Dkt.Slaa tunakushukuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dkt.Slaa tunakushukuru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaFalsafa1, May 3, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Dkt.Slaa tunakushukuru,kumbe watetezi wetu bungeni ni feki
  Written by Administrator
  Saturday, 02 May 2009 15:32
  Na Edson Kamukara

  ALIANZA kazi ya utetezi wa watu na wengi wakamwona kama mkombozi na kumuunga mkono,mara zote hakuchoka kuibua maovu aliyoyabaini japokuwa alifanya akifahamu dhahiri kuwa anawakwaza walafi na waroho wa madaraka na mali.

  Amejitahidi kutembelea maeneo mengi ili kuwafungua macho maskini na kuwapa ukweli wapi zilipo mali zao,na jambo zuri katika kazi hii kuna wenzake walijipendekeza kuungana naye kwa maneno kuwa nao ni watetezi wa wanyonge kumbe walitafuta tu mahala pa kutokea kisiasa ili wapate umaarufu kama yeye.

  Namzungumzia Dkt.Peter Wilbroad Slaa,Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiongozi ambaye amejizolea umaarufu ndani na nje ya Bunge kutokana na msimamo wake wa kupambana na rushwa bila woga ili kuhakikisha viongozi wabovu wanawajibishwa.

  Tangu ameingia bungeni mwaka 1995 Dkt.Slaa amekuwa mwanasiasa asiyeyumbishwa na hii inatokana na mwenyewe kujiridhisha kwanza kwa kufanya utafiti wa kile anachokuwa amekusudia kukiibua kwenye Bunge ama nje katika majukwaa ya kisiasa.

  Kwa kifupi kabisa kama ni umaarufu,sifa ama kuaminika kwa watu basi Dkt.Slaa anavyo tangu zamani siyo kwamba sasa hivi anatafuta umaarufu kama wanasiasa majitaka wanavyodhania,na bahati mbaya sana kuna wanasiasa wengi na hasa wabunge wa CCM walikuwa wakitumia mgongo wa hoja za mbunge huyu kuwarubuni wananchi waamini nao ni wapambanaji kumbe siyo kweli.

  Katika Biblia takatifu tunaambiwa kuwa Bw.Yesu baada ya kuwa amefanya miujiza ya kubariki mikate mitano na samaki wawili vikaongezeka na watu wakala na kusaza,kuna ambao walitaka kwendelea kufuatana naye kila mahali kwa sababu tu ya kwendelea kunufaika na miujiza ya chakula,lakini aliwakatalia baada ya kujua nia yao hiyo.

  Hata Dkt.Slaa baada ya umaarufu wake kwa Watanzania kuwa mkubwa kuna watu wenye roho nyepesi wamekwishaanza kufikiri kuwa mbunge huyu anataka kugombea urais na wengine wanahofia hata anapopita majimboni kwao kufanya mikutano ya kuimarisha chama chake wanadhania kuwa njia rahisi ni kubembea mabegani mwake ili nao waonekane ni wapambanaji kama yeye,lakini amewajua na kujitenga nao.

  Jumanne ya Aprili 22 mwaka huu siku ambayo kikao Bunge kilianza mjini Dodoma,Dkt.Slaa alijikuta anageukwa na kushambuliwa kwa maneno makali yenye vitisho na kebehi toka kwa wabunge wenzake wakidai kuwa aliwaudhi kwa kutaja mishahara yao na marupurupu wanayoyapa mbele ya wapiga kura wao.

  Mimi siyo hakimu wa Pilato aliyemhukumu Bw.Yesu,lakini kama Dkt.Slaa angeletwa mbele yangu kwa mashtaka hayo basi kwanza ningempongeza kwa ukweli wake,pili ningemshukuru kwa kuweza kutusaidia kutambua kwamba kumbe hatuna watetezi Bungeni bali wataka mishahara minono na mwisho ningemwambia kuwa sioni hatia yoyote kwake zaidi ya kumshauri atuibulie na mengine.

  Kwa wale wapenda kutazama simema watakubaliana nami kuwa hata mabomu ya Dkt.Slaa mwanzoni huonekana kama sinema na viongozi wengi wa serikali na CCM hujaribu kuwaaminisha wananchi kuwa mbunge huyo ni mzushi wasimwanini lakini mwishowe ukweli hujitokeza na watu kuamini kuwa tuhuma za Dkt.Slaa siyo sinema.

  Bila kuwapeleka mbali ebu tujikumbushe tuhuma za wizi wa fedha katika akaunti ya malipo ya nje kwenye Benki kuu ya Tanzania. Dkt.Slaa alipoanza kuhoji Bungeni akitaka kufahamu kama waziri wa fedha ameona habari kwenye mtandao zikidai BoT kuna ubadhilifu,waziri,spika na wabunge wote wa CCM walimwona kama mzushi na mwongo.

