Dkt. Wilsom Mahera simamia msimamo wako

Dkt. Wilsom Mahera simamia msimamo wako

Singo Batan

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2020
Posts
304
Reaction score
213
Kwanza nianze kwa kukupa pole, Pamoja na jukumu zito ulilo nalo la Kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020 ni wa kuaminika na shirikishi kwa Watanzania. Bado wapo Watanzania wachache kwasababu ya UBINAFSI wao wanataka kukutoa kwenye RELI, Usikubali!​

Umeianza Safari yako Vizuri sana na kwa weledi Mkubwa tangu uandikishaji wa Wapiga Kura ambapo kinyume na matarajio, Ulivuka lengo kwa kuongeza Wapiga Kura wapya zaidi ya Milioni Sita. Sisi Watanzania tunayaona Mafanikio haya Makubwa na yanayoweka Uhalali wa kazi unayoisimamia. Muamko Mkubwa wa Wananchi kuwa na hamu ya kupiga Kura na shauku yao ya kutaka kufahamu mambo mablimbali kuhusu Uchaguzi ni kiashiria cha mafanikio makubwa katika kufanikisha Mchakato huu Muhimu kwa Taifa Letu.​

Juzi nimekusikia ukiyasema mahitaji ya Watanzania kwa sasa wakati unuawaasa Wagombea kufuata Maadili ya Kampeni, Jambo ambalo ni sahihi na Ukweli Mtupu. Mahitaji yale yamewekwa pia katika ilani ya Vyama vyote vinavyoomba kura kwetu sisi Wananchi, Lakini Chama kimoja kimeibuka na kusema unafanyia kampeni chama kingine, hili linatafakarisha sana juu ya baadhi ya Wagombea wetu wanakotaka kutupeleka, Nakuhisi Daktari Usiwape nafasi, Simamia Msimamo wako huo huo.​

Maadili ya Kampeni ni Makubaliano ya vyama vyote vya siasa, hivyo tuseme vyama vyote vimeshiriki kikamilifu na wanajua nani akikosea awajibishwe wapi, kama ambavyo pingamizi zilifahamika sehemu sahihi ya kuzipeleka, Rufaa pia kwa baadhi ya wagombea waliojitambua. Naamini Malalamiko juu ya Maadili yana mahala pake pa kupelekwa zaidi ya Majukwaani ambako ukitafakari kwa kina Malalamiko hayo yanaposemwa jukwaani yana lengo moja tu kupandikiza chuki kwa Wananchi ili izae vurugu na Machafuko, Simama Imara hivyo hivyo.​

Ninaamini Msimamo wako ndio Msimamo wa Mwenyekiti wako Jaji Kaijage na Makamishna wake pia, Msikubali Vitisho vya watu wachache viwaondolee Credibility yenu na Legacy mliyoanza kuijenga. Naamini mtamaliza jukumu hili na Tanzania itabaki salama kuliko wakati mwingine wowote.​

Nimalize kwa kukupongeza kwa kuimarisha Uwazi na Ushirikishaji unaofanywa na Tume unayoisimamia keep it up Brother!​
 
Unamuongelea huyu ayeongea kwa unyenyekevu kwa boss wake?
Screenshot_2020-09-28-13-03-17-1.jpg
 
Aibu tupu

Mkurugenzi amekuwa mpiga kampeni badala majukum yake ya kusimamia timu za vyama husika?

He is disappointing all of us and doesn't fit in either case
 
Nafasi ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepwaya. Nahisi kwa mara ya kwanza Tume ndo imempata Mkurugenzi aliyepwaya tangu kuundwa kwa NEC
 
Ni kweli anatakiwa kusimama kwenye njia moja tu ya kusimamia Sheria asitishwe na vibaraka hawa ambao wanataka kutuharibia amani Yetu iliyolindwa kwa gharama sisi wananchi tupo pamoja nae kazi yake inaonekana zoezi hili atalimaliza kwa mafanikio makubwa Sana
 
Mahera huyu huyu au mwingine ?
 
