Dkt. Mpango mbona hutoi pesa za miradi ya maendeleo wakati Rais anasema serikali ina pesa nyingi sana haijapata kutokea?

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Kumekuwa na malumbano Bungeni kiasi cha mmoja wa Naibu waziri kulia mbele ya kamati moja kushindwa kutekeleza miradi huku akidai kuwa pesa kutoka wizara ya fedha haijatolewa.

Spika amelitolea maelezo na kumlalamikia waziri wa fedha kwa kushindwa kutoa fedha kwa wakati na mara nyingine kutozitoa kabisa na kausababisha miradi mingi kutotekelezwa

Wizara ta fedha imekalia fedha za korosho,fedha za REA na kusababisha hali mbaya katika hayo maeneo.

Na mbaya zaidi katika Wizara ya fedha iko kimya kabisa kuhusu kwanini inashindwa kutoa fedha
 
Nahisi kuna tatizo wizara ya fedha haitaki kuweka wazi. Either ni pesa hawana, au wamepeleka pesa kwingine
 
Hivi spika bado hajaelewa mpaka leo huyo waziri mpango ni sawa na galasa la karata? Madaraka yake ni waziri wa fedha lakini kiuhalisia waziri wa fedha ni Jiwe mwenyewe haoni kila fedha inatolewa kwa amri toka Ikulu
 
Unafikiri kila analosema Rais huyu ni kweli??

Kwamba anavosema serikali ina hela nyingi ni kweli??

Serikali haina HELA..Nchi IMEFILISIKA Ndugu.

Jiongeze kichwani.
 
Rais ametamka hadharani kuwa serikali ina pesa nyingi sana haijapata kutokea......tuna amini ni kweli.
 
Hivi spika bado hajaelewa mpaka leo huyo waziri mpango ni sawa na galasa la karata? Madaraka yake ni waziri wa fedha lakini kiuhalisia waziri wa fedha ni Jiwe mwenyewe haoni kila fedha inatolewa kwa amri toka Ikulu
Jiwe ni nani?
 
Fedha za kujenga reli ya kisasa zipo....

Fedha za kununua ndege zipo....

Hivyo vingine si vipaumbele vya serikali kwa sasa....
 
Kumekuwa na malumbano Bungeni kiasi cha mmoja wa Naibu waziri kulia mbele ya kamati moja kushindwa kutekeleza miradi huku akidai kuwa pesa kutoka wizara ya fedha haijatolewa.

Spika amelitolea maelezo na kumlalamikia waziri wa fedha kwa kushindwa kutoa fedha kwa wakati na mara nyingine kutozitoa kabisa na kausababisha miradi mingi kutotekelezwa

Wizara ta fedha imekalia fedha za korosho,fedha za REA na kusababisha hali mbaya katika hayo maeneo.

Na mbaya zaidi katika Wizara ya fedha iko kimya kabisa kuhusu kwanini inashindwa kutoa fedha
Mtamlaumu tu kwakuwa hawezi sema ukweli,kinachoharibu bajeti hata ya hizo ndogo zilizopo ni bajeti isiyo rasmi inayotengewa pesa kwa matamko!!natoa bilioni kumi kajenge hiki!!!wapi ulishaona kitu cha namna hiyo duniani??ndio maana kuna kipindi cha bajeti mnapitisha makadilio ya mapato na matumizi !!hiyo miradi inayo ibuka kila leo wakati haikuwa kwenye bajeti una dhani hizo pesa zinatoka wapi???
 
Spika amelitolea maelezo na kumlalamikia waziri wa fedha kwa kushindwa kutoa fedha kwa wakati na mara nyingine kutozitoa kabisa na kausababisha miradi mingi kutotekelezwa

Wizara ta fedha imekalia fedha za korosho,fedha za REA na kusababisha hali mbaya katika hayo maeneo.

Na mbaya zaidi katika Wizara ya fedha iko kimya kabisa kuhusu kwanini inashindwa kutoa fedha
Ndugai na Mpango wote wanajua tatizo liko wapi. Kilichobaki ni kutafuta njia ya kufikisha ujumbe. Hata waziri wa kilimo pia anajua alichofanya ni kuja na "agenda focussing event". Kwa kulia kwake sasa watu wanaulizana kwa sauti. Tujiulize yale mamilioni yanayotumika nje ya bajeti yanatoka wapi? Haya mambo yananikumbusha stori za Mzee Karume tulizokua tunazisikia kwamba baba yule account ya SMZ ilikuwa kama ya kwake na alikuwa anaitumia apendavyo (sijasema vibaya) lakini enzi hizo Zanzibar ilikuwa inakwenda kwa presidential decrees (hakuwa na bunge bali baraza).
 
