Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,809
- 6,081
RIWAYA; DOA LA VIPEPEO
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660.
-----1-----
Ulikuwa ni muda sahihi kwa kila mmoja kurejea nyumbani, muda ambao jua lilikuwa limeanza kuiacha Mashariki yake na kwenda kwa mchepuko wake bi. Magharibi. Harakati za hapa na pale zilianza kufungwa, watu walianza kujipa uchovu ili mradi tu, warejee majumbani mwao kupambana na masimango ya nyumba zao. Wale wenye gubu, ilikuwa ni wakati wa majuto kwa panya na mbu ambao huishia kuona na kusikia vibweka usiku kucha, kiasi cha kuwanyima uhuru wa kubarizi kwenye vyandarua na kuta za baridi.
Muda huu ni muda ambao huko mwituni, wanyama wakali nao walikuwa wanafunga hesabu za mawindo, huku wanyonge wa pori wakipumua na kulishukuru jua kuzamia kwa mchepuko wake, huku wakilaani ukali wa mke halali mashariki; licha ya kuwapa kula,mwanga na virutubisho, ila aliwachosha kwa kuwapa adhabu ya hekaheka za kunusuru uhai wao. Lakini licha ya kushukuru huko, wapo wanyama ambao muda huo kwao, ndio muda sahihi wa kuingia mawindoni, kuvizia na kujipatia shibe.
Hali hii ilikuwa ni furaha kwa bwana jua, ambae alifurahi kuona kwake na, mchepuko wake kunafaidisha viumbe wa Mungu kwa namna tofauti, hivyo kufanya iwe ni ratiba yake ya kila siku na wakati wote.
Wakati jua anazidi kujichimbia nyumba ndogo, Duniani kulikuwa na mambo mengi yanatokea, usiku huu wa rasharasha, usiku ambao haujaenda eda, kulikuwa na mwanamichezo mmoja, akijaribu kumalizia muda wake wa mazoezi ndani kwake. Hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo, alipiga balizi, kisha akapiga miinuko kadhaa, alojinyoosha na kujipinda kwa utalaamu, huku akiacha viungo vyake vikubali kwa kutoa sauti ya mvunjiko.
Mwanamichezo huyu, alikuwa ni kocha wa timu ya vijana ya Azan, timu ambayo ilikuwa inafanya vyema chini ya mkufunzi huyo raia wa Burundi. Makazi yake yalikuwa Sinza. Alikuwa akiishi kwenye nyumba ya waajiri wake ambao walikuwa ni kampuni ya Azan. Ilikuwa nyumba nzuri yenye hadhi yake, nyumba iliozungushiwa ukuta mrefu na juu yake kukapita nyaya za umeme.
Kocha huyu licha ya kuishi nyumba nzuri na kubwa, lakini hakuwahi kuwa na mke wala mtoto na, hakuna aliewahi kujua kuhusu familia yake.
Aliishi peke yake.
Aliendelea na mazoezi yake, lakini kwenye ukuta wake wenye nyaya za umeme, kulikuwa na kiumbe mwenye moyo wa nyama na miguu miwili yenye vidole vitano. Mtu yule alikuwa anamalizia kuhifadhi mkasi mdogo aliotumia kukata nyaya zile na sasa alikuwa amesimama wima akitizama upande wa mlango wa nyumba ile.
Mtu yule alikuwa amevaa mavazi meusi, kuanzia juu hadi chini kwenye raba zake. Alipokwisha kuhakikisha hakuna anaemuona pale ukutani, aliruka sarakasi moja kavu na kutua chini bila kutoa ukelele, kisha alipiga hatua fupi fupi kama vile alitarajia kuona jambo uani pale. Mtu yule hakunyoosha upande wa mlango uliokuwa wazi, bali alipita upande wa nyuma wa nyumba ile, kisha alitumia mlango wa jikoni kuingia ndani ya nyumba ile.
Muda wote huo, kocha hakujua yanayojiri, wala kuhisi kuna mtu wa ajabu atakuwa kamtembelea ndani kwake. Aliendelea kupiga zoezi jepesi, aliporidhika alielekea chumbani kwake na alipotoka, alikuwa amevaa taulo tu akielekea bafuni.
Wakati yeye akielekea bafuni,mgeni wake yeye alielekea sebuleni,ambapo alichukua simu iliokuwa mezani na kuipachika kwenye chaji na kuwasha,kisha alikaa nyuma ya jokofu kubwa na kutulia kimya.
Kwa nini alifanya vile, hakuna aliejua.
Kocha wa timu ya Azan alipotoka kuoga, alipitiliza chumbani kwake, huko hakukaa sana alirejea sebuleni, ambapo alianza kutafuta kitu, mara akasita na kushangaa.
