Timu zetu zitumie mbinu ya Morocco kukomesha uhuni wa waamuzi kwa jina la makosa ya kibinadamu kwenye ligi yetu

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,988
10,123
Jana mechi ya Morocco na RSA nimeshuhudia benchi la ufundi la timu ya taifa ya Morocco likiwa na mtu wa IT/TEHAMA/Video Analyst akiwa na laptop yake, kazi ya keni kufuatilia matukio yote na uhuni wote ndani ya pitch/uwanja na akiona dosari inayoipa faida timu yake alikuwa anamuita kocha wao aangalie kisha fasta kocha anawafuata waamuzi kwa kujiamini na kwa kukomaa.

Mwisho wa siku wakapata faida ya penati na alimanusura wafutiwe kadi nyekundu ambayo ilikuwa imeishatolewa tayari, hii ni mbinu nzuri mno hakishindikani kitu na sisi kutumia mbinu hii kinachohitajika ni tablet/laptop App ya Azam Max na bando.

Kisheria inaruhusiwa, tutawabana marefa wahuni ili ifike mahali TFF waone ulazima wa kuleta VAR.

Nawasilisha.
 
Ile review haikuwa ya kuangalia uhalali wa kadi nyekundu bali kuangalia kama kwa kosa lile alistahili ya njano ndiyo apewe nyekundu au iwe nyekundu ya moja kwa moja.

Walichokifanya Morocco kukaa na laptop kwenye benchi la ufundi kuna faida fulani, mfano kuna matukio ambayo hata wachezaji wenyewe wanaweza wasiyaone (mfano mechi ya juzi ya Cape Verde vs Mauritania, kuna mchezaji wa Mauritania alishika mpira ndani ya box karibu kabisa na goli ila nadhani wachezaji wa Cape Verde hawakuliona kwa hiyo hawakulilalamikia kabisa) ila wakiyalalamikia italazimu VAR itumike. Wakati mwingine watu wa VAR wanakaushia matukio kama wanaona timu inayotakiwa kufaidilka na jambo fulani ama hawajaliona tukio au hawajalilalamikia vya kutosha. Kwa hiyo ni aina fulani ya kuongeza pressure kwa waamuzi.

Tatizo la waarabu kwenye mipira, wao ni ushindi kwa namna yoyote ile. Kulalamika haimaanishi wanatafuta haki bali ushindi tu.
 
Ulaya kila team inayo video analysis
kinashindikana nini hapa bongo kwani laptop ya kurekodi mechi ambayo ipo live azam tv wakakaa nayo hapo benchini Tsh ngapi? unakumbuka mechi ya simba vs singida wachezaji walimgomea refa wakakosa suport ya kocha wao maana hakuona hilo tukio wangekomaa kama angeona asingekubali
 
Ile review haikuwa ya kuangalia uhalali wa kadi nyekundu bali kuangalia kama kwa kosa lile alistahili ya njano ndiyo apewe nyekundu au iwe nyekundu ya moja kwa moja.

Walichokifanya Morocco kukaa na laptop kwenye benchi la ufundi kuna faida fulani, mfano kuna matukio ambayo hata wachezaji wenyewe wanaweza wasiyaone (mfano mechi ya juzi ya Cape Verde vs Mauritania, kuna mchezaji wa Mauritania alishika mpira ndani ya box karibu kabisa na goli ila nadhani wachezaji wa Cape Verde hawakuliona kwa hiyo hawakulilalamikia kabisa) ila wakiyalalamikia italazimu VAR itumike. Wakati mwingine watu wa VAR wanakaushia matukio kama wanaona timu inayotakiwa kufaidilka na jambo fulani ama hawajaliona tukio au hawajalilalamikia vya kutosha. Kwa hiyo ni aina fulani ya kuongeza pressure kwa waamuzi.

