Inabidi ujue kwanza hili neno "Alien" lina maana gani...??
In fact "Alien" anaweza kuwa kiumbe chochote yule (hata wewe Binadamu) na hutokea hivyo kama ataingia kwenye mazingira geni kabisa nje kabisa ya mazingira yake ya asili.
Mfano; Binadamu akitoka Duniani kwenda Mars au kwenye Mwezi.. kule kama atakuta viumbe wengine basi hao viumbe watamchukulia huyo binadamu kama Alien. So.. Alien ni kitu kigeni katika mazingira yetu ya asili.
Turudi kwenye swali lako...
● Asee... mimi binafsi sina jibu la uhakika juu ya uwepo wa hawa viumbe maana bado naendelea kujifunza. Ila katika pitapita zangu nimegundua kuna makundi mawili yanazozana juu ya uwepo wa hawa viumbe huku moja likiamini kuwa hawa viumbe wapo na jingine likipinga.
● Lakini mambo niliyojifunza kutoka kila kundi ni kuwa kila kundi limekuja na sababu zake...;
○ Wanaopinga wanasema kuwa;
01. Hakuna ushahidi wa kutosha (Obvious physical evidence) juu ya kuonekana kwa hawa viumbe. Wao wanasema kuwa evidence nyingi zinazowasilishwa ni fake, nyingi ni picha za kubuni na computer... yaanu C.G.Is (Computer Generated Images) tuu hasa Video..
02. Matukio ya kuonekana kwa Aliens kwanini yanatokea Marekani, Canada, Amerika na Ulaya tuu... kwanini yasitokee China & Africa pia. Zaidi ya 90% ya kesi zote za kuonekana kwa hawa viumbe na ndege sahani zao ni huko Ulaya na America tuu... mbona wako biased kivile..??
Wanaosema Aliens wapo points zao ni kuwa;
01. Ulimwengu wetu huu ni mkubwa sana na unaendelea kutanuka (expand) kwa speed ya mwanga tangu uripuke kutoka kwenye bigbang... sasa kuna mabilioni ya Sayari na mifumo ya jua mingi sana ndani ya Galaksi (Galaxy) kibao ndani ya huu ulimwengu wetu na Sayari nyingi zinaweza stawisha maisha (potentially habitable planets)... sasa kwa fikra yako tuu kwa ukubwa wote huu wa Ulimwengu utaamini kuwa tupo peke yetu..???
02. Kuonekana kwa ndege sahani (Flying Saucer au Unidentified Flying Objects - U.F.O) mara kwa mara.
(hili sitoliongelea... nendeni mkacheki YouTube huko wanaupload video za hivi vitu kila uchwao ingawa siamini kama ni za kweli).
03. Antartica.
Inaaminika kuwa hii ndo base ya Aliens hapa Duniani. Kuna story nilisoma kuwa Google Earth satelites zilinasa picha zikiwa zinaonyesha shughuli zisizo za kibinadamu zikiwa zinaendelea huko Antarctica pia kuna mtalii (explorer) alikuta yaleyale na kupiga picha. Alikamatwa na kuambiwa asitoe siri juu ya alichokiona kule. Nchi zaidi ya 12 zimeingia mkataba kulilinda hili eneo ambalo ni barafu tupu... sasa kwa akili yako wanalinda nini pale..???
Sina nguvu ya ku-type kwa leo ila hayo machache yanatosha.
Kwenye Ulimwengu huu huwenda tupo pekee yetu au hatupo pekee yetu.... yote hayo yanaogofya.
Sent using
Jamii Forums mobile app