Zanzibar 2020 Dkt. Hussen Mwinyi: Tumaini linalorejea Zanzibar

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
179
DKT HUSSEN MWINYI TUMAINI LINALOREJEA ZANZIBAR

Na, Deogratias Mutungi

Nianze makala haya kwa kusema Zanzibar na Wazanzibar kwa ujumla wake awamu hii wanaweza kupata kiongozi aliye bora zaidi na mwenye maono ya pekee katika ukombozi wa Mzanzibar mwenyewe dhana hii inajengwa kutokana na waliojitokeza kuchukua fomu ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa wagombea wenye sifa zilizotukuka kiuongozi kiitikadi, kiimani na kitaaluma.

Hata hivyo maudhui ya “Tumaini linalorejea” ni nadharia kuwa maisha ya binadamu ni mapambano, ni mwenye uthubutu tu ndiye hatimaye hushinda aidha njia ya kuelekea ushindi siyo lazima iwe imenyooka, kuna wakati inapinda na kuna wakati inakuwa na vizingiti na wakati mwingine fumbo linakuwa halijafunguliwa na kutunza lengo ni sehemu ya kudumisha tumaini na hatimaye likarejea kwenye njia iliyochaguliwa na ushindi kwenda kwa kwa mstahiki. Na sasa makala haya yanasema tumaini linalorejea Zanzibar hatimaye limepatikana.

Ikumbukwe kuwa kama taifa tupo kwenye kipindi na hatua muhimu kidemokrasia wakati tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo Oktoba mwaka huu, Kama ilivyo desturi na taratibu ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM utaratibu wa ndani unaendelea ili kumpata kiongozi mwenye uwezo, uthubutu na misimamo isiyoteteleka katika nafasi ya Urais ili kukabiliana na changamoto za kimaendeleo ndani ya nchi na katika anga za kidiplomasia.

Makala haya kwa ufanisi wa hali ya juu yanaelekeza jicho lake la uchambuzi wa kisiasa kwa kumulika siasa za Zanzibar hasa katika nyakati hizi za kuwania nafasi mbalimbali za kiuongozi, aidha makala haya yanaangaza uwezo, weledi na utendaji kazi wa wagombea waliochukua fomu kuomba ridhaa ya ndani ya chama kutoa nafasi kwao kuwapa fursa kama wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM.

Tumesikia na kuona waliojitokeza ni wengi na wenye uwezo, sifa na uzoefu wa kutosha katika siasa za Tanzania bara na Visiwani Zanzibar kwa kuomba ridhaa ya kupewa nafasi hiyo muhimu kisiasa, lakini mantiki inaonyesha kati ya wengi waliojitokeza ni Dkt. Husseni Mwinyi tu mwenye sifa za upekee na utofauti wa aina yake anayestahili kupewa nafasi ya kuwa Urais wa Zanzibar na si vinginevyo, Wala huu si upendeleo bali ni ukweli wa kimantiki unaotumia mifumo ya kisiasa kumtambua mtu kulingana na sifa zake za kiuongozi, Kwa dhana hiyo uwajibikaji aliouonyesha Dkt. Mwinyi kwenye nafasi ya uwaziri unambeba sana ukilinganisha na wagombea wengine.

Kimantiki na kisiasa Dkt. Mwinyi ni tumaini linalorejea Zanzibar kuikomboa Zanzibar kifalsafa, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni, Upekee wa kiuongozi kwa Dkt. Mwinyi unasimama katika falsafa ya weledi, utashi, misimamo na maamuzi ikiwa ni pamoja na kuiva kiitikadi na kitaaluma “red and expert” bila shaka hili halina ubishi wa aina yoyote na ni imani ya makala haya kuwa hakuna wa kuhoji juu ya dhana hii dhidi ya Dkt. Mwinyi. Aidha mbali na wagombea wenzake ndani ya Chama Cha Mapinduzi kutomfikia kiuwezo katika nadharia ya uongozi lakni bado Dkt. Husseni Mwinyi huwezi kumliganisha na mgombea wa chama chochote cha kisiasa hasa upinzani ndani ya Zanzibar na viunga vyake.

