Uchaguzi 2020 Dkt. Lwaitama atabiri mshindi Uchaguzi Mkuu 2020

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,289
24,166
24 Agosti 2020

Katika mahojiano maalum Mwanzuoni wa masuala ya binadamu, mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha UDSM mwalimu Dr. Azavery Lwaitama amesema anaufuatilia michakato uchaguzi wa Oktoba 2020 kwa ukaribu

Tukio la uchaguzi wa 2020 ni kuthibitisha wananchi ndiyo watawala halisi wa nchi hii Tanzania na siyo Bunge, wala taasisi ya uRais, udiwani. Hilo ni muhimu waTanzania wapiga kura kutambua ni watu-huru na wasisahau kuwa tukio la Oktoba watambue wasiuze uhuru wao kwa wagombea wanaopenda kutawala badala ya kuongoza.

Hivyo wapiga kura wawe makini kuchagua wagombea ambayo hawatajitwalia madaraka ya kuwaswaga wananchi kwa kigezo cha kuchaguliwa kwa kura.

Tukio la kupiga kura kisigeuzwe kuwa ni maridhiano ya kuuza uhuru na utu wao ili watawaliwe kwa miaka mitano bila uhuru au sauti ya kuwakosoa au kushirikishwa ktk maamuzi na wanasiasa watakaokuwa wameingia madarakani ktk serikali, bungeni au ktk mabaraza ya madiwani.

Tofauti za Mvuto wa wagombea katika uchaguzi wa Oktoba 2020 kutafuta wadhamini, hivyo wapiga kura Watanzania wanahisia gani kwa wagombea wanaotafuta udhamini na wale wa kimya kimya waliopitishwa na vyama wanavyovipenda na kuviamini vyama vyao.

Chama cha ANC cha Afrika ya Kusini kilipigwa marufuku na makaburu kwa muda mrefu lakini ANC walikuja kuibuka washindi huku Mandela mbali ya kuweko nje ya siasa kwa miaka 27 alichaguliwa kuwa Rais na pia ANC chama kilichopigwa marufuku ya siasa kilipata wabunge wengi. Uchaguzi huo wa kihistoria wa mwaka 1994 baada ya ubaguzi kuondolewa ulihusisha vyama 19 vya siasa nchi Afrika ya Kusini ANC, PAC, NP na :

19 political parties: African National Congress (ANC), National Party (NP), Inkatha Freedom Party (IFP), Pan Africanist Congress of Azania (PAC), Freedom Front (FF), Democratic Party (DP), African Christian Democratic Party (ACDP), Africa Muslim Party (AMP), African Moderates Congress (AMC), Dikwankwetla Party of South Africa (DPSA), Federal Party (FP), Minority Front (MF), Sport Organisation for Collective Contributions and Equal Rights (SOCCER), African Democratic Movement (ADM), Women’s Right Peace Party (WRPP), Ximoko Progressive Party (XPP), Keep It Straight & Simple Party (KISS), Worker’s List Party (WLP), and Luso-South Africa Party (LUSO). The South African general elections: 1994 | South African History Online

Historia katika Sayansi ya Siasa ( Political Science) inaonesha vyama vinavyofungiwa kufanya siasa vina uwezekano wa kuibuka washindi kushika dola kupitia uchaguzi huru na wa haki.

Chama kilichopo madarakani kina fursa kutumia walichofanya kwa wananchi kushinda uchaguzi.

Lakini katika siasa chochote kinaweza kutokea bila kujali chama kilikuwa madarakani au katika katazo la kufanya siasa kushinda.

Ngazi ya ki-urais katika kuwania nafasi ya urais hata wakijitokeza watu 100 historia huonesha ni watu wawili tu ndiyo watakuwa wanachuana vikali.

Na mpaka sasa inaonesha uchaguzi wa mwaka huu utakuwa ngumu na matokeo ya kustaajabisha sana anamalizi mwanazuoni huyu mahiri aliye mtu-huru katika uchambuzi wake wa eneo lake la taalumu ya uchambuzi wa tabia za binadamu na leo ameangazia eneo la siasa na chaguzi.

SOURCE: MwanaHalisi TV
 
Ujumbe murua kabisa huu unaomgusa Lissu kwa asilimia 100.

Mfano wa kihistoria wa Mandela kutoka jela na kupata kura za huruma aliotumia kumuelezea Lissu,ni ukweli mchungu japo Lissu bado ana mtaji wa ziada wa kuwa mkosaji mkubwa wa Magufuli na serikali yake kabla hata ya kushambuliwa kwa risasi

Kuhusu hiyo historia,binafsi ndio maana niliwa sema historia hapa JF kuwa historia ni kioo katika Maisha tena kioo kisichovunjika bali huwa ni kioo kinachong'ara muda wote.

Kuhusu swala la kuungana,wapinzani mlifanyie kazi hasa katika nafasi za ubunge na udiwani kama alivyoshauri Dr.Lwaitama.
 
