Dkt. Stergomena Tax amaliza muda wake SADC

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
E9EVvP7WUAgqlr4.jpg

Dkt. Stergomena Tax akiwa na mrithi wake Bw. Elias Mpedi Magosi, raia wa Botswana


Katibu Mkuu wa nne wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena Tax amemaliza muda wake

Dkt. Stergomena alichukua nafasi hiyo September 2013 na ameaga rasmi Agosti 2021

Elias Mpedi Magosi amechukua nafasi yake kuanzia sasa

Katika posti yake kwenye mtandao wa Twitter, Dkt. Tax amempongeza na kumtakia kila la kheri Bw. Magosi katika safari yake ya kuongoza jumuia hiyo

"Hongera Mheshimiwa Elias Magosi kwa kuteuliwa kwako kama Katibu Mtendaji wa 7 wa SADC. Nakutakia kila mafanikio unapoanza kazi yako inayoanza tarehe 1 Septemba 2021. Pula!", ameandika Dkt. Tax

===

Katika hotuba yake ya kuaga kama kiongozi wa Jumuiya hiyo, Dkt. Sergomena Tax amesema:

Safari yangu kama Katibu Mkuu wa SADC ilianza Agosti 18, 2013 nilipochaguliwa na kuapishwa hapa Lilongwe. Mungu ameona ni vyema pia safari yangu kwenye nafasi hii ikaisha katika Mji huu

Namshukuru Mungu kwa kuanza salama na kumaliza salama kazi hii

Naomba pia kutoa shukran zangu za dhati kwa Serikali yangu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa heshima na kunipendekeza mimi kushika nafasi hii kati ya mamilioni ya Watanzania wenye sifa

Ninaondoka wakati Jumuiya imesimama vizuri kwenye maeneo mengi japo kuna machache yanayohitaji kutazamwa kwa umakini

Maeneo hayo ni kama Ukosefu wa Ajira, Umasikini, Magonjwa ya Mlipuko, Majanga, Ugaidi, Fujo na Mashambulio ya Usalama wa Kimitandao

Ninaondoka wakati Kiswahili kimekuwa moja ya Lugha za SADC

Nafarijika sana kama mwana SADC kwa kutambua mchango wa Lugha ya #Kiswahili katika ukombozi Kusini mwa Afrika na kama Mtanzania kwani ni Lugha ya Taifa langu

Najivunia na daima nitajivunia Umoja unaooneshwa na Nchi Wanachama wa SADC

Nakumbuka jinsi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyokuwa akihubiri kuhusu Umoja na Mshikamano kwa Nchi zilizo Kusini mwa Afrika

Desemba 1980 akiwa Bulawayo, Zimbabwe Mwl. Nyerere alisema "Tumeungana wakati tunapigania Uhuru, tumeungana tukiwa Huru Kisiasa, tuendelee kuungana tukipigania Ukombozi wa Kiuchumi na Maendeleo. Twende mbele tukiwa pamoja"

Kwenye SADC kuna Viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye amethibitisha kuwa Wanawake wana uwezo mkubwa wa kuongoza Mataifa kwa Umahiri na Busara

Tuendelee kumuunga mkono Kimataifa, Kikanda na Kitaifa


PIA, SOMA:
-
Elias Mpedi Magosi, mrithi wa Dkt. Stergomena Tax kiti cha Ukatibu Mkuu wa SADC
 
Hongera sana Dr. Stergomena Tax, hakika ameiwakilisha vyema Tanzania ktk nafasi yake aliye hudumu kwa miaka 8.

Dr. yuko vizuri sana tena sana hivyo Serikali yetu sasa imtumie ktk ujenzi wa Taifa lake.
 
Jina lake mbona kama halina asili ya kibantu

Mwenye wasifu wake auweke hapa nami nimfahamu uyu Daktari
 
Back
Top Bottom