Mbowe na viongozi wenzake wa chadema wakutwa na kesi ya kujibu kwenye mashtaka ya uchochezi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu viongozi tisa wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mbowe na viongozi wengine wanane wa chama hicho wakiwemo wabunge sita wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 112/2018 yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao.

Washtakiwa wengine ni mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Naibu Katibu Mkuu Taifa-Zanzibar, Salum Mwalimu; Mbunge wa Kibamba, John Mnyika; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya na katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji.

Jana katika kesi hiyo Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kipolisi Mbagala, Bernard Nyambari alitoa ushahidi na kuieleza mahakama hiyo kuwa taarifa za kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline zinaonyesha alikufa akiwa hospitali ya Mwananyamala akipatiwa matibabu.

Alisema Akwilina alipata jeraha kichwani lililosababishwa na risasi, lakini hafahamu aliyempiga risasi mwanafunzi huyo.
 
Hii kesi naìona ikienda mpaka 2021 baada ya uchaguzi.
 
Hahaha uchaguzi umekaribia hatukawii kusikia wamebadirishiwa mashitaka na kuwa wameua bila kukusudia, an kushikiliwa mahabusu bila dhamana na kesi yao itatajwa ila watuhumiwa hawataruhusiwa kujibu chochote mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na watuhumiwa watarudishwa rumande baada ya kesi kuahirishwa hadi hapo itakapopangiwa tarehe nyingine ya kusikilizwa.
They are very predictable.
We have laws but no justice.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu viongozi tisa wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mbowe na viongozi wengine wanane wa chama hicho wakiwemo wabunge sita wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 112/2018 yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao.

Washtakiwa wengine ni mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Naibu Katibu Mkuu Taifa-Zanzibar, Salum Mwalimu; Mbunge wa Kibamba, John Mnyika; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya na katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji.

Jana katika kesi hiyo Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kipolisi Mbagala, Bernard Nyambari alitoa ushahidi na kuieleza mahakama hiyo kuwa taarifa za kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline zinaonyesha alikufa akiwa hospitali ya Mwananyamala akipatiwa matibabu.

Alisema Akwilina alipata jeraha kichwani lililosababishwa na risasi, lakini hafahamu aliyempiga risasi mwanafunzi huyo.

Wawape wachunguzi wa kimataifa watajua nani aliyepiga risasi,hata askari waliowatawanya watu wanajua mwenzao aliyepiga risasi.Hata wakichukua maganda ya risasi si yana serial namba wazitumie kumpata aliyepiga risasi.
 
CCM inataka kuwafunga mahasimu wao wa kisiasa...hii yote ni maandalizi ya kuelekea mfumo wa chama kimoja.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu viongozi tisa wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mbowe na viongozi wengine wanane wa chama hicho wakiwemo wabunge sita wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 112/2018 yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao.

Washtakiwa wengine ni mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Naibu Katibu Mkuu Taifa-Zanzibar, Salum Mwalimu; Mbunge wa Kibamba, John Mnyika; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya na katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji.

Jana katika kesi hiyo Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kipolisi Mbagala, Bernard Nyambari alitoa ushahidi na kuieleza mahakama hiyo kuwa taarifa za kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline zinaonyesha alikufa akiwa hospitali ya Mwananyamala akipatiwa matibabu.

Alisema Akwilina alipata jeraha kichwani lililosababishwa na risasi, lakini hafahamu aliyempiga risasi mwanafunzi huyo.
Unaweza uliza maswali hata 1,000 ukayapa kila aina ya sifa, sijui maswali mazito, n.k Hayatasaidia, kinachoangaliwa ni mantic ya maswali hayo.
 
Back
Top Bottom