Pengine tujiulize ni kwanini halinganishwi na upande wa pili katika siasa za upinzani, Sababu kuu naya msingi ni moja tu ambayo ni kuwa Dkt. Mwinyi ni kiongozi mwenye msimamo wa kutetea hoja yake, Yuko tayari kusikiliza hoja mpya na kuzikubali kama hoja hizo zitakuwa zina maslahi kwa watu badala ya maslahi kwa makundi au mtu binafsi.

Mathalani kisiasa uwezi ukamlinganisha Dkt. Mwinyi na Mgombea wa ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharrif Hammad viongozi hawa wawili ukiwaweka kwenye mizania ili kutafuta ulali wao kisiasa bado Dkt. Husseni Mwinyi anampita kwa mbali sana Maalim Seif Sharrif Hammad, nafikri hata angeulizwa Maalim mwenye angekiri mashiko ya hoja hii na ukweli wake.

Lakini zipo sababu zinazowatofautisha nazo ni busara, upeo, tamaa ya madaraka na unyeyekevu kwa watu, kama makala haya yangetoa asilimia dhidi ya viongozi hawa basi Dkt. Mwinyi angepata 96% dhidi ya Maalim ambaye angepata 50% kwa mantiki hiyo Mwinyi ni kiongozi anayeweza na mwenye sifa zilizotukuka na za upekee katika uongozi ndani ya taifa letu.

Ikumbukwe kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kilianza kufanya kazi za kuainisha sifa za mgombea nafasi ya Urais mwaka 1985 wakati Mwl. Nyerere anang’atuka zilitungwa sifa thelathini na tano, ikaendelea hivyo hivyo kwa awamu zilizofuatia ikiwa ni pamoja na 1995, 2005, 2010, 2015

Na miongoni mwa sifa za mgombea Urais zilizotajwa na kuorodheshwa ni pamoja na; Kuwa na upeo wa kuona mbali, Asiyeyumbishwa katika msimamo wa kufanya maamuzi, Awe na uzoefu wa kuongoza, Awe mwadilifu, Asiependa kusikiliza majungu, Awe na elimu ya Chuo Kikuu, Asiwe na tamaa ya kujilimbikizia mali, Achukie rushwa, Asiwe mbinafsi na Asiwe Mbaguzi, hizi ni miongoni mwa sifa zinazomtambulisha mgombea wa CCM kuwa safi na mwenye kustahili kupata nafasi ya kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi.

Bila shaka Dkt. Husseni Mwinyi ndiye kiongozi mwenye sifa zilizoainishwa hapo juu na ndiye anayestahili kwa vyovyote vile kuipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi, Waswahili wanasema “Mnyonge myongeni lakini haki yake mpeni, tunahitaji kumpa nafasi Dkt. Mwinyi kuivusha Zanzibar kutoka hapa ilipo, ni kiongozi mwenye falsafa za kimapinduzi na mabadiliko katika kuwatumikia Wazanzibar, aidha ni kiongozi mwenye kutumia busara kufikia maamuzi yenye tija kwa watu na maendeleo yao.

Katika maandiko matakatifu ya dini ya Massiha (Yesu Kristo) kuna msemo usemao “Wanyenyekevu watarithi na kutawala dunia” Msemo huu wa maandiko matakatifu ni msemo ambao pamoja na mambo mengine unaelezea watu wa haiba ya Dkt. Husseni Mwinyi kwa vipi wanazingatia maadili ya chama na utii kwa viongozi na wazee bila kuuza roho yake kwa shetani, Si rahisi kujua lini Dkt. Mwinyi ana jambo linalomsumbua mpaka limemsumbua kweli.

Kwa muda mwingi Dkt. Husseni Mwinyi hutuliza roho yake kwa tabasamu na kukakataa kuzama katika sononeko, Tabia yake hiyo imemsaidia kutoweka fundo rohoni na vilevile kuwafanya marafiki na maadui zake wasijue kusudio lake wakati uliopo na pale anapobaini kwamba “ huu ndio muda muafaka” husema bila kificho wala woga chochote kile kilichopo rohoni mwake.

