Dkt. Emmanuel Nchimbi kutogombea tena Ubunge jimbo la Songea Mjini



NA STEPHANO MANGO,SONGEA

MBUNGE wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi amewaacha njia panda wapiga kura wake baada ya kuwaeleza taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Ccm kwa kipindi cha miaka 10 katika jimbo hilo na kuwaambia huenda kuwa hata gombea tena katika Jimbo hilo

Dkt Nchimbi akizungumza jana na viongozi wa mashina, matawi, kata ,madiwani,wenyeviti wa mitaa, mabalozi na wa Wilaya ya Songea mjini kwenye uwanja wa michezo wa Majimaji mjini hapa alisema ni ukweli uliowazi kuwa tumepata mafanikio makubwa katika maendeleo ya jimbo kwenye sekta ya elimu,maji,afya,barabara na ujenzi,kilimo na ushirika,mifugo na uvuvi,ardhi na maliasili,umeme,mawasiliano,biashara na masoko,utawala bora na michezo

“Nimepongezwa sana kwa mafanikio makubwa tuliyoyapa lakini naomba nikiri wazi kuwa kazi hizi sikuzifanya peke yangu, hivyo kwa heshima kubwa naomba niwashukuru nyie viongozi wenzangu wa chama na serikali mliopo hapa na wale ambao wamepita ndani ya miaka hii kumi ya uongozi wangu kwani walikuwa chachu ya maendeleo,hata hivyo sikusudii kugombea tena jimbo la Songea” alisema Nchimbi

Alisema kuwa katika kipindi hiko cha miaka kumi Jimbo la Songea Mjini lilipata heshima kubwa sana kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kumuamini na kumteua kushika Unaibu Uwaziri katika Wizara mbalimbali na baadae uwaziri kamili katika wizara mbili tofauti lakini pia amekuwa chachu na kimbilio langu wakati wote ambapo nilikwama katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya jimbo la Songea, hivyo namshukuru sana yeye binafsi na serikali yake kwa imani na mapendo yake kwa wananchi wa Songea Mjini

Alisema kuwa nimepata wakati mgumu sana kuyasema maneno haya lakini nimeyasema kwani ilani na ahadi zangu binafsi nimezitekeleza kwa ukamilifu na nyie wenyewe ni mashahidi kwani yote niliyoyasema hapa huko kwenye maeneo yenu mnayaona hivyo nataka niondoke nikiwa kifua mbele

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi hao walionyesha masikitiko makubwa sana na maneno aliyoyasema Dkt Nchimbi ambayo kisiasa yalionyesha kuwa ndio anawaaga kutogombea jimbo hilo ingawa pia hajasema anakwenda wapi.

Kwa upande wake Kada wa chama hicho Alfonce Haule alisema kuwa hatua hiyo imewachanganya sana na imewaacha njia panda wapigakura wa Jimbo hilo hivyo wazee wamejipanga kwenda kuzungumza nae ili aweze kuja kugombea tena kwani mchango wake kwa maendeleo ya jimbo hilo ni mkubwa sana.

Haule alisema kuwa Dkt Nchimbi uongozi wake tuliuzoea na hata alipokosea tulimshauri na alijirekebisha sasa leo ghafla anatuacha na nani na huyo anayekuja mpaka tutakapomzoea na kumsahihisha atakapokosea itakuwa kasi ya maendeleo imesimama kwa muda mrefu

Alisema kuwa timu ya wazee iliyoundwa kwenda kumshauri arudi ni timu makini na tunaamini siku ya jumapili juni 28 mwaka huu itatuletea majibu ili tujue namna ya kujipanga ingawa tunaamini kuwa Dkt Nchimbi ni msikivu ataelewa nia na kilio cha wanasongea

Naye kada mmoja wa Ccm kutoka Wilaya ya Nyasa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ya mkononi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa Dkt Nchimbi Juni 19 na juni 20 alikuwa Wilayani humo na alikutana na makundi mbalimbali na kuwakaribisha kwenye misa ya shukrani kwa Mungu kwa jinsi alivyomlinda kwa miaka yote ya maisha yake ambapo misa hiyo ilifanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mbaha wilayani Nyasa.

Kada huyo alisema kitendo hicho kimewashtua viongozi mbalimbali wa chama na wananchi kwani hawaelewi nia yake kwasababu amewaita na amesali nao na amekula nao kisha akawashukuru kwa kuja kwao kujumuika nae kwenye hafla hiyo bila kueleza nia kama ana nia yoyote, kumekuwepo na shinikizo kubwa kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wilayani Nyasa la kutaka agombee jimbo la Nyasa kwa kuamini kuwa kasi ya Maendeleo iliyopatikana Songea itapatikana pia Nyasa.