Hakuwa ameweka simu yake kwenye chaji, alishangaa imejiweka vipi pale na yeye anajua aliiacha mezani.
Ajabu hii!.
Aliifuata simu ile, nayo ikaanza kuita. Kocha aliruka nyuma na kutoa macho kama teja aliefumaniwa.
Aliiogopa simu yake mwenyewe.
Simu ile iliita na kukata.
Kocha bado alikuwa anajaribu kuweka kumbukumbu zake sawa, hakuwa yeye alieweka pale ile simu. Taratibu alianza kuisogelea tena, mara ikaita tena.
Wakati huu aliamua kuipokea, ilikuwa simu ya mmoja wa waajiri wake.
Kocha alikuwa katikati ya maongezi, hata wakati mgeni wake alipotoka mafichoni, yeye hakuwa na habari kabisa, aliendelea kupanga mikakati ya timu yake kusafiri mkoani kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu na timu moja maarufu.
Kocha alistuka akishikwa nyuma ya shingo na mkono ambao ulikuwa umevaa glavu. Alipojaribu kujitikisa, alipigwa teke la mgongo na kumfanya abinukie mbele, na hilo likawa kosa, mana mgeni alimbinua shingo na kukaa kama mtoto analazimishiwa uji wa chumvi.
Kila alipojaribu kujitikisa, hakupata sehemu ya kushika ili ajinasue na kabali ile matata.
Kocha alianza kuvuta pumzi kwa nguvu, hilo ndilo lilitegemewa na mgeni, kwani alizidi kumbinua kocha kwa kumwekea goti katikati ya uti wa mgongo.
Kocha alishindwa kuhimili kabali ile ya aina yake, aliaza kuishiwa pumzi huku macho yake yakianza kuona kiza kizito, huku masikio yake yakianza kusikia kelele za kuzomea za mashabiki wa timu alizozifunga.
Dakika mbili badae, mgeni alikuwa anamlaza chini taratibu, kisha alichukua simu na kuirejesha tena kwenye chaji, kisha alimvuta kocha hadi karibu na simu, kisha alimuinua na kumshikisha simu ile na kuipachika sikioni.
Alipohakikisha maiti ya kocha imeshika vyema simu ile, aliingia mfukoni mwake na kutoa kitu kidogo mithili ya punje ya mtama na kuipachika kwenye spika ya simu. Alipomaliza alisogea pembeni kidogo na kubonyeza saa yake, punde ukatokea mlipuko wa kiasi kidogo, lakini ulikuwa ni mlipuko uliobomoa kichwa cha kocha kuanzia upande wa kushoto kwenda juu na kufanya awe kama papai lilokatwa kipande.
Damu ilianza kutoka, na kusambaa hovyo pale ndani. Mgeni muuaji alianza kuondoka ndani ya nyumba ile, huku akiwa ameua bila kuacha alama ya ushahidi na hiyo ilikuwa ni sheria namba moja. Na kwa kifo cha kocha, maofisa wangeishia kujua alilipukiwa na simu wakati anaongea na simu ikiwa chaji. Muaji akiwa mbali na hisia feki za maaskari.
Wakati muuaji anaondoka ndani ya nyumba ya kocha, kulikuwa na mtu mwingine anaingia pale, akiwa amevaa sawa na yule alietoka, mtu huyu yeye alikuwa ni mfupi tofauti na yule wa mwanzo. Aliingia ndani ya nyumba ile kupitia dirishani,alipofika aliishia kukutana na maiti ya kocha ikiwa na simu iliolipuka pembeni yake.
Mtu yule alitoa simu janja yake na kupiga picha moja, kisha alitoa kibahasha kidogo sana na kukirusha chini ya uvungu.
Kibahasha kile kilikuwa kimeandikwa herufi moja iliochanganywa na namba. Ilisomeka hivi “F3”,Kisha aliondoka mle ndani kwa kupita njia tofauti na alioingilia.
Nyumba ya kocha ilikuwa imetembelewa na watu wawili, huku mmoja akiua na mwingine akiacha ujumbe wenye maana aliojua yeye, na dhahiri alieua hakujua kama ameonwa na mtu alieacha ujumbe.
Lakini kwa nini huyu aue na huyu aache ujumbe, kwanini?..
*****
Nb; Riwaya hii itaanza kuuzika kuanzia jumamosi ya wiki hii....
Ahsanteni nyote mlioshirikiana nami kwa kidogo mlichonacho,ahsanteni kwa wote mlionunua riwaya zilizopita na zitakazokuja...
Na kwa kidogo hicho, nimefanikiwa kupangiwa tarehe ya upasuaji ili kuondoa Figo ilioharibika.
Ahsanteni sana na karibuni kwa kazi hii mpya.