Kwa tabia hizo na hulka za namna hiyo kisiasa unaweza kumfananisha Dkt. Husseni Mwinyi na rais wa zamani wa Afrika Kusini, mzee Nelson Mandela ufanano wao unaanzia kwenye dhana ya hulka na utendaji kazi, Mandela alikuwa mpole na mwepesi wa kuzikiliza shida za watu wake, Mandela alisimamia mrengo wa kuwaunganisha watu na kuwaleta pamoja bila ubaguzi wa aina yoyote, ndivyo ilivyo kwa Dkt. Husseni Mwinyi ni kiongozi mwenye utashi wa kusikiliza na kutatua kero za watu zinazowakabili ili kuwakomboa pale walipokwama, Mandela na Mwinyi wote kwa pamoja wanaunganishwa na falsafa chanya kwa kuwa na fikra za kumkomboa myonge anayeonewa.

Kwa lugha nyepesi ya kisiasa ni vigumu kutenganisha hulka na tabia za Mzee Mandela na Dkt. Husseni Mwinyi, kama hivyo ndivyo basi Chama Cha Mapinduzi CCM kimpe fursa mgombea huyu aweze kufata nyayo za pacha wake mzee wetu Nelson Mandela kwa kuwaletea Wazanzibar ustawi wa maendeleo uliotukuka, Ni Imani ya makala haya kuwa Mwinyi atatenda na kufata yale yote ambayo Nelson Mandela aliwatendea wana Afrika Kusini na kuacha alama iliyotukuka, tuna imani na Dkt. Mwinyi kuwa atapata nafasi ya Urais na hatimaye atatenda na kuacha alama kwa Wazanzibar.

Aidha Dkt. Husseni Mwinyi anatambua kuwa Zanzibar inakabiliwa na changamoto lukuki hasa katika maeneo ya ajira, muungano na uchumi wa mtu mmoja mmoja pia ameishi na kulelewa katika mazingira ya kizanzibar hivyo basi anaelewa fika na kutambua changamoto hizo na ni kwa namna gani anaweza kuzitatua hili kuboresha maisha ya Wazanzibar, Kwa dhana hizo Dkt. Mwinyi ni chaguo tosha kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika kuhakikisha anapeperusha vyema bendera ya chama katika kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu hapo Oktoba.

dmutunid@yahoo.com
 
Usingehangaika kuandika habari ndeefu namna hiyo wakati lengo lako liko wazi. Na hizo sifa unazojaribu kumpa ili kujenga hoja yako wala hana.

Wazanzibari walio wenge wameshakata tamaa na kupoteza matumaini kwa Kiongozi yeyote toka chama cha mapinduzi. Toka kuanzishwa mfumo wa vyama vingi ccm imekuwa ikiwalaghai kupitia kwenye majukwaa. Sasa wamechoka na kibaya zaidi wamekuwa wakipitishiwa mgombea na Tanz Bara.

Safari hii usijeshangaa mabadiliko makubwa yakatokea huko Visiwani ktk kukataa kuburuzwa na Bara. CCM imeshindwa kuwapatia Kiongozi atakaeondoa Uunguja na Upemba. Kila anaekuja ukoleza moto wa ubaguzi. Na wao wanaamini kuwa ni Ndugu moja ila Viongozi wao wanawafarakanisha ili waweze kuwatawala kwa shinikizo kutoka Bara.
 
Walio chukua form wote wa ccm Zanzibar bado sijaona wa maana kwa kuwatukia wazanzibari, na hakuna alie tokea toka ilipo asisiwa mfumo wa vyama vingi, upinzani umekuwa ukiimarika siku hadi siku.

Siasa za Zanzibar zinahitaji matumaini na matendo, ccm Zanzibar wamekuwa kama mbuni, kutia kichwa kwenye mchanga, kiu ya wazanzibari ni kuona mfumo wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar unabadilika ,matarajio ya wazanzibari ni ule makataba wa muungano.

Uchumi

Uchumi wa Zanzibar imekuwa ni kizungu mkuti, Zanzibar ni visiwa yenye eneo dogo ambalo linategemea zaidi biashara na utalii, Leo Zanzibar hatuna Bandari wala Airport terminal ya kimataifa, viongozi wa upinzani wamekuwa wakipigia upatu sera zao kufanya mabadiliko hayo kwanza kwa muda wa miezi 6 tu , ndio moyo wa Zanzibar.

