Dkt. Mpango: Kodi si tatizo Bandarini

kabisa ukweli!!!!!!!! truth shall set us freeeeeeee
 
mchambe huyo sijui ni kula kulala hahah !!!!!!!kazi yake kukariri watu hawalipi kodi utazani kamezeshwa sumu na sangoma mana kutokulipa kodi ndo wimbo wa Taifa.
 
Si kila wakati watu hubisha kufanya mambo bila ya sababu!
Mpango angewaita wafanya biashara na kuzungumza nao! Labda angejifunza mengi toka kwao pia!
Hizi mentality za kuona wafanyabiashara ni evils ni mbaya sana!
Nililisema hili kitambo.

Serikali hiinitaangusha uchumi.

Imeanza kwa kuona wafanyabiashara wote wezi, tuwakamue damu yote wafilie mbali. Halafu uchumi ukianguka ndiyo tutakuwa tumeondoa tatizo la wafanyabiashara wezi hawa.

Ni kamandaktari anaona kuna mgonjwa ana ugonjwa mbaya sana, anasema " huyu mgonjwa ana ugonjwa mbaya sana. Dawa yake tumpe sumu. Tukimpa sumu akifa tutakuwa tumeua vimelea vyote vya ugonjwa.

Ridiculous.
 
Mimi nilisema hili. Nilisema hili la China ni changa la macho tu.

Nikisoma article ya Wall Street Journal nafikiri ni early July kama si late June kuhusu uchumibwa China kuanguka kusababisha slowdown katika bandari kubwa za dinia mpaka Europe.

Nikaona data za nchi nyingi pale. Lakini hawakitaja Africa.

Nikamfuata mdau wangu anayeijua bandari vizuri. Katika watu watano wanaoijua bandari ya Dar na historia yake vizuri bongo huyu hakosi.


Nikamuuliza. Unaona article ya Wall Street Journal hiyo? Mbona naona China kudodoka uchumi wametoa data za nchi kibao mpaka bandari kama Rottterdam na Los Angeles lakini bandari za Afrika hawajazitaja? Akaniambia hizi bandari zetu za Afrika mizigo yake hai mive scale ki hivyo kwenye world market, hatuna impact kubwa hivyo kwa hiyo gazeti kama Wall Street Journal linapoandika for the big dogs wanakuwa hawana interest na data za Africa ambazo laregly ni negligible kutokana na volume kuwa ndogo. Nikaelewa kwamba nilikuwa nime suspect kitu kama hicho, lakini kusikia kutoka kwa huyu top dog wangu kukawa kume confirm.

Sasa leo ukiniambia China ime affect bandaribya Dar ni changa la macho tu. Kwa sababu hatufanyi nao biashara kubwa kiasi hicho anyway katika world stage.

Mtu akitoa sababu ya China kwa kupungua mizigo bandarini ni sawa na kusema mortgage crisis ya US imeshusha bei ya viazi vya kinyasini. Ni kisingizio tu.
 
"Hakuna mfanyabiashara hata mmoja aliyechangia senti kwenye kampeini uchaguzi uliopita"!

Magufuli pale alichemsha sana.

Rais anakuwa anti business mpaka anawatukana wafanyabiashara wote kama wezi kwa lugha hii.

Kwa minajili hii uchumi lazima uyumbe.
 
Ni kweli tupu, tulishaonywa na IMF ya kwamba tusiitegemee sana China kwa ufadhiri wa Miradi ya Maendeleo, sababu China ikiyumba na sisi tutaanguka. Lakini mambo haya ni ya kujifunza kwetu, maana kama hakuna kinachoingia bandarini basi tufungue viwanda kuziba nakisi ya kilichokosekana na pia tujaribu kusafirisha nje. Watanzania huu ndio wakati wetu.
 
Kuwaongoza Watanzania ni rahisi sana ...Uchumi unaendeshwa kisiasa ?..
 
Mnataka kutuaminisha kuwa bandali ya mombasa iliyishehen makontena inatokana na ukwepaji kodi? Vip bandali ya S.A je?
 
Magufuli pale alichemsha sana.

Rais anakuwa anti business mpaka anawatukana wafanyabiashara wote kama wezi kwa lugha hii.

Kwa minajili hii uchumi lazima uyumbe.

