanga tu tatizo ni ccm.
 
Waueni tu hila kama nao wengikuwa wauaji km mnavyodai sidhani km mmengukuwa mnaandika utumbo huo kwa amani labda niulize kuna askar aliuwa raia akabaki salama na kazi yake si wote wapo jela? ss mnaposhabikia binadamu mwenzio kuuliwa we unajiona uko salama kbs?

Hapo ni sawa na nyani kucheka wakt chaka linawaka moto wkt jion atakosa pa kulala. Ebu tukemee maovu bila kujali ni nani wala nani kila raia ana haki ya kuishi na mungu hapendi tuwe wanyama kiac hicho.

Kamhanda baada ya shughuli Iringa sasa hivi kapanda cheo.

Mohamed msangi na Rama Ighondu, baada ya kumshugjulikia Ulimboka, mmoja mkuu polisi Mbeya, mwingine kapanda ngazi makao makuu upelelezi polisi
 
Back
Top Bottom