Dkt. Serera aipongeza posta kwa ubunifu wa usafirishaji

Dkt. Serera aipongeza posta kwa ubunifu wa usafirishaji

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
DKT. SERERA AIPONGEZA POSTA KWA UBUNIFU WA USAFIRISHAJI

📍Nanenane, Dodoma
🗓️ 06 Agosti, 2025

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amelipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa hatua kubwa ilizopiga katika utoaji wa huduma kwa njia za kidigitali pamoja na ubunifu wake katika sekta ya usafirishaji.

Amezungumza hayo wakati alipotembelea banda la Shirika la Posta tarehe 06 Agosti, 2025 katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, huku akisisitiza kuwa huduma za usafirishaji kupitia Posta ni nyenzo muhimu kwa wakulima na wafanyabiashara kufikisha bidhaa sokoni kwa wakati na kwa usalama.

Aidha, Dkt Serera amehimiza matumizi ya Postikodi sahihi katika shughuli za usafirishaji, akieleza kuwa ni nyenzo ya msingi kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma hususani kwa wakulima hadi mahali walipo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
 

Attachments

  • IMG-20250807-WA0109.jpg
    IMG-20250807-WA0109.jpg
    85.1 KB · Views: 10
  • IMG-20250807-WA0107.jpg
    IMG-20250807-WA0107.jpg
    466.4 KB · Views: 13
  • IMG-20250807-WA0110.jpg
    IMG-20250807-WA0110.jpg
    486.2 KB · Views: 11
  • IMG-20250807-WA0113.jpg
    IMG-20250807-WA0113.jpg
    417.2 KB · Views: 12
Back
Top Bottom