Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasihi viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla kutumia kipindi cha toba cha Ramadhani na Kwaresma kuiombea nchi, viongozi wa serikali na vyama vya siasa ili kuendelea kujenga taifa lenye upendo, amani na mshikamano.
Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki futari aliyoiandaa kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na viongozi wa serikali, taasisi za dini na Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyofanyika mkoani Dodoma.
Amesema jambo muhimu ni kuhakikisha hamasa ya mapenzi ya nchi inakuwepo kwa kila mmoja, huku chemchem ya uzalendo ikijengeka katika mioyo ya Watanzania ili waishi kwa kupendana na kushirikiana chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Makamu wa Rais amesema moja ya mambo muhimu ya kufanya katika kipindi cha toba ni kumwahidi Mwenyezi Mungu kuwa kila Mtanzania atajitahidi kuwaunganisha Watanzania wenzake ili kuijenga nchi kuwa taifa moja lenye upendo.
Futari hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, Waziri wa Madini Anthony Mavunde, wajumbe wa Kamati ya Maridhiano, viongozi wa dini, wabunge wa Mkoa wa Dodoma, wakuu wa wilaya pamoja na wananchi.