Dkt. Mpango: Usalama wa Mikoa haupimwi kwa idadi ya Mapolisi, Risasi, Bunduki na Mabomu ya machozi

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1621161339878.png

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango

Kutokea hapa “S/M Simbawanga,” nawasalimu watu wa huko Dar es Salaam kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nikiwa natarajia kuwa kazi inaendelea! Huku “Simbawanga” tuko wazima.

Leo, nimeona kwenye TV Rais Samia akiapisha wakuu wapya wa mikoa na viongozi wengine aliowateua juzi. Mara baada ya kula viapo, wakubwa kadhaa walipata fursa ya kutoa nasaha kwa wateule hawa.

Nasaha za Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango, zimenigusa sana. Nilikuwa hapa “S/M Simbawanga” nikiwa nasahihisha madaftari ya wanafunzi, lakini ikanibidi nisitishe kidogo ili kumsikiliza vema.

Dk. Phillip Mpango amesema kwamba, mbali na jukumu la wakuu wa mikoa la kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao, kuna jukumu jingine. Kwamba, wakuu wa mikoa pia wanalo jukumu la kusimamia usalama wa kiuchumi katika maeneo yao.

Anachosema Makamu wa Rais hapa, ni kwamba, ajenda ya usalama wa mikoa, na hivyo ajenda ya usalama wa Taifa zima, ni zaidi ya kile ambacho tumezoea kukisikia kikitamkwa na baadhi ya watu wenye mtazamo wa kimapokeo juu ya usalama wa nchi.

Hapo zamani, kabla ya Taarifa ya Maendeleo ya Watu iliyotolewa na UNDP mwaka 1994, kutoa fasili pana ya usalama wa nchi, tulizoea kuambiwa kwamba, kazi ya kulinda usalama wa nchi inafanyika kwa kuimarisha usalama dhidi ya vitisho vya kijeshi.

Huu ni mtazamo kwamba, maana ya usalama wa nchi ni kuwa huru dhidi ya vitisho vya kijeshi kwa sababu ya kuwa na wanajeshi wenye ufundi wa kutumia bunduki, risasi, vifaru, mizinga na makombora ya kuwadungua maadui wa ndani na nje.

Lakini, kama alivyosema Makamu wa Rais, kwa kuzingatia mazingira ya sasa, ajenda ya usalama wa nchi imebadilika sana, kiasi kwamba, usalama wa kijeshi ni sehemu ndogo sana ya “Mikakati ya Usalama wa Kitaifa” (National Security Strategies).

Taarifa ya Maendeleo ya Watu iliyotolewa na UNDP mwaka 1994 ilisisitiza kwamba, kwa kuwa Taifa ni jumla ya watu, nchi na serikali yao, basi, “usalama wa Taifa” unapaswa kugusa maeneo saba ya usalama wa watu, yafuatayo:

  • Usalama wa kiuchumi, kwa maana ya haki ya kila raia kuwa huru dhidi ya umaskini wa kipato, ama kutokana na kujiajiri, kuajiriwa au program za usalama wa jamii;
  • Usalama wa lishe, kwa maana ya haki ya kila raia kupata mlo kamili mara tatu kwa siku;
  • Usalama wa kiafya, kwa maana ya haki ya kila kupata huruma za kiafya bila vikwazo vya kifedha, kijiografia au vinginevyo;
  • Usalama wa kiikolojia, kwa maana ya haki ya kila raia kuishi katika mazingira yaliyo huru dhidi ya wanyama waharibifu, wadudu wakali, mionzi ya jua, mafuriko, mmomonyoko wa ardhi, ukame, hali ya jangwa, maji yenye chumvi, uchafuzi wa anga kwa njia ya moshi, na mambo kama hayo.
  • Usalama wa mtu mmoja mmoja katika ngazi ya kisaikilojia na kimwili, kwa maana ya haki ya kila raia kuwa huru dhidi ya uteswaji, utekwaji, vitisho, vita vya kikabila, wizi, ukatili wa kiuchumi, ukatili wa kijinsia, na uhalifu.
  • Usalama wa jumuiya mbalimbali, kwa maana ya haki ya kila raia kujiunga na jumuiya zitakazompatia nembo ya utambulisho wa kiuchumi, kisiasa, kielimu, kitabibu, kitaaluma, kimbari, kikabila, kidini, kirika, kijinsia, au vinginevyo.
  • Usalama wa kisiasa, kwa maana ya haki ya kila raia kuishi kama mtu aliye hudu dhidi ya ukatili unaotekelezwa kupitia mikono ya chombo cha dola, ambapo maneno “chombo cha dola” yanamaanisha mtu yeyote au kikundi chochote kinachotekeleza majukumu yake kwa niaba ya Jamhuri.
Ukisoma “Mikakati ya Usalama wa Kitaifa” kwa ajili ya nchi mbalimbali utaona kwamba, mikakati hiyo inakubaliana na ukweli huu ulitamkwa kwa mara ya kwanza na UNDP.

