GE2025 Dkt. Nchimbi: CCM kugharamia matibabu ya saratani na figo ndani ya siku 100 za kwanza madarakani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,233
Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewakumbusha Watanzania kuhusu ahadi za Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizoziahidi kutekeleza ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza tena nchi.

Amesema hayo alipowasili katika Kata ya Mkula, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, leo Septemba 1, 2025, kwa ajili ya kunadi sera na ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025–2030.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa, ndani ya siku 100 za kwanza Madarakani, Serikali ya CCM itaanza kugharamia matibabu ya magonjwa yanayowatesa Watanzania, ikiwemo saratani na magonjwa ya figo.

Kwanini hawakufanya hivyo 2021-2025?
 
Wakati anahutubia kwanini wasianze sasa hivi?maana wanaongoza chama na serikali
 
Ivi hawa mbogamboga wanamuonaje mtanzania wa 2025 kama ni wale wa 1995...!!
 
Ahadi hizi ni matokeo ya CCM kuwa na hali mbaya hivyo inabidi watoe ahadi nzito kwa matumaini labda watanzania watawakubali japo kidogo.
 
Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewakumbusha Watanzania kuhusu ahadi za Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizoziahidi kutekeleza ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza tena nchi.

Amesema hayo alipowasili katika Kata ya Mkula, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, leo Septemba 1, 2025, kwa ajili ya kunadi sera na ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025–2030.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa, ndani ya siku 100 za kwanza Madarakani, Serikali ya CCM itaanza kugharamia matibabu ya magonjwa yanayowatesa Watanzania, ikiwemo saratani na magonjwa ya figo.

Kwanini wasianze leo!? Au serikali ijayo itatokea mbinguni??
 
Ocean Road tu hapo sahv kizungumkuti

Ova
 
Kabla ya utawala wa Samia matibabu ya Kansa ya shingo ya kizazi ilikuwa free,umeme kuingiza majumbani ilikuwa 27000,baada ya Samia kuwa in full charge kila kitu kikabadirika.
Matibabu ya kansa zote ikawa ni malipo.Umeme ukapanda bei,baada ya uchaguzi huu tegemea Sukari kupanda bei mara dufu
 
Kwanini wasioneshe mfano sahivi?
Waongo wazushi tu

Nishauguza mgonjwa alikuwa na pancreatic cancer mbilinge na gharama tulizopitia tunazijuwa

Hawa wanasiasa waache uhuni wa kucheza na akili za wajinga

Kwanini wasubirie mpaka uchaguzi uishe ndy watoe huo unafuu wanaosema

Huo ni uwongo uwongo tu

Ova
 
Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewakumbusha Watanzania kuhusu ahadi za Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizoziahidi kutekeleza ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza tena nchi.

Amesema hayo alipowasili katika Kata ya Mkula, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, leo Septemba 1, 2025, kwa ajili ya kunadi sera na ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025–2030.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa, ndani ya siku 100 za kwanza Madarakani, Serikali ya CCM itaanza kugharamia matibabu ya magonjwa yanayowatesa Watanzania, ikiwemo saratani na magonjwa ya figo.

Hawa matapeli hatudanganyiki
 
Aisee! Kwa hiyo shida ya Wananchi wa Busega ni Saratani kweli?
 
Back
Top Bottom