Aliyewahi kuvuma kwa umaarufu katika mnada wa kununua nyumba za Lugumi!
Amefariki hivi punde huko mkoani Mwanza baada ya kuugua kansa kwa mda mrefu!
Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina lake lihimidiwe!
Taratibu za mazishi zitatolewa baadae!
Hapa chini ni Sauti ya Mwanafamilia ya Dokta Shika na kutoa mpangilio mzima wa Mazishi yake yatakayofanyika hapo kesho.
UPDATE:- Agosti 25, 2020 - Dkt. Shika azikwa
Mwili wa Dkt. Louis Shika Kidola '900 itapendeza' umepumzishwa katika nyumba yake ya milele jana Agosti 25,2020 katika kijiji cha Muda Nyanguge wilayani Magu- Mwanza.
Dkt. Shika amewahi kumiliki kampuni ya kusambaza kemikali viwandani nchini Urusi, taarifa ya wasifu wa marehemu ilieleza.
====
Lunyalula Kidola Makani maarufu kama Dr. Shika alizaliwa kitongoji cha Chamugasa kijiji cha Kalemela wilaya Busega mkoani Simiyu. Shika alijipatia umaarufu mitandaoni baada ya kutangaza kutaka kununua nyumba za mnada za Kigamboni kwa bei ya Milioni 900 au Mia tisa itapendeza zaidi.
Habari kutoka Hospitali ya Nyanguge Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, zimethibitisha kufariki kwa Dkt Shika ambaye alifariki Duniani jana saa nne asubuhi akiwa anauguzwa nyumbani kwa kaka yake Joseph Kidola, Wilayani Magu, Mwanza wakati wa uangalizi baada ya matibabu katika Hospitali ya Nyanguge iliyopo Magu mkoani Mwanza.
Kaka wa Marehemu amesema chanzo cha kifo cha Dr. Shika ni figo kufeli na kwamba atazikwa kesho mchana mkoani Mwanza. Dkt Shika alilazwa Hospitalini Nyanguge wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa siku kadhaa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu na umauti umemfika akiwa hospitalini hapo.
Ikumbukwe tu kipindi cha nyuma zilitoka taarifa kwamba Dkt Louis Shika anahitaji msaada wa kifedha kwa ajili ya kufanyiwa matibabu kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiafya.
Awali Dr. Shika alilazwa katika Hospitali ya Bugando Mwanza ambapo alipatiwa matibabu.
RIP Dr, Njia zetu ni tofauti kwani huyu ni mtu maarufu na kwa nyakati hizi msiba huu unaweza kugombaniwa na WANASIASA kama vile Yanga na Simba walivyomgombania BM