Dkt. Kipilimba, sasa yatosha!


Kwa kweli kwa akili kama za huyo jamaa na kama huko idara kweli kabisa tumelamba sio garasa tu bali Jockel na Mchezo ukaisha hapo..
 
Inawezekana walijua wakaamua kukaa kimya kila Mr haambiliki huu mwaka wake
 
Kwa mtazamo wangu mimi sidhani kama Kapilimba ana shida au shida na matatizo ndani ya TISS yameanzi kwa ndugu yangu Kapilimba. LAHASHA...shida hii ilianza mwaka 2008 pale ambapo ilianzishwa recrutment directory ya vijana wa kuingia TISS. Vijana wengi walikuwa wakifuatwa vyuoni na makazi kisha kupewa training kidogo kisha majukumu huku directory ikidhani kuwa kwa vile ni wasomi wanaelewa.

Kabla ya hapo kulikuwa na random selection ma DSO na RSO na wengine walikuwa wanapita mashuleni (sekondari) wanaongea na waalimu, wanaewa vijana ambao aminika toka chini na si mashuleni tu hata makazini, pia walitumia taasisi za dini kama makanisa na misikiti kuwatafutia watu waaminifu, wasiri na wachapa kazi na walitumika wangali katika nafasi zao zile zile.
Nadhani baada ya uwepo wa directory hii hayo hayakuzingatiwa na walichakuliwa walitazamwa kwa juu juu sana ndo mana haya yanatokea.

kuna mifimo mingi sana imevurugwa hapa katikati tukiirudia tutakuwa salama
 
Yaani muandamanaji mmoja amebeba bango eti Nyie Wasauzi tuliwasaidia kuwashinda makaburu duh!

Sasa ina maana kama uliisaidia nchi kupata uhuru ndo uingilie utaratibu wake wa kujiendesha kama taifa huru?
Na kwa vile maneno hayo yamesemwasemwa na Rais hata PM pale Mazimbu mbele ya Ramaphosa na hata Kabudi amekuwa akiyarejea basi wenye akili kule SA na nchi zingine wanajuwa wazi maandamano yalikuwa yameandaliwa na serikali
 
Hahaha

Nahisi lengo lake kuwe na idara ya uenezi kama chama cha siasa wakati ni nadra. Taasisi ipo imara sana
 
Je hao ambao walichukuliwa kimakosa makosa waondolewe kazini?
 
Wakimkia wakamteka wakampoteza kabsa then??????
 
Mkuu huo mfumo wa zamani wakutumia RSO na DSO ndio ulikuja kusababisha makada wa CCM na watoto wa vigogo kuwa recruited idarani kwa wingi bila kujali vigezo muhimu au uwezo wao kiakili, kitabia(usiri) na kimwili.

Na hao makada na watoto wa vigogo walikuwa watumishi wa idara upande moja na upande wa pili ni watumishi wa makundi ya kimtandao ndani ya CCM na wengine baadhi wanatumikia vyama vingine vya kisiasa au makundi ya kiimani ya kidini.

Hii ndio ikazalisha balaa kubwa la kuvuja siri za serikali ovyo hata kwa barmaids na wauza maandazi wanafungia wateja maandazi kwa kutumia classified documents(i.e. zilikuwa zinachapwa magazetini na akina Kubenea kisha magazeti yanatumika kama vifungashio).

Baada ya awamu ya 5 kushika dola kuna mabadiliko makubwa mno yanaendelea. Tena ya kuendana na kasi ya teknolojia na siasa za kiriberali au utandawazi.
Hiyo Directory uliyosema ilianzishwa 2008 ni ktk kujaribu kutoka ktk matatizo niliyosema.
 
.....
.....salute mingi sana MKUU
 
Huu mfumo wa directory pia umepelekea baadhi ya wanausalama kuwaingiza marafiki zao wengi ambao walikuwa wote kwenye discussion, hawaangalii tabia ya mtu husika ni kwamba kama ulibahatika kuwa rafiki wa mmoja wa wanausalama basi anapeleka majina moja kwa moja.

Hili nimelishuhudia sana.
 
Hivi kuna TISS ilikuwa mbovu kushinda ya awamu iliyopita?? wizi wote huo kuanzia kagoda mpaka escrow..tena hapa hapa ndani, Dr. Kipilimba amerithi TISS mbovu huwezi mlaumu kwa yanayotokea sasa.
 

Hapo ndipo walipokosea.

Ingawa makuruta huchukuliwa tangu vyuoni, makazini na sehemu zingine ulizotaja, bado ile misingi ya kumpata mtu sahihi ilianza kuvunjwa.

Tulianza kuiga wenzetu waloendelea ambao hata kama wanachagua watu kutoka vyuoni lakini wale watu wanakuwa wamepita mafunzo maalum kama kile cha Mbweni.

Tatizo ni aina ya mtu unaemchagua ambapo ukianza kuingiza undugu na kujuana ndipo matatizo yanaanza hapo.

Unafahamu, hata ukipata kijana aleiva kisawasawa na ukamtuma afanye espionage nchi fulani na akatoa taarifa za kutaka kuizuia ndege kule Jo'burg, ujue unao vijana makini, lakini tumeshindwa hata kuvuna vijana hata wale ambao wamezamia tu kule nakuwapa mafunzo makini watusaidie kwenye majangq kama hili la ndege, wategemea nini zaidi?

Kwenye masuala ya kulinda maslahi ya taifa haijalishi ni mtu au watu fulani tuu ndo wateule wachache wewe waangalia masuala haya kwa upana wake.

Wenzetu wengine siku hizi wameenda mbali sana wanaweza kuanza kukufuatilia hata unapokuwa ukitumia Xbox au PS na wakawa wanakupa mitihani bila wewe kujua wafanya majaribio ya kuonakama wafaa.

Mara tu waona barua inakwambia unahitajika mahala kwa usaili (wanakwambia labda umepata kazi nzuri tu) ambapo ukifika kule waambiwa kazi yako halisi na iwe siri na hata familia iisijulishwe.

Ila serikali hii sasa inaendelea kuifumua TISS ambayo ilioza sana na kuwa nyuma kwa kila kitu.
 
'Good thinking' hata wanaoitwa watu wasiojulikana ni doa kubwa sana '' why give them a shield that is if they are still existing the so called unknown criminals ''
 
HAWEZI KUKUELEWA, AMEAHIDIWA UBUNGE WA KILOMBERO NA UWAZIRI JUU.
SASA HIVI IDARA INAONGOZWA NA WAP.UMBAVU KAMA KINA MUSIBA.
HATA ISSUE YA KOROSHO, SUKARI, MBAAZI N.K NI MATOKEO YA UDHAIFU MKUBWA NDANI YA IDARA. WANAWAZA SANA VYEO NA MATUMBO YAO BADALA YA KUSHAURI MAMBO YA UCHUMI N.K
WAO WANAAMINI KUBORESHA UCHUMI NI KUNYANG'ANYA WATU PESA KWENYE AKAUNTI ZAO NA KWENYE BUREAU DE CHANGE, AIBU SANA!.
 

Acha utani mkuu, yaani Idara iongozwe na mtu kama Musiba?

Dah!!
 
Yaani muandamanaji mmoja amebeba bango eti Nyie Wasauzi tuliwasaidia kuwashinda makaburu duh!

Sasa ina maana kama uliisaidia nchi kupata uhuru ndo uingilie utaratibu wake wa kujiendesha kama taifa huru?
Ule ni myandiko wa Bashite [emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…