  Lakini kwa ujasiri wake Dkt.Slaa aliendelea na hoja ile na hatimaye akaomba kuwasilisha hoja binafsi bungeni juu ya hilo,na hapo ndipo muziki ilipoanzia kwani Spika wa Bunge Bw.Samwel Sitta alifanya kila awezavyo hadi akapangua hoja hiyo isiwasilishwe huku akidai vielelezo vya mbunge ni vya kughushi.

  Spika Sitta bila aibu akiwa amealikwa katika mdahalo kwenye televisheni ya Taifa TvT wakati huo,alisema wazi mbele ya Dkt.Slaa kuwa vielelezo vyake ni vya kughushi vyenye ushahidi dhaifu wa kwenye matando (internet),na kudai kuwa amewaagiza vyombo vya dola vimchunguze na kumchukulia hatua ili kukomesha tabia hiyo ya kuzua mambo.

  Oktoba 15 mwaka 2007,Dkt.Slaa bila kujali chochote aliamua kuihamishia hoja yake hiyo jukwaani katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke Dar es Salaam na kutaja orodha ya vigogo kumi na moja aliodai ndiyo walikwapua fedha katika EPA.

  Kilichofuata tunakikumbuka kuwa baada ya rais kuunda tume pale BoT ilibainika kuwa kiasi cha sh.bilioni 133 zilikuwa zimeporwa na makampuni hewa kama ushahidi wa Dkt.ulivyokuwa ukionesha. Gavana alifukuzwa kazi na kinachoendelea watuhumiwa wengine wamekamatwa na kufikishwa mahakamani huku wengine wakiambiwa warejeshe fedha na kusamehewa.

  Haya ndiyo matunda ya Dkt.Slaa ambaye awali tuliaminishwa kuwa ni mwongo mwenye ushahidi wa kughushi lakini Mungu ametenda miujiza leo ukweli wake umebainika na tangu hapo wako wabunge ndani ya CCM wameanza kuimba kuwa nao wanapambana na ufisadi ndani ya serikali na chama chao,japokuwa tukio la karibuni alilofanyiwa Dkt.Slaa na baadhi ya wabunge wenzake limebainisha kuwa wapambanaji wa ukweli ni wachache mno.

  Kitendo cha baadhi ya wabunge wa CCM na upinzani tena wale ambao awali tulidhania ni wapigania wanyonge kama Bw.Lucas Selelii(CCM),Bw.John Cheyo(UDP),Bi.Anna Komu(Chadema),Bw.Lazaro Nyalandu(CCM)na wengine kuhoji eti kwanini Dkt.Slaa ametaja hadharani mishahara na marupurupu yao kwa wapiga kura.

  Wabuge hawa walitaka kujua ni hatua gani zimechukuliwa na Bunge kutokana na kitendo hicho walichodai ni cha kukiuka maadili,wako waliofikia hata hatua ya kwenda mbali zaidi wakimuonya mbunge huyo kuwa aache mara moja tabia hiyo wakidai kuwa anajitafutia umaarufu wa kugombea urais.

  Ziko taarifa za chini chini kuwa baadhi ya wabunge wameanza kuandaa makakati wa kumuondoa Dkt.Slaa katika uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LARC)ili liwe fundisho na kupunguza makali yake.

  Mimi nawapongeza wabunge hawa na wengine kwa mawazo yao hayo na misimamo hiyo wanayokusudia kufanya kama kweli ndiyo nia zao,maana yawezekana ni kweli walikuwa hawataki kabisa wapiga kura wao wafahamu wanalipwa mshahara na marupurupu kiasi gani ili wasije kuwasumbua kuwaomba misaada.

  Pengine tujiulize ni kwanini waheshimiwa hawa hawataki wajulikane wanalipwa kiasi gani mpaka wafikie kumchachamalia Dkt.Slaa kiasi hicho, na je ni kweli mbunge huyu alikosea ama alikuwa sahihi kwa vile anachokitetea ni fedha hiyo itakayokatwa ipelekwe kuwasaidia wanyonge.

  Katika hoja yake Bw.Nyalandu (CCM)alisema kuwa Dkt.Slaa anajitafutia umaarufu majukwaani ili kujijenga kisiasa kwani hata kama wabunge wakipuguziwa mishahara na marupurupu yao bado fedha hiyo haiwezi kuwasaidia Watanzania wote,isipokuwa cha kufanya ni kutafuta utaratibu mzuri wa kuinua maisha ya masikini.

  Katika hili, mimi nadhani inabidi wabunge waache kuogopa vivuli vyao kwa hofu kuwa kila anayefanya jambo zuri na kupendwa na jamii basi anakuwa anatafuta umaarufu wa kugombea uongozi kama udiwani,ubunge au urais.

  Wabunge lazima wakubali kuwa wanalipwa mishahara na marupurupu makubwa na pengine tofauti na kazi wanazozifanya katika kuwawakilisha wananchi ama ikilinganishwa na elimu zao,na kumbe hii ndiyo sababu inayowakimbiza wasomi na wadau mbalimbali kukimbilia kwenye siasa na kufanyiana kila hila kwenye majimbo ilimradi waupate ubunge kwa vile kuna ulaji.

