engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,149
- 1,441
Wana deal na mustakabali wa maendeleo yetu..that's why..
Kwa nini Taasisi nyingine nazo zisifutwe?
Kwa sababu TAKUKURU ndiyo polisi wa taasisi hizo nyingine. Ikifutwa TAKUKURU itaanzishwa taasisi imara inayoheshimu wajibu wake na ikiheshimu wajibu wake hizo taasisi nyingine timiza wajibu wake
kwanza haina kazi,toka ianzishwe imeshindwa kutushawishi kwamba kwa nini tubaki nayo,kwa nini iendelee kutumia kodi zetu.
kazi zote inazofanya zinaweza kufanywa na jeshi la polisi. kwanza ni watu wenye tamaa ya utajiri wanashindana kununua magari kwa hela haramu.
mimi nashauri ivunjwe mara moja kwa sababu kazi wanayofanya ni tofauti na waliyotumwa(kutetea wala rushwa)
Mara kadhaa uongozi wa TAKUKURU unapokosea jambo wananchi mbalimbali huwa wanakimbilia kudai kwamba Taasisi hiyo ifutwe! (Kwa mfano soma Gazeti la Mwananchi la leo) Sijawahi kusikia kwamba Taasisi nyinginezo viongozi wake wanapokosea idaiwe kwamba Taasisi zao zifutwe!
- TRA inawabeba wafanyabiashara wakubwa na wanakwepa kodi kuliko maelezo, sijawahi kusikia hoja kwamba ifutwe.
- Polisi "wanachakachua" rushwa si mchezo na wanaonea mno wananchi, wengine huuawa hata bila kufikishwa mahakamani kila iitwapo leo lakini hatujasikia kwamba Jeshi hilo lifutwe.
- TANESCO wanatukatia umeme mara kwa mara lakini sijawahi kusikia wakidai ifutwe.
- Usalama wa taifa ndio uko likizo si mchezo, ni kama haupo, lakini sijawahi kusikia hoja ya kufutwa kwa Taasisi hiyo nyeti.
nk, nk, nk, nk.....
Kwa nini linapokuja suala la TAKUKURU huwa inatolewa hoja kwamba ifutwe? Wengine hudai kwamba iwe chini ya Bunge. I can't imagine kwamba chombo cha utendaji ambacho kinatakiwa kiwe chini ya executive kinakuwa chini ya Parliament. After all Wabunge (hasa wa CCM) ni wala rushwa wakubwa, sasa TAKUKURU ikiwa chini yao si ndio watang'oa hata yale meno machache ambayo TAKUKURU ilikuwa imebakiwa nayo?
Tujadili wandugu!
Polisi anayeua jambazi bila hata kulifikisha mahakamani, ambalo ni kosa la jinai, (ambayo hiyo si rushwa) anasimamiwaje na TAKUKURU?
Kwa nini Taasisi nyingine nazo zisifutwe?
Mara kadhaa uongozi wa TAKUKURU unapokosea jambo wananchi mbalimbali huwa wanakimbilia kudai kwamba Taasisi hiyo ifutwe! (Kwa mfano soma Gazeti la Mwananchi la leo) Sijawahi kusikia kwamba Taasisi nyinginezo viongozi wake wanapokosea idaiwe kwamba Taasisi zao zifutwe!
- TRA inawabeba wafanyabiashara wakubwa na wanakwepa kodi kuliko maelezo, sijawahi kusikia hoja kwamba ifutwe.
- Polisi "wanachakachua" rushwa si mchezo na wanaonea mno wananchi, wengine huuawa hata bila kufikishwa mahakamani kila iitwapo leo lakini hatujasikia kwamba Jeshi hilo lifutwe.
- TANESCO wanatukatia umeme mara kwa mara lakini sijawahi kusikia wakidai ifutwe.
- Usalama wa taifa ndio uko likizo si mchezo, ni kama haupo, lakini sijawahi kusikia hoja ya kufutwa kwa Taasisi hiyo nyeti.
nk, nk, nk, nk.....
Kwa nini linapokuja suala la TAKUKURU huwa inatolewa hoja kwamba ifutwe? Wengine hudai kwamba iwe chini ya Bunge. I can't imagine kwamba chombo cha utendaji ambacho kinatakiwa kiwe chini ya executive kinakuwa chini ya Parliament. After all Wabunge (hasa wa CCM) ni wala rushwa wakubwa, sasa TAKUKURU ikiwa chini yao si ndio watang'oa hata yale meno machache ambayo TAKUKURU ilikuwa imebakiwa nayo?
Tujadili wandugu!
Hiyo Quote yote ni upuuzi mtupu, hakuna cha kujadili hapo, zoote TANESSCO, TAKUKURU na nyinginezo doesn't make sense
inabidi ifutwe kwa sababu hizo taasisi nyingine zilikuwepo tokea enzi hizo....takukuru imeanzishwa juzi juzi tu hapa, na haifanyi kazi iliyotakiwa kufanya....na kazi yake ni moja tu....kudeal na mambo ya rushwa.....ambayo haideal nayo......hizo taasisi nyingine zinafanyaka kazi zake, ingawa mara mojamoja zinachemsha lakini kwa ujumla kuna kitu kinafanyika.......TAKUKURU ni kushnehe....na wanaendelea kuharibu....