Labda ameshindwa kung'amua utofauti wa majukumu ya Mkuu wa Nchi na Baba wa familia..
 
halifichiki pembe la ng'ombe...

wakati Wa tozo ya vat walisema haitamuathiri mtumiaji..Leo tunayaona...
 
Huyo kasuku hawezi kuongea tofauti na bosi wake.
 
Maisha magumu awamu ya 5 nani atatuhurumia wananchi mbona wamemuachia Rais peke
 
yes, walipe kodi sio kubaki kuiombea nchi njaa ili wao washibe. hawa wakwepa kodi sio watu wema.
 
Network ya kutolipa kodi ilikuwa kubwa sana.
Utitiri wa bandari kavu, kampuni za clearing and Forwarding na wafanyakazi bandarini. Kila nanayefanya bandarini ni tajiri mpaka makuli wanajenga nyumba zaidi ya 3 wakati serikali haipati mapato.
Ni kweli kodi sio tatizo.
Tatizo mtandao wa wezi wanatafuta bandari isiyosimamia mambo yake sawasawa.
 
Mm kinachiniuma ni makato kwenye miamala ya sim,, yani kama tigo pesa una elfu 55, unatoa 52,500 yani makato 2,500!! So sad tunakamuliwa sana kwa kweli
 
Propaganda za kitoto SEMENI UKWELI NCHI INAYUMBA SANA


NCHI HAIYUMBI, WAKATI WA KIKWETE NCHI ILIKUWA INAONGOZWA KAMA JAHAZI HALINA CAPTAIN, NA NCHI ILIKUWA IKIELEKEA KUZAMA, RAIS MAGUFULI AMEIOKOA. MAJENGO MAREFU, NA NYUMBA NZURI CHACHE ZILIZOKUWA ZIKIJENGEKA KWA KASI KUBWA, WENGI WAO WALIKUWA WAKIJENGA NA PESA ZA WALIPA KODI WANYONGE. PESA ZAO BADALA YA KUJENGA MABALABALA, KUNUNUA VIFAA VYA HOSPITAL NA KUNUNUA MADAWA HOSPITALINI ZILIKUWA ZIKIIBIWA KWEIPU NA WACHACHE. SERIKALI INANUNUA PEN YA SHILLING 100 KWA SHILLING 30000 NA NCHI HAIKUYUMBA. WATANZANIA WENGI WAVUMILIVU WALIKUWA WAKIUMIA KIMYA, WAKUBWA WANAPIGA SUTI, WAKIUGUA AMERIKA AMA APPOLLO HOSPITAL INDIA, WA LALA HOI WANAKUFA PEKE YAO. MUHIMIMBILI WAGONJWA WALIKUWA WAKILALA KWENYE VARANDA, RAIS ALIKUWA HAONI, AKIUGUA ANAZICHINJA ZA MAREKANI KWENYE HOSPITAL YA GEORGE BUSH. UNAONA DUNIA HIYO. PESA ZA WALIPA KODI MASIKINI NDIZO ZILIKKUWA ZIKITUMIKA KUMANTAIN MAHOTELI KWA MIKUTANO ISIYOWANUFAISHA, PESA ZA WALIPA KODI ZILIKUWA ZIKITUMIKA KUJENGA MAJUMBA YA FAHARI MBEZI BEACH NA MAHALI PENGI, NENDA MBEZI BEACH, MAJUMBA YAMESIMAMA, VIWANJA BEI ZIMETELEMUKA, KWA SABABU SHAMBA LA BIBI NIMETIWA KUFULI, WEZI WOTE WANAILAUMU SERIKALI YA MAGUFULI BADALA YA KUFANYA KAZI. MUNGU NI MUKUBWA, KASIKIA VILIO VYA WATANZANIA, SIYO KWA MAWE AMA KWA FUJO KATUTUPIA MUKOMBOZI. AMESHIKA TU MADARAKA KAGUNDUA CONTAINER ZA WAZURUMAJI ZINAPITA BILA KODI, WAGONJWA WANALALA CHINI, MAFUTA BANDARINI YANAPITA BILA KUPIMWA, WATOTO WETU HAWANA VITABU WALA VITI MASHULENI, MACHINE ZA HOSPITAL ZA WALALA HOI HAKUNA HATA MASHINE MOJA INAFANYA KAZI KUSEMA NCHI INAYUMBA KWA SASA LAZIMA ULIKUWA MUMOJAWAPO WA WANYONYAJI. MUNGU AKUSAMEHE ZAMBI ZAKO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…