Dkt. Edward Hosea anatafuta nini Urais wa TLS?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,635
218,067
Kuna taarifa kwamba Mzee Edward Hosea ametia nia ya kugombea Urais wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS), bila shaka kama Mwanasheria anayo haki ya kugombea Cheo hicho.

Bali kwa mtu aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kuja kuomba kura ili awe Rais wa TLS, ni lazima watu wenye akili timamu tujiulize malengo yake hasa ni yapi, TLS inajulikana kwa kazi zake za kupigania haki ili kuhakikisha nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria, huyu Hosea anao uwezo wa kupigania haki za kisheria ikiwemo kuielekeza serikali aliyoitumikia kwa miaka mingi?
 
Miongoni mwa wagombea wote wanne, binafsi sijaona mwenye azma ya kweli na nia ya dhati kuiongoza TLS

Hivi kwa mfano Msando anagombea ili iweje....au ndo wanasheria/ mawakili wamekoswa kabisa mtu smart wa kuwaongoza?

Ngoja chama kichukuliwe na "siri-kali" ndo wataelewa
 
TLS. Moja ya taasisi zilizokuwa under attack miaka ya hii karibuni. Kuanzia kujaribu kuwachomekea viongozi ambao wanajulikana kabisa ni wafia CCM, mpaka wanachama wake ambao ni outspoken kuundiwa mizengwe mbalimbali.

Kama anagombea kwa nia ya kuwahujumu. Then waliomtuma can add this also to the list of their failures. Hawatafanikiwa.
 
Wadau walishamuibua huko 👇🏾...
 
Wadau walishamuibua huko 👇🏾...
Asante sana
 
Na msaliti mzee wa MIGA Lisu anashangilia sana.

Amefikia hatua ya kuionea aibu maiti kwamba kwa nini inaliliwa sana
 
Kuna taarifa kwamba Mzee Edward Hosea ametia nia ya kugombea Urais wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika ( TLS ) , bila shaka kama Mwanasheria anayo haki ya kugombea Cheo hicho .

Bali kwa mtu aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kuja kuomba kura ili awe Rais wa TLS , ni lazima watu wenye akili timamu tujiulize malengo yake hasa ni yapi , TLS inajulikana kwa kazi zake za kupigania haki ili kuhakikisha nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria , huyu Hosea anao uwezo wa kupigania haki za kisheria ikiwemo kuielekeza serikali aliyoitumikia kwa miaka mingi ?
Huyu alikwiba mapesa enzi ya jk,sasa hivi kaona afufukie kwingine
 
Back
Top Bottom