Kwanza nianze kwa kukupa pole, Pamoja na jukumu zito ulilo nalo la Kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020 ni wa kuaminika na shirikishi kwa Watanzania. Bado wapo Watanzania wachache kwasababu ya UBINAFSI wao wanataka kukutoa kwenye RELI, Usikubali!
Umeianza Safari yako Vizuri sana na kwa weledi Mkubwa tangu uandikishaji wa Wapiga Kura ambapo kinyume na matarajio, Ulivuka lengo kwa kuongeza Wapiga Kura wapya zaidi ya Milioni Sita. Sisi Watanzania tunayaona Mafanikio haya Makubwa na yanayoweka Uhalali wa kazi unayoisimamia. Muamko Mkubwa wa Wananchi kuwa na hamu ya kupiga Kura na shauku yao ya kutaka kufahamu mambo mablimbali kuhusu Uchaguzi ni kiashiria cha mafanikio makubwa katika kufanikisha Mchakato huu Muhimu kwa Taifa Letu.
Juzi nimekusikia ukiyasema mahitaji ya Watanzania kwa sasa wakati unuawaasa Wagombea kufuata Maadili ya Kampeni, Jambo ambalo ni sahihi na Ukweli Mtupu. Mahitaji yale yamewekwa pia katika ilani ya Vyama vyote vinavyoomba kura kwetu sisi Wananchi, Lakini Chama kimoja kimeibuka na kusema unafanyia kampeni chama kingine, hili linatafakarisha sana juu ya baadhi ya Wagombea wetu wanakotaka kutupeleka, Nakuhisi Daktari Usiwape nafasi, Simamia Msimamo wako huo huo.
Maadili ya Kampeni ni Makubaliano ya vyama vyote vya siasa, hivyo tuseme vyama vyote vimeshiriki kikamilifu na wanajua nani akikosea awajibishwe wapi, kama ambavyo pingamizi zilifahamika sehemu sahihi ya kuzipeleka, Rufaa pia kwa baadhi ya wagombea waliojitambua. Naamini Malalamiko juu ya Maadili yana mahala pake pa kupelekwa zaidi ya Majukwaani ambako ukitafakari kwa kina Malalamiko hayo yanaposemwa jukwaani yana lengo moja tu kupandikiza chuki kwa Wananchi ili izae vurugu na Machafuko, Simama Imara hivyo hivyo.
Ninaamini Msimamo wako ndio Msimamo wa Mwenyekiti wako Jaji Kaijage na Makamishna wake pia, Msikubali Vitisho vya watu wachache viwaondolee Credibility yenu na Legacy mliyoanza kuijenga. Naamini mtamaliza jukumu hili na Tanzania itabaki salama kuliko wakati mwingine wowote.
Nimalize kwa kukupongeza kwa kuimarisha Uwazi na Ushirikishaji unaofanywa na Tume unayoisimamia keep it up Brother!
Ni msimamo wake au wa kupewa?