Awali duru za kisiasa zilionyesha kuwa miongoni mwa makada vijana ambao walikuwa wanatajwa sana kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais Dkt Nchimbi alikuwa ni mmojawapo lakini mpaka leo hajajitokeza kuchukua fomu na wala kusema jambo lolote

Hata hivyo taarifa kutoka kwa mtu wa karibu naye ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe amesema kuwa Dkt Nchimbi amekwisha kaa vikao na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali mjini Songea na kuwashukuru kwa kipindi chake cha miaka kumi ya ubunge, ingawa ajasema chochote kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu Dr Nchimbi anafahamika sana kwa uwezo wake wa kutunza siri moyoni kwa hiyo lolote linaweza kutokea anaweza kugombea Nyasa au anaweza kugombea Songea au hata Urais siku zinakaribia kitendawili kitajitegua.
MWISHO
 
.......Naye kada mmoja wa Ccm kutoka Wilaya ya Nyasa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ya mkononi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa Dkt Nchimbi Juni 19 na juni 20 alikuwa Wilayani humo na alikutana na makundi mbalimbali na kuwakaribisha kwenye misa ya shukrani kwa Mungu kwa jinsi alivyomlinda kwa miaka yote ya maisha yake ambapo misa hiyo ilifanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mbaha wilayani Nyasa.

Kada huyo alisema kitendo hicho kimewashtua viongozi mbalimbali wa chama na wananchi kwani hawaelewi nia yake kwasababu amewaita na amesali nao na amekula nao kisha akawashukuru kwa kuja kwao kujumuika nae kwenye hafla hiyo bila kueleza nia kama ana nia yoyote, kumekuwepo na shinikizo kubwa kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wilayani Nyasa la kutaka agombee jimbo la Nyasa kwa kuamini kuwa kasi ya Maendeleo iliyopatikana Songea itapatikana pia Nyasa.


Hata hivyo taarifa kutoka kwa mtu wa karibu naye ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe amesema kuwa Dkt Nchimbi amekwisha kaa vikao na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali mjini Songea na kuwashukuru kwa kipindi chake cha miaka kumi ya ubunge, ingawa ajasema chochote kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu Dr Nchimbi anafahamika sana kwa uwezo wake wa kutunza siri moyoni kwa hiyo lolote linaweza kutokea anaweza kugombea Nyasa au anaweza kugombea Songea au hata Urais siku zinakaribia kitendawili kitajitegua.

Ndugu yangu yangu, ACHA KUZUNGUKA MBUYU! Sema kweli daima. Usiwe na fitina.
1. Hao unaowataja bila kutaja majina yao ni kina nani (angalia ilipowekwa rangi nyekundu).
2. Usifanye kuwa nia ya Nchimbi kugombea Nyasa ni tetesi. Hana siri anayotunza. Ukweli ni kuwa ATAGOMBEA Nyasa na mpango huo anao tangu zamani. Taarifa zipo!
3. Umeonesha kuwa alifanya misa kujitambulisha...Sasa hapo unadhani nini kinafuata? Hakuna makundi yoyote yanayo muhitaji. Hii ni propaganda. Atakutana na Muhandisi Manyanya maana naye kajipanga vema huko Nyasa. Kumbuka pia kuna UKAWA! Nchimbi kazi anayo. Nashauri atosheke na kazi alokwisha fanya kama mbunge kwa ZAIDI ya miaka 10!


 
Ukuaji wa siasa kwa vijana wazawa wa Songea mjini wa muhatarisha mbunge Nchimbi kwa hata kupelekea kutaka mabadiliko ya uongozi lakini inaonekana njemba bado inauchu na madaraka kwani aliandaa mpango kabambe wa watu kumlilia na kuonesha bado anahitajika sana duu..ccm mwaka huu sio mchezo ngoja tufuatilie episode tuone kama atawaachia wengine wagombee au ataendelea kugombea ubunge daa...kweli shikamoo CCM.
 
sio kwa nchmbi tu, hili ni tatizo la mfumo wa madaraka ndani ya ccm, maana vjana nao wanataka kushika hatam..
 
Inasemekana ule mpango wa kusema hatagombea ni moja ya strategies zake na kuna watu amewaandaa tayari ili waonekane wanamuomba agombee na kumlilia ili achukue nafasi tena...sijui kakosa mbinu mpaka atumie hizi danganya toto??
 