Mzee Lubuva na uzee wake alikua mtu bora na mwenye busara kuliko huyu mnafiki wa sasa,no wonder alitukanwa na Jerry Muro kwa kuitwa mpuuzi,hakika ni mpuuzi
 
Attachments

  • VID-20200929-WA0008.mp4
    2.7 MB
Kwanza nianze kwa kukupa pole, Pamoja na jukumu zito ulilo nalo la Kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020 ni wa kuaminika na shirikishi kwa Watanzania. Bado wapo Watanzania wachache kwasababu ya UBINAFSI wao wanataka kukutoa kwenye RELI, Usikubali!​

Umeianza Safari yako Vizuri sana na kwa weledi Mkubwa tangu uandikishaji wa Wapiga Kura ambapo kinyume na matarajio, Ulivuka lengo kwa kuongeza Wapiga Kura wapya zaidi ya Milioni Sita. Sisi Watanzania tunayaona Mafanikio haya Makubwa na yanayoweka Uhalali wa kazi unayoisimamia. Muamko Mkubwa wa Wananchi kuwa na hamu ya kupiga Kura na shauku yao ya kutaka kufahamu mambo mablimbali kuhusu Uchaguzi ni kiashiria cha mafanikio makubwa katika kufanikisha Mchakato huu Muhimu kwa Taifa Letu.​

Juzi nimekusikia ukiyasema mahitaji ya Watanzania kwa sasa wakati unuawaasa Wagombea kufuata Maadili ya Kampeni, Jambo ambalo ni sahihi na Ukweli Mtupu. Mahitaji yale yamewekwa pia katika ilani ya Vyama vyote vinavyoomba kura kwetu sisi Wananchi, Lakini Chama kimoja kimeibuka na kusema unafanyia kampeni chama kingine, hili linatafakarisha sana juu ya baadhi ya Wagombea wetu wanakotaka kutupeleka, Nakuhisi Daktari Usiwape nafasi, Simamia Msimamo wako huo huo.​

Maadili ya Kampeni ni Makubaliano ya vyama vyote vya siasa, hivyo tuseme vyama vyote vimeshiriki kikamilifu na wanajua nani akikosea awajibishwe wapi, kama ambavyo pingamizi zilifahamika sehemu sahihi ya kuzipeleka, Rufaa pia kwa baadhi ya wagombea waliojitambua. Naamini Malalamiko juu ya Maadili yana mahala pake pa kupelekwa zaidi ya Majukwaani ambako ukitafakari kwa kina Malalamiko hayo yanaposemwa jukwaani yana lengo moja tu kupandikiza chuki kwa Wananchi ili izae vurugu na Machafuko, Simama Imara hivyo hivyo.​

Ninaamini Msimamo wako ndio Msimamo wa Mwenyekiti wako Jaji Kaijage na Makamishna wake pia, Msikubali Vitisho vya watu wachache viwaondolee Credibility yenu na Legacy mliyoanza kuijenga. Naamini mtamaliza jukumu hili na Tanzania itabaki salama kuliko wakati mwingine wowote.​

Nimalize kwa kukupongeza kwa kuimarisha Uwazi na Ushirikishaji unaofanywa na Tume unayoisimamia keep it up Brother!​

Punguza upuuzi.
 
Huyo Mahaera hawezi kuwa na msimamo zaidi ya kutekeleza alichotumwa. Huyu ni mukurugenzi wa hovyo katika history ya Tume.
 
Zimeingia kwenye afya, barabara, maji, umeme........ ulitaka ukabidhiwe wewe mwenyekiti wa kitongoji?
Vumilia hapohapo sababu awamu hii ya pili atawapatia zaidi ya hizo ila chini ya miradi ya maendeleo ya vijiji
Nakubali sana tu.
Screenshot_2020-09-17-22-19-17-1.jpg
 
Huyo Mahera asimsmie msimamo upi ? Wa kuvuruga uchaguzi? Anawaambia upinzani watangaze sera watu wanataka maji , miundombinu , afya haya Sasa sera Safi kabisa kutoka kwa baba yake mbona yeye hamwambia wananchi wanataka nini?
IMG_20200929_223621.jpg
 
Unaandika kwa aya vizuri kumbe umeandika pumba tupu!

Eti wananchi wanataka umeme na barabara nzuri!Tokea lini mkurugenzi wa tume akawa msemaji wa wananchi?
 
Back
Top Bottom