Dkt. Kimei(CRDB): Hali ya uchumi nchini ni tete

Status
Not open for further replies.
Hii habari iliyoandikwa hapa haina ukweli wowote.Wengine tunafuatilia speech za Dr Kimei na hakuwahi kusema yaliyoandikwa hapo juu.Gazeti la Mtanzania wamepotosha habari na sio jambo la busara kupindisha taarifa.mnawachanganya wananchi.
Narudia tena hayo maneno hayajazungumzwa na Dr Kimei labda yamewekwa ili kuuza gazeti.

Wewe ni msemaji wa CRDB?
 
NBC kwa sababu ya ugeni wao hawakuwa na ushawishi serikalini, hasa ikizingatiwa hawakuwa na network pana, hivyo tangu mwanzo walijiwekeza kwenye makampuni binafsi na ndiyo maana hata leo hawateteleki maana wadadili na makampuni makubwa tu. CRDB yeye anakuja kustuka kujifunika shuka asubuhi, maana sasa hayo makampuni ya mafuta anayosema yanamikopo toka NBC na bank za nje yeye hana portfolio huko. Na ndipo hapo atakapoonekana kajanja maana walizoe kufanya biashara na serikali
Kwa hiyo serikali inafilisika ama inawafilisi raia zake?
 
Mkuu huu ni wakati mzuri sana kununua property kwa wadau ambao wapo kwenye real estate, miaka ya nyuma speculators kwenye real estate walikuwa wengi sana. I guess now is the time for the real investors to make a killing.
Swala la kufa kwa biashara ambazo zilikuwa zinategemea hela za serikari to sustain their businesses sio tija provided those savings are channelled into other labour intensive investment and have returns. Hapo mzunguko wa pesa unakuwa umeuacha kwa njia nyingine na kama umejenga miradi ya nyumba in the future ni mapato au kuwekeza kwenye viwanda.
 
Kuna njia nyingi za kuvutia wateja kwenye biashara; lakini kutoa taarifa ambazo sio sahihi ni kupotosha jamii. Hizo khabar sio za kweli. Kiufupi Dr.Kimei hajatamka maneno hayo.
 
Dk. Charles Kimei

BENKI ya CRDB imesema imepunguza kasi ya utoaji mikopo kuangalia hali ya uchumi nchini inavyokwenda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, alisema kwa sasa beni hiyo inaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo wa kukopesheka.

“Kipindi hiki ni cha mpito bado watu hawajatulia, tunaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo kwa sababu kama hoteli zinayumbayumba lazima tusubiri hali ikae vizuri.

“Sisi tunasimamia fedha za watu hivyo hatuwezi kucheza nazo, tunazidi kujipanga kufuatana na sera ya Serikali,” alisema Dk. Kimei.

Akitoa mfano, alisema sekta za mafuta na gesi ni kama vile zimesimama hivyo CRDB inasubiri hali ikae vizuri iweze kufanya tathmini.

“Mikopo mingine kama ya watu binafsi tunaendelea kuitoa na kama ni waajiriwa waje watapewa lakini katika sekta nyingine hali imekuwa tete sana,” alisema.

Serikali ilieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya vipaumbele yatakayozingatiwa kama yalivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 ni pamoja na kuendeleza huduma za fedha, biashara na masoko.

Hata hivyo, hatua ya Serikali kutangaza mkakati wa kupunguza na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima imeanza kuathiri sekta nyingi ikiwamo ya fedha.

Licha ya mkakati wa kubana matumizi, pia Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika ada ambazo benki inatoza wateja wake kwenye huduma mbalimbali zinazotolewa ni miongoni mwa vitu vilivyochangia mtikisiko huo.

Wakati akisoma bajeti ya serikali bungeni kwa mwaka 2016/17, Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, alisema serikali inakusudia kutoza VAT katika huduma za benki zinazotozwa na benki zote nchini ili kupanua wigo wa kodi.

Chanzo: Mtanzania
Acha kupotosha watu kwa kutoa taarifa za uzushi. Gazeti la Mtanzania tunzeni heshima yenu kwa watanzania ili mzidi kupendwa na kuaminika. Toeni taarifa za kweli sio kuuza gazeti tu, tafuteni habari kwa kina zenye ukweli ndani yake. Tunzeni "brand" yenu.
 