Inasemekana ule mpango wa kusema hatagombea ni moja ya strategies zake na kuna watu amewaandaa tayari ili waonekane wanamuomba agombee na kumlilia ili achukue nafasi tena...sijui kakosa mbinu mpaka atumie hizi danganya toto??
Alikuwa na mpango wa kuchukua fomu ya kugombwa uraisi lakini muda umeshamwacha.Nafikiri kada wa mwisho kutia nia atakuwa huyu caterpillar na ni wa 42 kwenye orodha. Wapo waliodhani ni kuwa na million ya kuchukua fomu. Hao wameishia njiani kwa kukosa hela ya kuendelea kupata wadhamini watapongezwa kwa kutuniaha mfuko wa chama chao kwa hiari. Wengine walidhani elimu ya darasa la saba inaweza kuongoza nchi na hata wasomi wengine wa chuo kikuu kwa kushindwa tu kusoma masharti wakadhani umri wa miaka 34 wanaweza kuteuliwa. Sasa nafasi aliyobaki nayo Nchimbi ni kukimbilia fomu za ubunge jimbo aliloacha marehemu Komba. Vinginevyo asubiri fadhila za raisi ajae na awe alikuwa na maelewano mazuri nae kwani hata swahiba wake naona mambo sio mazuri kwenye uteuzi wa mshika bendera ya kuwania uraisi.
 
Kaka Yangu wa Songea Mjini Emanuel ametangaza Rasmi kutogombea ubunge.

Mimi nimeamua kuhangaisha ubongo wangu na kulitazama hili jambo kwa upeo mpana, nimeng'amua kwamba nakaribia kupata jibu la maswali niliyokuwa nikijuliza kuhusu Plan B ya King Maker na Kaka yangu wa Monduli.

Wamegundua kuna nafasi kubwa ya kupatikana kwa nafasi moja ya mgombea kijana kwenda katika zile nafasi tatu zitakazopigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu.

Kutokana hali hiyo nao kwa akili ya fasta wameona walitafutie kundi hili kijana mwenzao wamuingize kwenye mpambano ili Upande wao waidhibiti nafasi hii kutoka katika kundi la vijana.

Kijana mwenyewe siyo mwingine bali ni yule yule aliyepikwa, aliyekulia na kupata malezi ya kiuongozi ndani ya chama. kijana mtiifu sana kwa Kaka Yangu wa Monduli naye ni Emanuel wa Songea.

Akili yangu inaniaminisha kwamba kuuacha Ubunge ni mwanzo wa safari hii na siku chache zijazo Emanuel wa Songea atajitokeza na kuchukua Fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama ili awe mgombea wa Urais katika uchaguzi ujao.

Matokeo wanayoyatarajia ni:

1) Emanuel wa Songea atawazidi wagombea wengine wa Kundi la Vijana na kuikamata nafasi hiyo ambayo inaweza kuwepo.

2) Ikitokea Kaka Yangu wa Monduli amevivuka vikwazo vyote na kufika kwenye hatua ya Tatu Bora. Hatakuwa na Upinzani mkubwa kutoka kwa Emanuel wa Songea ambaye atakakuwa amepita kupitia kundi la Vijana Viongozi, Maana Kaka Yangu wa Monduli anaamini akifanikiwa kufika 3 Bora hakuna wa kumzuia.


3) Ikitokea Kaka Yangu wa Monduli hajafanikiwa kuvuka na majaribio yao yote ya kushinikiza yasipofanikiwa, nguvu zao watazihamishia kwa kwa kijana wao Emanuel wa Songea.

Akili yangu inaniaminisha bila shaka yoyote Kaka Yangu wa Monduli na King Maker wamepanga kuwekeza nguvu ya kutosha kwa Emanuel wa Songea ili malengo yao yakuwa na nguvu katika Serikali ijayo na ndani ya chama yatimie.

Karibuni

Hivi unaelewa hadi tarehe ya leo 29/6 zimebekia siku ngapi kabla ya dead line ya kurudisha fomu kwa wagombea uraisi? Akachukue fomu azunguke mikoa 15 bara na visiwani kupata wadhamini atawahi? Hata kama atapewa ile ndege maalumu ya boss bado kachelewa.
 
Emmanuel Nchimbi KAJIMALIZA rasmi pale alijaribu KUMFIA mfadhiri wake ndani ya Kamati Kuu ya CCM. Hadhi yake ndani ya CCM imeporomoka. Aliyempinga ndiye kapendekezwa na Chama. Kwa hiyo kama JPM akifanikiwa kuwa raisi na mwenyekiti wa CCM, basi Nchimbi akalime maparachichi na matiki maji huko Matimila!
 
mpuuzi sana huyo hata siku moja hajawai kukanyaga jimboni toka 2010. Mbinga pia wamchinjie mbali
Kweli. Nyasa walimchinjia mbali.Sasa CC ya CCM wamemchinjia mbali. Kuwa bBalozi kutamfanya awe MBALI na shughuli za CCM.....
 
Back
Top Bottom