Leo zaidi ya miaka 15 terminal haijamaliza, mabilioni yakiliwa ujenzi haumalizi.

Ccm Zanzibar miaka 60 inakata imeshindwa kuwapa maendeleo wananchi na matumaini, ni wakati wa kufunga virago, kila ajae anakuja ku endelea na kuimaliza Zanzibar
 
Tanzania ni Republic hatutaki tabia chafu iendelee ya kurithishana urais kimila na kifamilia!! kwani kunao wangapi wenye akili ya uongozi nchi hii si lazima kina Mwinyi na kina Karume tumechoooka ati, kila mtu ana haki kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi , Zenji ni yetu sote hatutaki usultani hapa ni kwetu watu weusi!! kwanza wako kina Jecha , Nahodha , Seif nk hao ni wenyeji wa Zenj wanafaa zaidi huyo Mwinyi junior ni Mzanzibara!! akaa bara hajui chochote cha Zenji wala hawezi kuwa na uchungu wa mahali asipoishi!! hata bei ya mapembe ikiongezeka hawezi kujali!!! hatumtaki!

sie wabara wote tunamtaka Jecha awe rais kwa maslahi mapana ya muungano, Jecha ni jeshi la mtu mmoja! mzalendo wa kweli mwenye mapenzi ya dhati kwa muungano, mwalimu mkuu wa zenji mwenye ujasiri shupavu na mwenye akili zaidi mjini Zenji kwa kujificha chini ya uvungu na kumtangaza rais!

huyu Jecha wazenji wana chuki nae na wanamzingua sana kujaza forms zake za udhamini sasa mimi ni sisiem nawashauri kamati kuu sisiem impitishe Jecha kibabe hata wazenji wasiposaini udhamini na apitishwe kugombea na kuwa rais , huyu ndie anatufaa bara kwa kuwa ni mtu mzima, ni mzalendo wa vitendo, ana hekima na busara na kwakuwa wazenji wamemzingua basi ana usongo nao atawaadhibu, atawakomesha na kuwanyoosha kina yakhe wote wenye fyoko fyoko kuanzia hasimu yake mkubwa Maalim na hata wasio na fyokofyoko, atapiga wote wenye damu moto na wenye damu baridi, atapiga wote wenye mihemko na waliotulia!!! sie waBara tunahitaji kumsimika Zenji rais ambae wazenji wanamchukia na hawamtaki, tukiweka wanaempenda wataelewana nae kwenye vikao vya kahawa na halua na atavunja muungano!!

Kwanza kuna kashfa kubwa ya upotevu wa mabilioni huku bara za ufisadi wizarani kwa huyo Mwinyi junior yasemekana wameiba mabilioni kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi wa hesabu!! kuna uzi mahsusi ulishatupiwa humu JF.
 
Kiu ya wazanzibar ni kuona Serikali tatu au kuvunjika kabisa kwa Muungano. Takwa hili haliwezi kutekelezwa na Rais kutoka CMM abadan. Raisi kutoka upande wa CMM huekwa kwa kutumia mabavu na nguvu ya jeshi, ataweza wapi kutetea Wanzanzibar wakati anajuwa ni vipi ameingia ikulu. Atakachofanya ni kujilimbikia mali na kumaliza muda wake apumzike.
 
Wazanzibari waliuondoa Usultani,Walifanya Mapinduzi kuondoa thulma ya kuridhishana uongozi kifamilia...

Sasa CCM Zanzibar wanataka kuuendeleza Usultani kwa style Yao..

Zanzibar Safari iende upinzani,ACT,CDM au chama chengine Cha siasa lakini sio CCM
 
Mtoto wa mwinyi anataka urais Zanzibar,mtoto wa karume anataka urais Zanzibar na mtoto wa abood Jumbe naye anataka urais Zanzibar. Hii kitu inaitwa Nini?
 
Samahani kabla sijachangia Deogratius Mutungi, wewe una uhusiano na mkuu wa usajili wa vyama Jaji Mutungi?

Isije ikawa tiyari una majibu ya uchaguzi kabla ya uchaguzi, sisi tukaumiza vidole gumba kwa kubofya, keyboards..

Everyday is Saturday... :cool:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom