DNA yaendelea kuleta balaa kwa wanandoa

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,745
21,196
Mwanamke mmoja amechakazwa vibaya na mwanamme anayedhaniwa kuwa ni Mme wake baadaya kutokea hali yenye utata dhidi ya watoto wao.

Mwanaume huyo tajiri na mfanyabiashara alikuwa na mpango wa kuhamisha family yake kutoka nchini Benin kwenda nchini Canada ndipo ubalozi wa Canada nchini Benin ulipohitaji Vipimo vya DNA kwa watoto wake hao watatu kwa kuhofia kuwa huenda alikuwa akitaka kusafirisha watu wasiokuwa na uhusiano naye kinyume cha sheria (human trafficking).

Vipimo vilikuja na majibu kuwa bwana huyo siyo baba halali wa watoto wote watatu hivyo ufanyike utaratibu mwingine wa kupata Visa na taratibu zingine za kisheria ili aruhusiwe kuingia Canada.

Aliporudi nyumbani kumhoji mke wake juu ya baba halali wa watoto hao na kwanini amekuwa msaliti kwa kiwango cha hatari kiasi hicho lakini hakupata majibu ya kueleweka.

Jamaa akaamua amuue kabisa lakini watu wakawahi kuokoa uhai wa mwadada huyo huku meno manne yakiwa yameng'olewa kwa ngumi nzito nzito alizosukumiwa.

Bado taarifa zaidi hazijatolewa kuhusu kukamatwa kwa mwanaume huyo, lakini tunaendelea kupeana taarifa kwa undani hapa JF.

IMG-20200226-WA0001.jpg

👆Picha baada ya kibano kikali kutoka kwa Jamaa anayesadikiwa kuwa ni mumewe.

IMG-20200226-WA0000.jpg

👆 Kabla ya mipango kuvurugika hapo walikuwa wakila kuku kwa mikono.
 
Mimi nina watoto kibao wanalelewa na njemba wakidhani ni wa kwao
Unajua mwanao ananiita dady, nampeleka shule namrudisha nyumbani baada ya kazi?

Nalipa ada, ada usizokumbuka kutoa, mwanao amefikia balehe na nimemfunza kunyoa...

Nimemfunza ushahiri nimefunza kufanya mahesabu, nimemfunza kufunga tai kisha kamba za viatu...

Nimemfunza sheria zinazoongelewa bungeni, na nilienda kumtetea alipoonewa shuleni...

Una hoja yeyote defensively? Maana hujui ka' wanalala ama wanaamka safely...

It's Scars
 
Asante kwa kumlea mwanangu. Mama yake tukichepuka tunakuchekaga sana tukirukaruka kitandani👌😆😬
 
Back
Top Bottom