Mikakati ya Usalama wa Kitaifa kwa ajili ya mataifa 204 duniani inapatikana kwenye anwani ifuatayo mtandaoni:
Mikakati ya Usalama wa Kitaifa Duniani.

Lakini, katika orodha hii hakuna “Mkakati wa Usalama wa Kitaifa” wa Tanzania. Na hauonekani mahali popote kwenye tovuti za serikali.

Maana yake ni kwamba, ama Tanzania hatuna “Mkakati wa Usalama wa Kitaifa” au upo lakini unafichwa fichwa, lakini kwa sababu ambazo, kwa maoni yangu, hazina uzito.

Vyovyote iwavyo, jambo hili ni dosari kubwa inayowanyima wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Mawaziri, na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali, kuwa na fokasi moja ya kiusalama.

Hapa naongelea ajenda ya usalama wa nchi ndani ya
pembetatu ya utawala, usalama na maendeleo. Haya matatu hayatenganishiki.

Kwa kweli, matarajio yangu ni kwamba, “Mkakati wa Usalama wa Kitaifa” lazima uwe na kifungu kinachosema kuwa, kila Halmashauri, kila Mkoa, kila Wizara, na kila Idara ya serikali, inapaswa kuwa na Mipango Mkakati ya Muda Mfupi na Mrefu, ili kwa njia hiyo, Taifa liweze kujipima katika kipengele cha kuweka na kusimamia mipango yake ya maendeleo.

Kama hivi ndivyo, kuna mtu anajua ni Halmashauri ngapi zilikuwa na mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita pamoja na mipango kazi ya kila mwaka?

Je, kuna mtu anajua ni Sekretarieti za Mikoa mingapi zilikuwa na mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita pamoja na mipango kazi ya kila mwaka?

Lakini pia, kuna mtu anajua ni Wizara ngapi zilikuwa na mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita pamoja na mipango kazi ya kila mwaka?

Huku kwetu “Simbawanga” hakuna kitu kama hicho. Lakini bado naona RC wetu amepewa ofisi tena.

Pia, yupo DED mmoja kutoka sukuma-land, kazi yake kuvaa suruali, kuchomekea shati, na kila jioni kusanitaizi koo kwa kutumia Balantine anazonunuliwa na wafanyabiashara.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, katika serikali ya awamu ya sita, yafaa “mvua za kwanza” ziwe ni kwa ajili ya kung'oa visiki na kupanda miche mipya yenye rutuba ili kijua kikianza kuwaka tuanze kupalilia shamba letu la kisiasa.

Kwenye Mikoa na katika Halmashauri sio sehemu ya kuchezea, kwa kuwa, huko ndiko serikali "inapokutana" na mwananchi uso kwa uso, siku kwa siku.

Huko ngazi ya Mikoa na Taifa, ambako naona kuna mawaziri na ma-RC ambao walishindwa hata kuandaa Strategic Plan za maeneo yao, na bado wamepewa nafasi tena, kuna shida ambayo huenda Rais ataitatua mbeleni.

Uhamisho wa watendaji dhaifu, katili na dhalimu sio sera nzuri. Kwa mfano, Mkuu wa Mkoa ambaye amesimamia utekaji wa raia, akaruhusu kambi ya Jeshi iliyo chini yake kuhifadhi na kusambaza kura feki wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, akashindwa kulinda uhai wa vyama vya ushirika, hafai kuteiliwa katika nafasi yoyote.

Uteuzi wa watu wa aina hii ni hatua ya kwanza katika safari ya kuhujumu pembetatu ya utawala, usala na maendeleo.

