Nipe Maji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 335
- 190
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi ameielekeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha mradi wa usanifu na ujenzi wa bandari mpya ya Mbamba Bay, iliyopo Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma unakamilika kwa wakati na kwa viwango bora.
Dk Nchimbi ametoa maelekezo hayo leo Jumamosi, Aprili 5, 2025, baada ya kutembelea na kukagua mradi huo mkubwa na wa kimkakati na kupata maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Dk Baraka Mdima.
Dk Nchimbi amesema kukamilika kwa bandari hiyo kutachochea ukuaji wa biashara katika mikoa ya kusini pamoja na nchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Aidha, Dk Nchimbi ameipongeza menejimenti ya TPA kwa usimamizi mzuri wa mradi huo muhimu, ambao umetajwa kuwa miongoni mwa vipaumbele vya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Awali, akitoa taarifa kuhusu mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Baraka Mdima amesema mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miezi 24, unatarajiwa kukamilika kwa mujibu wa mkataba.