Dkt. Mwinyi akosa mahaba Zanzibar

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
Habarini wakuu.,

Nimeona kuna haja ya kuja na uzi huu, ni baada ya tathmini halisi iliyofanywa na wachambuzi mbali mbali kuhusu maendeleo ya wazanzibari wote unguja na pemba.

Sera ya Dr Mwinyi wakati wa uchaguzi ilikuwa ni ''yajayo yanafurahisha'' lakini sasa imekuwa ni kaa la moto baada ya mwaka mmoja na ushei hivi ambapo Dr Mwinyi akiwa madarakani kule Visiwa vya Zanzibar.

Wananchi wa Zanzibar wamejarib kulinganisha baina ya awamu iliyopita ya Dr Ali Mohamed Shein na sasa na kuona angalau kulikuwa na afadhali hapo kabla, mfano halisi ni huduma za maji safi na salama kwa vijiji na miji ya Unguja na Pemba wakati ule ilikuwa ni kwa 98% watu wa Zanzibar walikuwa wanapata maji kupitia mabomba na miundo mbinu ya serikali ambayo iliimarishwa na utawala wa Dr Shein ambapo sasa imekuwa ni kilio cha wananchi mbali mbali kisiwa cha unguja na hasa Pemba, wananchi wamekuwa wakifufua visima vyao vya asili na kuyatafuta maji mbali ikiwa ni pamoja na kubeba ndoo kichwani kwa akina mama na kina baba saa zote mitaani ni dumu za maji kwa gari za ngombe ama baiskeli au kwa kichwa takriban sasa ni muda usiojulikana hali hii imekuwa ikudumu bila ya suluhisho.

Lakini jengine ni ukali wa maisha vyakula kupanda bei ingawa hapo awali serikali ilikuja na jibu kwamba ni vita ya Russia na Ukrean ndio iliyosababisha., lakini watu wanajiuliza ni kwanini basi Dr toka aingie madarakani ameshindwa kujenga japo ka-barabara hata kilomita moja kote Zanzibar?

Wengine wansema kwamba Dr mwinyi inaonekana lengo na madhumuni yake si kuwaneemesha wazanzibar bali ni kuwalipisha makodi jambo ambalo ndio linaonekana sana toka aingie madarakani,

Ameanzisha mpango wa kujenga masoko ya bidhaa za kuuza chakula katika maeneo mbali mbali Zanzibar lakini wananchi pia wanajiuliza hivi wazanzibar walikuwa hawana masoko? au walilalamika kuhusu kutokuwa na uhabawa masoko mpaka kufikia kujengwa kila kona ya Zanzibar? lakini jibu likaja kwamba nia na madhumuni yake ni ile ile tu kufanya revenue collections kwa wananachi ambao wataingia na kuomba sehemu za biashara baada ya majengo hayo ya masoko kukamilika.

Watu ambao wametumbuliwa kuwa kuhujumu uchumi au kuiba fedha serikalini inaonekana hakuna tija, kwamba hata hao watu wakitumbuliwa maana fedha inayokusanywa ama kudhibitiwa maendeleo yake pia hayaonekani, Wazanzibar wanajiuliza fedha hizi tunazoambiwa zinaokolewa ziko wapi?

Natanguliza shukurani.
 
Lakini jengine ni ukali wa maisha vyakula kupanda bei ingawa hapo awali serikali ilikuja na jibu kwamba ni vita ya Russia na Ukrean ndio iliyosababisha., lakini watu wanajiuliza ni kwanini basi Dr toka aingie madarakani ameshindwa kujenga japo ka-barabara hata kilomita moja kote Zanzibar?

heb jaribu kutuliza kichwa uandike vitu kwa mpangilio unaoeleweka...km paragraph inahusu ukali wa maisha or vyakula stik to it sio unazungumzika vyakula then unachomekea mambo ya barabara
 
Mji wote umezungushwa mabati ila hakuna kinachofanyika.
Haya ni matatizo ya kuwa na rais wa mazoea.
 
Lakini jengine ni ukali wa maisha vyakula kupanda bei ingawa hapo awali serikali ilikuja na jibu kwamba ni vita ya Russia na Ukrean ndio iliyosababisha., lakini watu wanajiuliza ni kwanini basi Dr toka aingie madarakani ameshindwa kujenga japo ka-barabara hata kilomita moja kote Zanzibar?

heb jaribu kutuliza kichwa uandike vitu kwa mpangilio unaoeleweka...km paragraph inahusu ukali wa maisha or vyakula stik to it sio unazungumzika vyakula then unachomekea mambo ya barabara
soma ujumbe wote hutakosa cha kujib kama unahoja
 
Back
Top Bottom