Ukiwasikiliza CHADEMA wa Jamii Forums waweza kudhani Tundu Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii. Bora hata CHADEMA wa mitaani wanakubali ukweli. Ukitaka kuamini hata 2015 pamoja na Lowassa kuongea dk 3 kwenye kampeni mliaminishwa na Mbowe na mkadeki barabara. Ngoja niwape hints basi...

Kuna wapiga kura milioni 29 mliwahi kuwahesabu?, Kuna vituo zaidi ya 80000 vya kupigia kura nchi nzima mliwahi kuvihesabu?, Let say vipo kweli ili msiibiwe mnahitaji wasimamizi wenu CDM angalau wawili wawili kila kituo na mkisema muwalipe elfu 20 (20000)kila mmoja, kwa vituo vyote mnahitaji (20000x2x80000)zaidi ya bil. 3.2 je mnazo?

Kama mnazo zinawatosha wasimamizi wenu wasirubuniwe na pesa zaidi na CCM?,kwa tume hii nikiona mtu mzima tena mwanaume na p.umbu zake anaamini Lissu anaweza kuwa Raisi wa nchi hii namuona MPUMBAVU sana.

Badala ya kukomalia vitu vya maana mnakomalia UPUMBAVU wa mara Amsterdam mara Lwaitama. CHADEMA wote na viongozi hamna akili.
 
Ukiwasikiliza CHADEMA wa Jamii Forums waweza kudhani Tundu Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii. Bora hata CHADEMA wa mitaani wanakubali ukweli. Ukitaka kuamini hata 2015 pamoja na Lowassa kuongea dk 3 kwenye kampeni mliaminishwa na Mbowe na mkadeki barabara. Ngoja niwape hints basi..
Naona umeandika ukiwa na stress, chuki na jazba, katika hivo vitatu ukipunguza kila kimoja kiwe wastani utaandika
 
Umecopy kwa nani hii post? Maana naona kila sehemu unapita unajambajamba.

Gharama za uchaguzi kwa vyama vyote kwenye issue za mawakala huwa zinabebwa na kata au jimbo pamoja na mgombea, hii ni kwa vyama vyote.

Unatujazia mashuzi tu hapa.
Hizo kata zinatoa wapi hizo fedha mmeshawahi kuziwezesha? Mgombea gani anaeweza kujigharamia? Lissu?
 
Ukiwasikiliza CHADEMA wa Jamii Forums waweza kudhani Tundu Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii. Bora hata CHADEMA wa mitaani wanakubali ukweli. Ukitaka kuamini hata 2015 pamoja na Lowassa kuongea dk 3 kwenye kampeni mliaminishwa na Mbowe na mkadeki barabara. Ngoja niwape hints basi...
.
Huu ni ukweli mchungu.
 
Cdm ina wananchama wangapi hadi sasa acha uzembe wa kufikiri
Ada ya mwanachama wa chadema ni tsh2500 wanacham 1,250,000 tu wakichanga Hilo limeisha na hili mbali ruzuku za miaka 5 chama ni wanachama kama kimeweza kusimamisha wabunge kila jimbo ... wanakosaje wasimamizi na kumbuka hukochadema pesa sio kigezo kama kwa ccm... anglia kidogo clip a Lisu..... MSITUFANYE
WOTE WAJINGA mwishowa Nukuu ya LISU pale Dodoma
 
Ukiwasikiliza CHADEMA wa Jamii Forums waweza kudhani Tundu Lissu atakuwa Raisi wa nchi hii. Bora hata CHADEMA wa mitaani wanakubali ukweli. Ukitaka kuamini hata 2015 pamoja na Lowassa kuongea dk 3 kwenye kampeni mliaminishwa na Mbowe na mkadeki barabara. Ngoja niwape hints basi...

Kuna wapiga kura milioni 29 mliwahi kuwahesabu?, Kuna vituo zaidi ya 80000 vya kupigia kura nchi nzima mliwahi kuvihesabu?, Let say vipo kweli ili msiibiwe mnahitaji wasimamizi wenu CDM angalau wawili wawili kila kituo na mkisema muwalipe elfu 20 (20000)kila mmoja, kwa vituo vyote mnahitaji (20000x2x80000)zaidi ya bil. 3.2 je mnazo?

Kama mnazo zinawatosha wasimamizi wenu wasirubuniwe na pesa zaidi na CCM?,kwa tume hii nikiona mtu mzima tena mwanaume na p.umbu zake anaamini Lissu anaweza kuwa Raisi wa nchi hii namuona MPUMBAVU sana.

Badala ya kukomalia vitu vya maana mnakomalia UPUMBAVU wa mara Amsterdam mara Lwaitama. CHADEMA wote na viongozi hamna akili.
Huu ni ukweli mchungu mnoo kwetu wapenda manadiliko.
Lakini why chadema yenye wasomi hawayaoni haya??
 
Back
Top Bottom