Lakini, pia kwenye ngazi ya Halmashauri, ambako kazi ya uteuzi inaelekea, kanuni hii ya kuyaacha magugu na ngano vikue pamoja, kwa hofu kwamba jaribio la kuyang'oa magugu linaweza kuiyumbisha miche ya ngano, haifai kabisa kwa sasa.

Kazi kwako Mhe. Rais kama mwamuzi: akili za kuambiwa changanya na zako;

Kazi kwako Makamu wa Rais, mleta hoja, na mshauri wa jumla wa Rais: Msaidie Rais kuzingatia kanuni za SWOT Analysis na TOWS analysis katika hatua anayopiga;

Kazi kwako DG wa TISS kama mshauri mkuu wa kiusalama wa Rais: Msaidie Rais kuujua ukweli wote juu ya watu anaofanya kazi nao, kwani wewe unazo taarifa nyingi zaidi kuliko yeye.
 
Usalama wa Taifa wamegeuka usalama wa kutetea chama tawala hawana hata moral authority kusaidia usalama wa uchumi....anzia ngazi familia hadi juu...wao wamekomalia tu kusaidia wana siasa na kuteka teka watu kuwalawiti ndio sifa yao sikuhizi
 
Kwa hili bandiko refu nimeamini kweli ww ni mwalimu. Huku mitandaoni watu wanataka habari zinazowasisimua, na sio kama hizi zilizoko kama masomo ya darasani. Hata hivyo hongera.
 
Hata kwenye vikao vya vyama vya siasa ikiwemo chama tawala wasiwe wajumbe katika sekretarieti za mikoa na wilaya zao.
 
Noted,

Lakini, kwa heshima, nakufahamisha kuwa, hao unaowaongelea sio sehemu ya hadhira niliyoikusudia katika bandiko hili.

Katika kuandika meseji yoyote huwa tunaongozwa na kanuni kuu tano:

  • Principle 01: Topic-Author-Purpose Triangle as determinant of content
  • Principle 02:Topic-Tone-Audience Triangle as determinant of content
  • Principle 03: General Approach
    • Specific-to-General;
    • General-to-Specific;
    • Specific-to-General-Specific;
  • Principle 04: General organizational structure: Intro-Body-Conclusion;
  • Principle 05: Body structure:
    • major premise-minor premise-conclusion (Aristotelian Model);
    • Point-counter point;
    • Geographical/Spatial(North, South, East, West)
    • Temporal/Chronological (Yesterday, Today, Tomorrow)
    • claim-ground-warrant-backing-objection-rebuttal-qualifier (Toulmin Model);
    • Question-antithesis-thesis-antithesis refutation (Thomistic Model)
    • Observation-Puzzle-Hypothesis-Evidence Collection and testing-Theorizing-Action Recommendation or OPHETA (Scientific Model)
Na kila mwalimu na mwanafunzi wa "Communication Skills" anazifahamu kanuni hizi.

Ni kwa kutumia kanuni hizi ndio tunaamua urefu wa andiko.

Nimezizingatia.

Mama Amon,

Karibu "Simbawanga"

Nimecheka kwa nguvu, thank you anyway.
 
Basi Sumbawanga kuna tatizo kubwa sn, sijaona jambo la maana hapo
Hata hii pointi hujaiona?

Ukisoma “Mikakati ya Usalama wa Kitaifa” kwa ajili ya nchi mbalimbali utaona kwamba, mikakati hiyo inakubaliana na ukweli huu ulitamkwa kwa mara ya kwanza na UNDP.

Mikakati ya Usalama wa Kitaifa kwa ajili ya mataifa 204 duniani inapatikana kwenye anwani ifuatayo mtandaoni: Series

Lakini, Tanzania na nchi nyingine chache hazimo. Bado wanaficha “Mikakati ya Usalama wa Kitaifa” kwa sababu ambazo, kwa maoni yangu, hazina uzito.

Kwa hakika, jambo hili linawanyima wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Mawaziri, na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali, kuwa na fokasi moja ya kiusalama.
 
View attachment 1790866
Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango

Kutokea hapa “S/M Simbawanga,” nawasalimu watu wa huko Dar es Salaam kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nikiwa natarajia kuwa kazi inaendelea! Huku “Simbawanga” tuko wazima.