Mmezoea taarifa za kumsifia mfalme sio? Hali si hali mtaani yaani mambo bado bila bila
 
Swala la kufa kwa biashara ambazo zilikuwa zinategemea hela za serikari to sustain their businesses sio tija provided those savings are channelled into other labour intensive investment and have returns. Hapo mzunguko wa pesa unakuwa umeuacha kwa njia nyingine na kama umejenga miradi ya nyumba in the future ni mapato au kuwekeza kwenye viwanda.
Mkuu, pesa zote ni za serikali na serikali ndio watu hao hao unaosema wanafanya biashara kutegemea pesa za serikali sijui unamaanisha nini hapo?!

Ukifanya biashara yoyote unalipa kodi ili iendeshe serikali na serikali haipaswi kuifungia hii pesa kwenye makabati ya BoT inatakiwa izunguke kwenye huduma mbali mbali ikiwemo na kwa wafanya biashara.

Mteja mkuu wa mfanyabiashara ni serikali sasa ukisema waliozoea kufanya biashara kwa pesa za serikali ndio wanalalamika sijui unamaanisha nini? Unadhani kuna namna nyengine serikali itapata huduma nje ya wafanyabiashara?

Nielimishe mkuu.
 
CRDB kwa muda mrefu wamekuwa washika hela wa Serikali, taasisi kubwa nyingi na waajiriwa wao walikuwa na akaunti huko. Agizo la Serikali kuwa fedha za taasisi zake zikae Benki Kuu ndio liloharibu ulinganifu waliouzoea, oops na yale matumizi na miamala ya anasa ilikuwa inapitia kwao pia.
Sijui kama mwaka huu Misa ya Shukrani pale KKKT Msasani itafanyika...
Mkuu nafikiri umenena vyakutosha na ubarikiwe sana,kama mashirika makubwa ya umma na watu binafsi walikua wanaweka pesa huko na sasa zimeondolewa lazma kimei alie sana sasa asitushughulishe aseme benki yake ndio imeyumba
 
H

Dk. Charles Kimei

BENKI ya CRDB imesema imepunguza kasi ya utoaji mikopo kuangalia hali ya uchumi nchini inavyokwenda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, alisema kwa sasa beni hiyo inaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo wa kukopesheka.

“Kipindi hiki ni cha mpito bado watu hawajatulia, tunaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo kwa sababu kama hoteli zinayumbayumba lazima tusubiri hali ikae vizuri.

“Sisi tunasimamia fedha za watu hivyo hatuwezi kucheza nazo, tunazidi kujipanga kufuatana na sera ya Serikali,” alisema Dk. Kimei.

Akitoa mfano, alisema sekta za mafuta na gesi ni kama vile zimesimama hivyo CRDB inasubiri hali ikae vizuri iweze kufanya tathmini.

“Mikopo mingine kama ya watu binafsi tunaendelea kuitoa na kama ni waajiriwa waje watapewa lakini katika sekta nyingine hali imekuwa tete sana,” alisema.

Serikali ilieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya vipaumbele yatakayozingatiwa kama yalivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 ni pamoja na kuendeleza huduma za fedha, biashara na masoko.

Hata hivyo, hatua ya Serikali kutangaza mkakati wa kupunguza na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima imeanza kuathiri sekta nyingi ikiwamo ya fedha.

Licha ya mkakati wa kubana matumizi, pia Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika ada ambazo benki inatoza wateja wake kwenye huduma mbalimbali zinazotolewa ni miongoni mwa vitu vilivyochangia mtikisiko huo.

Wakati akisoma bajeti ya serikali bungeni kwa mwaka 2016/17, Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, alisema serikali inakusudia kutoza VAT katika huduma za benki zinazotozwa na benki zote nchini ili kupanua wigo wa kodi.

Chanzo: Mtanzania
Hii habari haina ukweli wowote na inapotosha jamii!gazeti kubwa kama hili kuandika vichwa vya habari vya kuvutia wateja inasikitisha!Muda ufike tutafute na tuandike taarifa za kweli zinazoendanqr na habari kamili!Tutoe taarifa sahii na dr kimei hajaongelea hayo yote mliyoandika!
 
Embu Kimei aache kupotosha,aseme ukweli kwamba tangazo la serikali kwamba fedha zake zisiwekwe ktk mabenk binafsi ndicho kinachoiyumbisha CRDB,hivi kama mashirika yote ya umma yamehamisha fedha zake kutoka huko kwann wasione maisha magumu,fikiria Tanesco,ewura, n.k wanaweka billion of shilings ktk benki yako alaf watoe zote usiyumbe Kimei acha kutafuta huruma ya Wananchi
 
Mkuu huu ni wakati mzuri sana kununua property kwa wadau ambao wapo kwenye real estate, miaka ya nyuma speculators kwenye real estate walikuwa wengi sana. I guess now is the time for the real investors to make a killing.
Personal naona bado but that is matter of my beliefs ningesubiri kwanza correction bado ipo kwenye early stages, nimesikia nyumba kuanza kuwa empty kwa sababu ya watu waliokuwa wanapangishia vimada, benki imeanza foreclosure kwa wale waliokuwa wananunua nyumba kubwa kupita uwezo wa mishahara yao and all other ufisadi supported economic activities.