  Wako watumishi wasomi wenye elimu kubwa kuliko za baadhi ya wabunge na wameitumikia serikali hii kwa muda mrefu kwa kufanya kazi nzito sana lakini ukitajiwa mishahara na marupurupu yao kama una roho nyepesi unaweza kuzimia,sasa kwanini tusimuunge mkono Dkt.Slaa kuwa wapo wabunge ambao elimu zao ni ndogo sana na hata majimboni kwao hawajafanya jambo lolote la maana ikilinganishwa na mchango wa watumishi wengine.

  Sina maana kwamba wabunge wote hawawajibiki. La hasha!,wapo na wamefanya kazi nzuri za kuwatetea wananchi kwa nguvu kubwa sana kama Dkt.Slaa na wengine, isipokuwa wanalipwa mishahara na marupurupu ni makubwa hali ambayo inaongeza pengo baina yao na masikini.

  Kwanini tusiseme Dkt.Slaa tunakushukuru,maana kumbe hatuna wabunge wa kutetea matatizo yetu badala yake wako wanaolilia mishahara yao iwe mikubwa lakini wapiga kura hatutakiwi kufahamu wanalipwa kiasi gani.

  Hoja ya Dkt.Slaa ni kwamba kama gari moja la waziri(shangingi)linagahrimu sh.milioni 120 wakati zahati moja ya pale Urambo inagharimu sh.milioni 80,kwanini mishahara ya wabunge ukiwemo wa kwake isikatwe kodi au ipunguzwe ili kupunguza matumizi na kutatua kero za wapiga kura?

  Wabunge hawa walitaka Dkt.Slaa aisemehe hoja yake wapi kama si kwa mabosi wao ambao ndio wamewaajiri na kuwawezesha kupata mishahara na marupurupu hayo wanayotaka kumtoa nayo roho mbunge mwenzao.

  Mbona ni wabunge hawa hawa tunaowaona kila bajeti wakijifanya kutaja mishahara na marupurupu ya walimu na polisi Bungeni na majukwani wakidai watumishi hawa pamoja na kufanya kazi kubwa lakini serikali imewasahau,sasa iweje hawako tayari kupunguzwa mishahara wao ili wanufaike na wenzao?

  Ndiyo wakati huu ni mgumu sana kwa Dkt.Slaa kwa vile kila mmoja atamnyooshea kidole kwa vile amegusa maslahi yao,huu ndiyo mfano wa mlevi kwani utakunywa naye pombe muda wote mkiwa pamoja ila ukitaka kumkorofisha na kuwa adui basi mwaga pombe yake uone nini kitatokea.

  Spika wa Bunge Bw.Sitta alimtukana Dkt.Slaa tusi la ngoni japokuwa ilikuwa katika mithili ya utani kwa kusema kuwa mbunge huyo pamoja na kwamba hoja zake zimejaa upotoshaji,bado ataendelea kuwa mwenyekiti wa kudumu wa Bunge wa kamati ya LARC,lakini hivi ni vikwazo na kauli za kukatisha tamaa ambazo zimeandaliwa kumdhoofisha mbunge huyo hivyo hana budi kuwaona wahusika kama wafa maji.

  Nasema tena kuwa wale wanaofikiria Dkt. Slaa anatafuta umaarufu wakati huu wajue kabisa wamepotoka kwa vike umaarufu alikwishakuupata na anachokifanya ni kuwashawishi watanzania wafungue macho ili katika uchaguzi ujao wachague wawakilishi wenye kuwajali na kuwatete badala ya hawa wenye kuangalia kwenda Bungeni kutajirika.

  Laiti kama wabunge wote wangesimama kidedea kama Dkt.Slaa na kuisimamia serikali basi hizi kero za EPA,Richmond,wizi wa fedha ya wafadhili wa Norway katika wizara ya Maliasili na Utalii,Rada,ndege mbovu ya rais,mikataba mibovu ya madini visingekuwepo nchini tena,maana wahusika wangekuwa gerezani zamani. tunakushukuru,kumbe watetezi wetu bungeni ni feki

  Laiti kama wabunge wote wangesimama kidedea kama Dkt.Slaa na kuisimamia serikali basi hizi kero za EPA,Richmond,wizi wa fedha ya wafadhili wa Norway katika wizara ya Maliasili na Utalii,Rada,ndege mbovu ya rais,mikataba mibovu ya madini visingekuwepo nchini tena,maana wahusika wangekuwa gerezani zamani.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Asante na hongera ndugu Slaa.Mengine tutayasema baadaye
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwakweli hii makal ina mguso mkubwa sana, natamani ingewezekana ikatolewa copy na kusambazwa kwa wabunge wote! Labda yaweza kuwasaidia kuwarudisha katika ufahamu/sense wao badala ya kuwa wachumia tumbo!
   
Loading...