Leo, nimeona kwenye TV Rais Samia akiapisha wakuu wapya wa mikoa na viongozi wengine aliowateua juzi. Mara baada ya kula viapo, wakubwa kadhaa walipata fursa ya kutoa nasaha kwa wateule hawa.

Nasaha za Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango, zimenigusa sana. Nilikuwa hapa “S/M Simbawanga” nikiwa nasahihisha madaftari ya wanafunzi, lakini ikanibidi nisitishe kidogo ili kumsikiliza vema.

Dk. Phillip Mpango amesema kwamba, mbali na jukumu la wakuu wa mikoa la kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao, kuna jukumu jingine. Kwamba, wakuu wa mikoa pia wanalo jukumu la kusimamia usalama wa kiuchumi katika maeneo yao.

Anachosema Makamu wa Rais hapa, ni kwamba, ajenda ya usalama wa mikoa, na hivyo ajenda ya usalama wa Taifa zima, ni zaidi ya kile ambacho tumezoea kukisikia kikitamkwa na baadhi ya watu wenye mtazamo wa kimapokeo juu ya usalama wa nchi.

Hapo zamani, kabla ya Taarifa ya Maendeleo ya Watu iliyotolewa na UNDP mwaka 1994, kutoa fasili pana ya usalama wa nchi, tulizoea kuambiwa kwamba, kazi ya kulinda usalama wa nchi inafanyika kwa kuimarisha usalama dhidi ya vitisho vya kijeshi.

Huu ni mtazamo kwamba, maana ya usalama wa nchi ni kuwa huru dhidi ya vitisho vya kijeshi kwa sababu ya kuwa na wanajeshi wenye ufundi wa kutumia bunduki, risasi, vifaru, mizinga na makombora ya kuwadungua maadui wa ndani na nje.

Lakini, kama alivyosema Makamu wa Rais, kwa kuzingatia mazingira ya sasa, ajenda ya usalama wa nchi imebadilika sana, kiasi kwamba, usalama wa kijeshi ni sehemu ndogo sana ya “Mikakati ya Usalama wa Kitaifa” (National Security Strategies).

Taarifa ya Maendeleo ya Watu iliyotolewa na UNDP mwaka 1994 ilisisitiza kwamba, kwa kuwa Taifa ni jumla ya watu, nchi na serikali yao, basi, “usalama wa Taifa” unapaswa kugusa maeneo saba ya usalama wa watu, yafuatayo:

  • Usalama wa kiuchumi, kwa maana ya haki ya kila raia kuwa huru dhidi ya umaskini wa kipato, ama kutokana na kujiajiri, kuajiriwa au program za usalama wa jamii;
  • Usalama wa lishe, kwa maana ya haki ya kila raia kupata mlo kamili mara tatu kwa siku;
  • Usalama wa kiafya, kwa maana ya haki ya kila kupata huruma za kiafya bila vikwazo vya kifedha, kijiografia au vinginevyo;
  • Usalama wa kiikolojia, kwa maana ya haki ya kila raia kuishi katika mazingira yaliyo huru dhidi ya wanyama waharibifu, wadudu wakali, mionzi ya jua, mafuriko, mmomonyoko wa ardhi, ukame, hali ya jangwa, maji yenye chumvi, uchafuzi wa anga kwa njia ya moshi, na mambo kama hayo.
  • Usalama wa mtu mmoja mmoja katika ngazi ya kisaikilojia na kimwili, kwa maana ya haki ya kila raia kuwa huru dhidi ya uteswaji, utekwaji, vitisho, vita vya kikabila, wizi, ukatili wa kiuchumi, ukatili wa kijinsia, na uhalifu.
  • Usalama wa jumuiya mbalimbali, kwa maana ya haki ya kila raia kujiunga na jumuiya zitakazompatia nembo ya utambulisho wa kiuchumi, kisiasa, kielimu, kitabibu, kitaaluma, kimbari, kikabila, kidini, kirika, kijinsia, au vinginevyo.
  • Usalama wa kisiasa, kwa maana ya haki ya kila raia kuishi kama mtu aliye hudu dhidi ya ukatili unaotekelezwa kupitia mikono ya chombo cha dola, ambapo maneno “chombo cha dola” yanamaanisha mtu yeyote au kikundi chochote kinachotekeleza majukumu yake kwa niaba ya Jamhuri.
Ukisoma “Mikakati ya Usalama wa Kitaifa” kwa ajili ya nchi mbalimbali utaona kwamba, mikakati hiyo inakubaliana na ukweli huu ulitamkwa kwa mara ya kwanza na UNDP.

Mikakati ya Usalama wa Kitaifa kwa ajili ya mataifa 204 duniani inapatikana kwenye anwani ifuatayo mtandaoni:
Mikakati ya Usalama wa Kitaifa Duniani.

Lakini, katika orodha hii hakuna “Mkakati wa Usalama wa Kitaifa” wa Tanzania. Na hauonekani mahali popote kwenye tovuti za serikali.

Maana yake ni kwamba, ama Tanzania hatuna “Mkakati wa Usalama wa Kitaifa” au upo lakini unafichwa fichwa, lakini kwa sababu ambazo, kwa maoni yangu, hazina uzito.

Vyovyote iwavyo, jambo hili ni dosari kubwa inayowanyima wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Mawaziri, na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali, kuwa na fokasi moja ya kiusalama.

Hapa naongelea ajenda ya usalama wa nchi ndani ya
pembetatu ya utawala, usalama na maendeleo. Haya matatu hayatenganishiki.

Kwa kweli, matarajio yangu ni kwamba, “Mkakati wa Usalama wa Kitaifa” lazima uwe na kifungu kinachosema kuwa, kila Halmashauri, kila Mkoa, kila Wizara, na kila Idara ya serikali, inapaswa kuwa na Mipango Mkakati ya Muda Mfupi na Mrefu, ili kwa njia hiyo, Taifa liweze kujipima katika kipengele cha kuweka na kusimamia mipango yake ya maendeleo.

Kama hivi ndivyo, kuna mtu anajua ni Halmashauri ngapi zilikuwa na mpango mkakati katika miaka mitano iliyopita?

Je, kuna mtu anajua ni Sekretarieti za Mikoa mingapi zilikuwa na mpango mkakati katika miaka mitano iliyopita?

Lakinio pia, kuna mtu anajua ni Wizara ngapi zilikuwa na mpango mkakati katika miaka mitano iliyopita?

Huku kwetu “Simbawanga” hakuna kitu kama hicho. Lakini bado naona RC wetu amepewa ofisi tena.

Pia, yupo DED mmoja kutoka sukuma-land, kazi yake kuvaa suruali, kuchomekea shati, kung’arisha viatu, kuvivaa, na kila jioni kusanitaizi koo kwa kutumia Balantine anazonunuliwa na wafanyabiashara.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, katika serikali ya awamu ya sita, yafaa “mvua za kwanza” ziwe ni kwa ajili ya kung'oa visiki na kupanda miche mipya yenye rutuba ili kijua kikianza kuwaka tuanze kupalilia shamba letu la kisiasa.

Kwenye Mikoa na katika Halmashauri sio sehemu ya kuchezea, kwa kuwa, huko ndiko serikali "inapokutana" na mwananchi uso kwa uso, siku kwa siku.

Huko ngazi ya Mikoa na Taifa, ambako naona kuna mawaziri na ma-RC ambao walishindwa hata kuandaa Strategic Plan za maeneo yao, na bado wamepewa nafasi tena, kuna shida ambayo huenda Rais ataitatua mbeleni. Uhamisho wa watendaji dhaifu sio sera nzuri.

Lakini, kwenye ngazi ya Halmashauri, ambako kazi ya uteuzi inaelekea, kanuni hii ya kuyaacha magugu na ngano vikue pamoja, kwa hofu kwamba jaribio la kuyang'oa magugu linaweza kuiyumbisha miche ya ngano, haifai kabisa kwa sasa.

Kazi kwako Mhe. Rais kama mwamuzi;

Kazi kwako Makamu wa Rais, mleta hoja, na mshauri wa jumla wa Rais;

Kazi kwako DG wa TISS kama mshauri mkuu wa kiusalama wa Rais;
Mwl unajielewa sana. Unafundisha shule gani nilete mwanagu hapo.
 
Back
Top Bottom