Dkt. Mashinji afika Kisutu kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wa CHADEMA. Mdee agoma kumpa mkono, Wakili ajitoa kumtetea

Kuna mtu alikataa mkono wa Rais wa nchi Fulani na maisha yakaendelea sembuse mkono wa mwanaharakati?

Hakika Masinji alipokuwepo awali sipo alipotakiwa kuwepo ,kazungukwa na watu wasiopenda mafanikio ya wengine. Kwa umri ,elimu na uzoefu wa Mashinji ,kuachwa bila jukumu lolote ni aibu na fedheha huku wanaharakati wakiula
 
Behaviourist,
Kukataa kumpa Mkono ndiyo Ustaarabu na Ukomavu wa Kisiasa wa Mtu makini kama Mbunge Halima Mdee? Siasa si Uadui na hiki Kitendo alichofanya Mbunge Halima Mdee ni cha Kipuuzi kuliko maelezo na nasikitika huku nikishangaa pia kuona wapo Watu wanampongeza.

Tusisahau kuna Maisha nje ya Siasa na hizi Demokrasia na labda Mbunge Mdee nae atuambie na atuhakikishie je, na Yeye akihama CHADEMA Watu aliokuwa nao CHADEMA wamnunie au wamsusie?

Kama Mbunge na Msomi makini kwa Kitendo hiki cha Kishamba na Kijinga amejishushia mno Hadhi yake. Kwahiyo Mbunge Mdee ndiyo ana Machungu zaidi na CHADEMA kuliko hao Wabunge wenzake wote waliompa mkono wa Salamu Dkt. Mashinji na hata wana CHADEMA waliokuwepo hapo Mahakamani hii leo? Waafrika tuna taabu sana hata kama tumebahatika kwenda Shule kutoa Upumbavu wetu.
 
Back
Top Bottom