Nahisi kuna tatizo wizara ya fedha haitaki kuweka wazi. Either ni pesa hawana, au wamepeleka pesa kwingine
Pesa zote kachukua Maliyamungu Bashite kwa kazi ya kudidimiza chadema na kudhoofisha upinzani hawana pesa hao ndiyo maana waziri wa fedha anasuasua
 
Spika wa bunge Job Ndugai,leo kwa masikitiko ameweka bayana kuwa wizara ya fedha imekuwa haiwapi baadhi ya mawaziri fedha za bajeti ambazo zinaidhinishwa na bunge hali ambayo imesababisha baadhi ya mawaziri kuangua kilio mbele ya kamati za bunge wanapotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya kushindwa kutimizwa kwa baadhi ya mambo yaliyoidhinishwa na Bunge.

Yapo mambo unajiuliza
1.Kwa nini baadhi ya wizara tunaambiwa zimepewa asilimia sifuri ya pesa walizoodhinishiwa na bunge?na tukumbuke mwaka jana bajeti hii tuliambiwa ni ya kihistoria na haijawahi kutokea,hiki ndicho kilichokuwa tunaambiwa?maana tangu Mwalimu Nyerere sidhani kama kuna wizara iliwahi pewa asilimia sifuri ya bajeti ya maendeleo.

2.Baadhi ya mawaziri kwa mujibu wa Spika,sasa wanalazimika kuwapigia magoti wizara ya fedha ili wapewe fedha,sasa kwa nini wizara ya fedha haiwapi pesa baadhi ya mawaziri?ndiyo kusema,hakuna pesa,serikali haikubaliani na vipaumbele vya wabunge?ama serikali inajua bunge halina ubavu wa kuwafanya chochote?

3.Nape analalama kuwa kile kikao ambacho Spika alikiitisha kati ya NAPE,kamati ya bajeti na wizara ya fedha wakae na kusaka muafaka kuhusu suala la Korosho,eti wizara ya fedha hawakutokea kwenye vikao ambavyo aliviitisha spika,mpaka spika anasema ataongea na waziri mkuu,ikishindikana atawaachia wabunge waamue,sasa unajuliza waziri wa fedha kugoma kwenda kwenye kikao(Kwa mujibu wa Nape,)ni kiburi dhidi ya Spika na bunge,kuwa hawawezi kufanya jambo lolote kwao?

Bahati mbaya sana,bunge halipo live wakati wa mijadala,kuna mambo mengi sana watanzania wanashindwa kuyajua,nimesikia hata shirika la umeme Tanesco lina madeni sana,kwa mujibu wa Esther Bulaya akinukuu ripoti ya Kamati.

Miongoni mwa misingi ya utawala ni uwazi,utawala wa sheria,matumizi sahihi na stahiki ya Rasilimali za nchi.
 
Kumekuwa na malumbano Bungeni kiasi cha mmoja wa Naibu waziri kulia mbele ya kamati moja kushindwa kutekeleza miradi huku akidai kuwa pesa kutoka wizara ya fedha haijatolewa.

Spika amelitolea maelezo na kumlalamikia waziri wa fedha kwa kushindwa kutoa fedha kwa wakati na mara nyingine kutozitoa kabisa na kausababisha miradi mingi kutotekelezwa

Wizara ta fedha imekalia fedha za korosho,fedha za REA na kusababisha hali mbaya katika hayo maeneo.

Na mbaya zaidi katika Wizara ya fedha iko kimya kabisa kuhusu kwanini inashindwa kutoa fedha
Pesa zote wamekula kikundi cha Maliyamungu Bashite watu wasiojulikana na wale wanaojulikana sasa akina Le mutuz, Lipumba, Cyprian msiba, Jerry muro , Heri Kisanduku makapero na Boss wao Maliyamungu idd Amin Bashite
 
Back
Top Bottom