Based on those facts itafika wakati rent charges au bei za nyumba zitarudi on realistic asking prices kutokana na uwezo wa mtanzania na rough estimate ya bei halisi utaijua kwenye minada ya benki overtime kwa sasa kuna watu watakurupuka tu kununua lakini bei zitashuka tu provided ufisadi aurudi na mpaka wote tuanze kuishi kwa vipato halali.
 
Kimei acha kutisha watu... niko katikati ya jiji la Dar, DSE iko sawa.. umetumia instrument gani kusema UCHUMI HALI TETE..?

DSE ndio indcator ya haraka kidogo... au katumia macho..? Dr. Kimei nia yake hapo ni kuongelea hiyo VAT.. ili tu afikishe ujumbe.. kuwa VAT anapinga.. kasema indirectly..!!

Kama CRDB ilizoea fedha za madili toka serikalini sasa hakuna.. anaona net flow inapungua CRDB.. asiseme hali ya UCHUMI ni tete..

Aache kututisha..!!
endelea kujadili uchumi kwa theory za stock.exchange fake ya DSE.nenda kwenye real life situation mtaani.Dr kimei amechelewa kuongea huo ukweli.
 
Hali ni tete mkuu!..ingia mtaani watu wanafunga maduka.cjui huko kijijini kukoje.wanaopigwa kiyoyozi hii hali hawaijui kabisa!..
Aisee mkuu nimeshangaa kuona"frame" nyingi zimefungwa kariakoo. Hivi wachumi wetu wako wapi karne na karne wanashindwa kuteletea suluhisho?

Ninachokiona ikitokea uchumi wa nchi umepanda basi ujue mtaani tutasugua na ikitokea uchumi wa mtu mmoja mmoja umepnda basi ujue serikali iko hoi.

Hivi kiuchumi ikoje hii? Hao walio balance uchumi wa serikali na ule wa mtu mmoja mmoja waliwezaje?
 
Kimei hajaishauri serikali,au anaogopa kuieleza serikali ukweli!!! Serikali izilinde taasisi,viwanda na wafanyabiashara wakubwa nchi inawategemea sana na niwachache
 
Mkuu, pesa zote ni za serikali na serikali ndio watu hao hao unaosema wanafanya biashara kutegemea pesa za serikali sijui unamaanisha nini hapo?!

Ukifanya biashara yoyote unalipa kodi ili iendeshe serikali na serikali haipaswi kuifungia hii pesa kwenye makabati ya BoT inatakiwa izunguke kwenye huduma mbali mbali ikiwemo na kwa wafanya biashara.

Mteja mkuu wa mfanyabiashara ni serikali sasa ukisema waliozoea kufanya biashara kwa pesa za serikali ndio wanalalamika sijui unamaanisha nini? Unadhani kuna namna nyengine serikali itapata huduma nje ya wafanyabiashara?

Nielimishe mkuu.
Kigezo cha kufungua biashara ni opportunity zilizopo; mtu awezi kufungua biashara ya hoteli kwa kutegemea semina tu za kifisadi lazima ufikirie kuna substitute ya hizo semina kufanyika sehemu zingine ambazo ni bure kwa serikari. Pale utaratibu utakapo badilika kama uliwekeza kwa sababu ya vigezo vya warsha na semina madhara yake ndio haya.

Tatizo ni kwamba uchumi wetu umekuwa ukitegemea pesa za kifisadi kwa asilimia kubwa ambazo zinaanza kuyoyoma ni tatizo kwa sababu mzunguko umepungua na ndio chanzo cha kilio; wao kama serikari kuzuia kudorora kwa uchumi walitakiwa watafute mbinu za kuirudisha hii hela. Common sense says bado na wao watakuwa wanasubiri kujua how much savings they will make maana zoezi lenyewe halina ata mwaka. Lakini walitakiwa waweze ku anticipate the possibilities of risks za maamuzi yao na kutenga budget ya kufidia mzunguko wa hela kwa kuirudisha kwa namna nyingine ambazo zina social impact.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom