TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,868
- 5,753
Kambi ya Waziri Mkuu wa Zamani , Edward Lowassa inayoaminika kuwa ni ya siku nyingi zaidi katika kinyang'anyiro cha kusaka uteuzi wa kugombea urais kupitia CCM , hatimaye imeanza kusambaratika baada ya mmoja kati ya vigogo wake wa kutegemewa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa kuanza kuisaliti kimya kimya.
Chanzo hicho cha habaari cha kuaminika kutoka kambi hiyo kigogo huyo ambaye alichangia kwa sehemu kubwa kujenga ngome imara ya LOWASSA katika Kanda ya Ziwa, hivi sasa amegeuka kimyakimya huku ikielezwa kuwa anayeibomoa ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli.
Inasemekana kigogo huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM amekwenda kumshawishi Magufuli kwamba achukue fomu ya kugombea nafasi hiyo ya urais.
Habari zaidi zinasema kuwa Wajumbe wengi hasa wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM hawana imani tena na LOWASSA kutokana na sababu mbalimbali .
Wajumbe hao wamesema sasa hawataangalia nani ana nguvu kiasi gani ila watazingatia zaidi matakwa ya chama kwamba kinamtaka nani agombee urais.
Aidha wajumbe hao wamelaani tabia ya badhi ya Makada wa CCM kuwasingizia wananchi wa maeneo yao kuwa wamewatuma kwenda kwa Lowassa ili kumshawishi atangaze nia ya kugombea urais.
Wajumbe hao wamesema watu hao ni maswahiba wa LOWASSA wa siku nyingi na wanafanya hivyo kwa sababu hiyo na siyo kwamba wametumwa na wananchi wao.
Baadhi ya Makada hao wa CCM na ambao ni maswahiba wa siku nyingi wa LOWASSA ambao wanakwenda kwa LOWASSA kwa madai kuwa wametumwa na Wananchi ni pamoja na Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya BUSEGA, Dk. RAFAEL CHEGENI na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Serengeti na mjumbe wa NEC.
Chanzo: Gazeti la CHANGAMOTO