Tatizo la waarabu kwenye mipira, wao ni ushindi kwa namna yoyote ile. Kulalamika haimaanishi wanatafuta haki bali ushindi tu.
mbinu itumike kwenye ligi kuwapa presha TFF
 
hii hii tanzania ...? mpira wenyewe hatujui tunabutu butu tu
hivyo hivyo mkuu safari ndefu huanza na hatua fupi fupi mfano refa alalamikiwe na wachezaji pamoja na makocha kwakosa halali la mwamuzi kuzingua alafu timu igome kucheza au iendelee hapo tutakuwa tunawapa presha TFF na bndi ya marefa kutuondolea marefa wa mchongo maana watu watakuwa wanalalamika kwa kujiamini
 
mbinu itumike kwenye ligi kuwapa presha TFF
Bila VAR ni nadra sana refa kubadili maamuzi kisa tu amepewa presha. Mwamuzi hawezi kubadili maamuzi kwa kumpelekea kisimbuzi chako aangalie. Haiko practical sana katika mazingira yetu.

Ligi yetu kivyetu vyetu. Jana kuna mchezaji kacheza huku akiwa na magonjwa ya kuambukiza halafu mashabiki wa timu yake ni watu wa kwanza kutetea hilo jambo lililofanywa na timu yake. Wanauliza kwani huo ugonjwa umeua wangapi?
 
Tatizo siyo VAR tatizo wachezaji wa Tz hawajui mpira kabisa wenye vipaji ni wachache wengi wanacheza kwasababu baba zao walikua wachezaji na wao wamejua kutuliza ball kutanguliza mpira mbele na kuukimbilia ndo hivyo kimagumashi magumashi anapata timu ila vipaji hamna wanatumia nguvu nyingi

Na kwenye mashindano haya hakuna sehem Tz wameonewa ni wao tu uwezo mdogo back pass nyingi timu haina muunganiko hujui kiungo nani mshambuliaji nani mpira haufiki mbele
 
Bila VAR ni nadra sana refa kubadili maamuzi kisa tu amepewa presha. Mwamuzi hawezi kubadili maamuzi kwa kumpelekea kisimbuzi chako aangalie. Haiko practical sana katika mazingira yetu.

Ligi yetu kivyetu vyetu. Jana kuna mchezaji kacheza huku akiwa na magonjwa ya kuambukiza halafu mashabiki wa timu yake ni watu wa kwanza kutetea hilo jambo lililofanywa na timu yake. Wanauliza kwani huo ugonjwa umeua wangapi?
Mtaje tu ni kinda la Yanga aka Mzize
 
sasa timu ya taifa picha linaanza ni mwijaku na baba levo kupitisha bakuri .angalau hata bongo zozo jamaa anaweza kusaidia timu
 
Bila VAR ni nadra sana refa kubadili maamuzi kisa tu amepewa presha. Mwamuzi hawezi kubadili maamuzi kwa kumpelekea kisimbuzi chako aangalie. Haiko practical sana katika mazingira yetu.

Ligi yetu kivyetu vyetu. Jana kuna mchezaji kacheza huku akiwa na magonjwa ya kuambukiza halafu mashabiki wa timu yake ni watu wa kwanza kutetea hilo jambo lililofanywa na timu yake. Wanauliza kwani huo ugonjwa umeua wangapi?
Daktari yupi aliyethibitisha kuwa alikuwa na ugonjwa wa kuambukiza?
 
Sijui umeanza kuangalia mpira lini..ila izo Tablet na Laptops zimeanza zamani sana kabla hata ya VAR kufikiriwa...Kama ni mtu wa Analysis wapo sana tu Ligi kubwa duniani EPL wapo sana hao watu...ila kama hujui huo ushairi wako maKocha watachezea Umeme kama njugu..Kocha haruhusiwi kuingilia maamuzi ya refa ndomana Refa anampa onyo la kwanza asilosikia analambwa kadi....
 
Bila VAR ni nadra sana refa kubadili maamuzi kisa tu amepewa presha. Mwamuzi hawezi kubadili maamuzi kwa kumpelekea kisimbuzi chako aangalie. Haiko practical sana katika mazingira yetu.

Ligi yetu kivyetu vyetu. Jana kuna mchezaji kacheza huku akiwa na magonjwa ya kuambukiza halafu mashabiki wa timu yake ni watu wa kwanza kutetea hilo jambo lililofanywa na timu yake. Wanauliza kwani huo ugonjwa umeua wangapi?
Unaweza kuthibitisha kua red ayes ni ungonjwa wa kuambukiza? Rage ni nabii
 
Niliwahi kushauri hapa wengi hamkunielewa tena morocco ni wazi wanawajua vizuri wasauzi endeleeni kupuuza ushauri
 
Back
Top Bottom